MHAINI
We olewa na yoyote, hunikomoi
Tena uende popote, hunikomoi
Kisha ufanye vyovyote, hunikomoi
Hata utoke na kaka, hilo sijali
Yaani uwe kibaka, hilo sijali
Tembea unapotaka, hilo sijali
Ni wewe na Mola wako, halinihusu
Ubaya ni juu yako, haunihusu
Ikiwa mema ni yako, hayanihusu
Aibu ni yako wewe, sio ya kwangu
Kaburi ni lako wewe, sio la kwangu
Si mtu wewe ni mwewe, si kosa langu
Talaka yako chukua, ondoka ndani
Waume wawachukua, ni mhaini
Maradhi utaugua, ondoka ndani
Wanangu unawaacha, toka wewe tu
Wafanana na pakacha nenda wewe tu
Sitaki kuziba pancha,nenda wewe tu
Abuuabdillah [emoji1621]
0744883353
Moshi,Tanzania