Hata wakipiga kitabu ni kazi bure kwani mwisho wa siku atawapa 0%, wamdhibiti asiaribu maisha yao
Ninyi vijana acheni uvivu, kaeni chini mpige shule. Hakuna mtu yeyote atakae wabadilishia mwalimu. Acheni kuzoea shule lainilaini. Nendeni Library someni sana muelimike vizuri. Hamuwezi kuwa discontinued!!. Mimi pia ni mwalimu wa chuo kikuu. Hizo ni strategies za kuwafanya wanafunzi wasome kwa ku concentrate. Watu wengi huwa hawawezi kusoma bila ongoing pressure, na ndo maana huwa mitihani ikikaribia huwa watu wanasoma sana, sasa kwa nini soma ile isiwe kuanzia mwanzo wa semester?. Mimi mwenyewe nilipokuwa nasoma nilikuwa naambiwa hivyo hivyo, "darasa hili ni dogo sana na nyie watu ni wengi lakini tutajua cha kufanya". Mkitoka hapo kila mtu anasambaa liblary. lakini mnajikuta watu mnafaulu, ikitokea kukamatwa au disco hata watu wengine wote, deep down mnaona kabisa kuwa mwenzetu huyu alistahili. Si mnafahamu kufeli university is not accident, Huwa mtu unaona kabisa kwamba somo hili ninafeli, kwani Continous assessments huwa zinakuonesha kuwa unakoelekea ni kufeli. Na mtu akifeli maana yake ni mjumuisho wa CAs na UE. So kaeni chini msome muweke sawa hizo CAs. The quality of education should not be left to be compromised by students' politics. Kama mnataka kusoma ingieni madarasani msome.
Kumbukeni University, pamoja na kufundishwa taaluma zenu, pia mnafundishwa namna ya kukabiliana na changamoto za kimaisha. Siyo unatoka hapo hujapigwa stress hata kidogo, unaenda uraiani unapata challenge kidogo unakimbilia kujinyonga, badala ya kutumia akili na uvumilivu kutafuta ufumbuzi.
So kupigwa zero is part of life, kaeni msome. Hata hao waalimu wenu iko siku moja chuoni kwao walipata maksi za ajabu i.e single digits, wakaongeza bidii na ndo maana leo wako hapo. Sasa nyie endeleeni kulilia miteremko muone mtaishia wapi.
Mwisho kabisa natoa wito kwa mwalimu muhusika kama utasoma hii thread, nakuomba uzidi kukaza kamba, kwani hii ndo njia pekee itakayowafanya vijana hawa wasome kwa bidii na kutoka wakiwa na elimu ambayo watanzania wanatarajia watakua noyo. Napia walimu wengine wa vyuo tujitahidi kuwaweka bize vijana hawa kwani ndo namna pekee ya kuwafanya wafungue makaratasi kwenye vitabu.