Mhadhiri Bashir Ally (UDSM) Atafutiwe Jimbo!

I knw the Guy in and out,we unambeza kwa kuangalia paradigm ya mijadala ya TV na redio una bahati mbaya sana.
Bashiru ukiachilia kukulia mikononi kwa pro.Haroub Othman (R.I.P) baada ya kufariki akaendelea kuwa chino ya Prof.Issa Shivji.
Bashiru Ana maandiko yake mengi tu,nakushauri ukayasome na ujitahidi kuelewa msimamo wake juu ya mustakabali wa taifa hili.
Binafsi ninamjua kama ni mjamaa,mzalendo,mtaifa na asiyeona haya kuusema ukweli bila kujali ni mchungu kwa kiasi gani.
Mwisho,aendelee kuwa mhadhiri ( taaluma) bungeni wataenda wengine maana kwa ninavoona awamu ijayo wataenda wazuri wengi sana watakaotuwakilisha kwa upana sana. yeye tukihutaji mawazo yake tutayapata vitabuni na kwa wachambuzi wengine anaozalisha pale mlimani.
 

nilikuwa naangalia kipima joto leo cha itv nna imani kuwa huyu ni yule nlimuona kule akitoa hoja zake(i stand to be corrected)..turudi kwenye mada...binafsi niko pamoja na mleta mada kuwa watu wenye ufahamu mkubwa kama hawa ndio wanatakiwa waingie katika nyadhifa za uongozi kwa sababu wataweza kutoa maamuzi sahihi kutokana na ujuzi wao...nifupishe tu na niseme kuwa tunahitaji wahandisi(engineers),madaktari(medical doctors) na wataalamu wengine katika nyadhifa muhimu kama bunge. Ni miongoni mwa makosa wataalamu wengi wanafanya kwa kuacha siasa then wanakaa kulaumu viongozi mara vilaza mara vihiyo wanasahau kuwa wao ndo walikosea kwa kutotafuta uongozi WITO WANGU:let us STOP making STUPID people famous
 
Nchi hii watu wanasoma ili wawe wanasiasa? ...why why why my country? Prof Anna Tiba, Mwandosya, Hemed Msolla et al. Yani uprof wenu mnaiexercise bungeni ambako hata non-elite anaweza perform?



 
Ni kati ya wasomi makini sana. Hata mimi nimekuwa nikimfuatilia kwa muda mrefu. Ingawa simshauri kujiunga na vyama vya upinzani maana huko nilishapoteza imani nao, ni kama kuna wachumia tumbo na wala sio wanamageuzi wa kweli kama tunavyofikiria. Simshauri kupoteza Heshima yake amabayo ametumia muda mrefu kuijenga. Anaweza kujiunga na CCM bado akawa chachu ya mabadiliko ndani ya hicho chama au akaendelea na kazi yake akiwa mtaalamu anayetoa ushauri bila kuegemea upande wowote.
 
I knew it'd turn out this way! There is nothing nowadays that could be discussed in here regarding Tanzanian society without this :'udini' thing, especially when a muslim or muslims are part of the subject. The stone age still exists.

Wewe hujaona hao aliwa-cc....it tells all
 
Anatoka Bukoba. Unashangaa nn?

wewe ni mkabila sana ndugu yangu na ntakupa mifano mingine ili ukatafiti tujue na hao watu kama wanatokea huko Bkb

jamaa anaitwa Afande Mkisi pale Jiteute twambie anakotoka

jamaa anaitwa Prof.Maghembe waziri wako twambie anatoka Bkb upande upi?

jamaa anitwa Mwigulu Nchemba naye utwambie anatokea Bkb sehemu gani?

ukimaliza hao list ni kubwa tutaomba utusaidie na wengine
 
Nakupa changamoto moja. Nchi ya Tanzania mpaka sasa imeongozwa na maraisi wanne (4): wawili wakristo na wawili waislamu. Hebu kuwa mkweli na utuambie ni viongozi gani walioonesha uhodari wa kuongoza na kusimamia maslahi ya Taifa, badala ya kuporomosha matusi hovyo humu jamvini! Hata kwa huyo mteja wako unayemnadi hamna kitu hapo. Huo ni umaarufu wa kuonekana kwenye runinga tu ambao hata "LULU" wa marehemu Kanumba anao!

Katika hii dunia ukiona mtu anajali usafi wa nguo alizovaa badala ya mwili wake-huyo mtu ni hatari sana manake akili zake haziko sawa!

 
Dah!! Hatuishi vituko watanzania. Ngozi ya fisi haijifichi hata akijichanganya na kondoo.
 
haha..mmeshafikia hapo?Si wa kile kitengo cha wapiga matarumbeta wa kukodi toka chuo kilichoipa nchi hasara UDSM.?Haha...napita tuu.

Hapo kwenye red: Unamaanisha Dr. Bashiru yupo kwenye kundi la Dr. Benson Bana; yule mpiga tarumbeta maarufu wa Lumumba? Kama yupo kwenye kundi hili naye hana maana zaidi ya wachumia tumbo.
 
Wanazuoni wabaki kwenye taaluma zao ili wakosoe mamlaka zilizoko madarakani. Wakiingia kwenye siasa wengi wao hugeuka kuwa vipofu baada ya kulambishwa peremende zipatikanazo huko kwenye siasa.
 
And the only reason Bashir anaonekana kuwa bora ni kwa sababu anapewa airtime ya kutosha na vyombo vya habari mbali mbali huku akiwa anazungumzia mambo ambayo jamii ya watanzani iko addicted kwayo: siasa, chadema vs ccm, 2015 nani atakuwa nani, well, na ugaidi wa kitaifa na kimataifa.

Lakini kuna other unsung academic heros. Hawa hawapewi airtime zozote zile na kwa hiyo watanzania hawawajui kabisa na pengine ni wataalamu wa fani ambazo watanzania hawajui kuwa ni muhimu kuliko hata siasa.

Hivi kwa nini vyombo vya habari haviwezi siku moja kwenda kwenye vyuo vyetu vikawapa airtime baadhi ya maprofesa tofauti na Ayoub Rioba, Bensoni Bana, Mukandara na huyu wa leo, Bashiru Ali? Siasa bongo?
 

I do not call this guy msomi nadhani he is a looser anaye amini kwamba CIA walilipua Kanisa Arusha wakitaka kutuchanganya ili wachukue gas nk na huku anawalinda wa China .Huvu huyu ana chuki hivi huko UDSM anafundisha kutumia lugha gani ? Mdini mkubwa huyu hope anatumia kiarabu kufundisha huko na si Kiingereza .
 
huyu nshomile mwenzangu anaweza kabisa, akija bukoba vijijini kura za itahwa, maruku,katoma zote zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…