Mhadhiri ashauri shule binafsi zitozwe kodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhadhiri ashauri shule binafsi zitozwe kodi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by pareto 8020, Apr 22, 2010.

 1. p

  pareto 8020 Member

  #1
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wednesday, 21 April 2010 19:39
  Felix Mwagara na Minael Msuya

  HASARA ya Sh752.4 bilioni iliyopata serikali kutokana na misamaha ya kodi imewakera wasomi na wanasiasa ambao sasa wameitaka iifute misamaha yote ya kodi ambayo haina tija.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, walisema hali hiyo haivumiliki kuona nchi ikiendelea kupata hasara kiasi hicho wakati bado ni maskini.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alimtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Cag) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (Tra) kuangalia vyanzo vingine vya kodi na kuifuta sheria ya misamaha ya kodi kwa kuwa haina tija wa taifa.

  Dk Bana ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Sayansi ya Siasa na Uongozi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alitoa kauli hiyo jana wakati akiwa anatoa maoni yake kuhusiana na serikali kupoteza Sh752.4 bilioni katika makusanyo yake ya kodi kutokana na kutoa misamaha mbalimbali ya kodi kwa watu binafsi, taasisi na wawekezaji wakubwa wa sekta ya madini.

  Cag, Ludovick Utouh juzi mjini Dodoma aliwaeleza waandishi wa habari juu ya ripoti za ukaguzi wa serikali za mitaa, serikali kuu na ukaguzi wa mashirika ya umma.

  Dk Bana alisema serikali inatakiwa itoze kodi shule za binafsi ambazo zinalipisha wanafunzi ada kubwa hali inayosababisha wamiliki wa shule hizo kupata faida zaidi ikiwa wanajipangia ada hizo kadiri wanavyopenda hali ambayo ni tofauti na shule za serikali ambazo zinajulikana.

  Alisema baadhi ya shule inamlipisha mwanafunzi kwa ada ya mwaka mmoja tu zaidi ya milioni tatu wakati mwanafunzi wa PhD chuo kikuu anatoa milioni mbili inakaribia na nusu.

  ================================================================================


  Wakati nakubaliana na hoja ya msingi juu ya serikali kupunguza misamaa ya kodi ili kuongeza pato lake, ninatofautiana na Mwalimu Bana katika hoja yake ya kuzitoza kodi shule zote (binafsi, serikali etc).
  Misamaa ya kodi katika sekta ya elimu, ndio imevutia uwezekaji katika sekta hiyo ambayo kwa muda mrefu uwekezaji umekuwa ukifanywa na serikali na mashirika ya dini peke yake. Ukweli ni kwamba ilifika mahala mzigo ulikuwa mzito kwa serikali ndio maana milango ikafunguliwa watu binafsi wawekeze katika shule. Mwalimu Bana atakubaliana nami, taifa lisilowekeza katika elimu, mwisho wake si mzuri hata kidogo. Na uwekezaji katika elimu hauna mwisho…ndio maana mpaka leo Marekani pamoja na maendeleo makubwa waliyopiga katika kila Nyanja, wanaongelea umuhimu wa kuwekeza zaidi katika elimu ya msingi na sekondari….leo hii wanahofu tatizo la viwango vya elimu, wana hofu upungufu wa waalimu wa sayansi na hesabu katika mashule…..sasa kama marekani inahofu…sisi tusemeje.

  Sisi bado tupo nyuma sana katika sekta ya elimu..actually tulishawahi kufika mbali, lakini sasa tumerudi nyuma…in terms of ‘education standards’. Leo hii, tuna upungufu mkubwa wa waalimu, vifaa vya maabara na vitabu na fedha zilizopo hazitoshi. Last week tumesikia Mkuu wa Nchi akisema zinahitajika 1.3Billion USD, kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu…. Until that is figured out, attracting Private Capital katika sekta ya elimu bado ni muhimu sana katika kuendeleza sekta hii MAMA. Na tax incentive….ni mbinu moja wapo ya ku attract private investment katika sekta ya elimu. FAIDA yake tutaiona mbeleni zaidi…..

  Hii hoja ya Mwalimu Bana ya kwamba fees za Private schools zipo juu sana ndio maana zinastahili kutozwa kodi kwa mtazamo wangu ni simplistic argument. Kufanya benchmark ya fees za private schools na public schools or universities ni makosa makubwa kama haujafanya student unit cost analysis. Ni lazima ku establish, what it takes to train a student…..hapo lazima uchukue costs zote..vitabu, vifaaa, mishahara, umeme, mafuta etc…ndio ujue gharama halisi ya kumfundisha mwanafunzi…

  Kwa vyovyote vile zitafotautiana baina ya shule na shule kulingana na costs zao. Kama shule moja ikiamua kumujiri mwalimu aliyesoma vizuri mwenye credential kama za Mwalimu Bana Bachelor of Education (B. Ed.-First class Hons.), Master of Arts (M.A) (Political Science & Public Admin.) na Phd….kwa vyovyote gharama zake katika soko zitakuwa kubwa zaidi ya mwalimu aliyemaliza Form IV akapata crush-programme training ya miezi mitatu na kuingia darasani. Kwa msingi huo, utaona ulazima wa kuwepo tofauti ya fees katika ya shule moja na nyingine.

  Isitoshe, kulinganisha fees za Private na Public schools ni kukosea sana….kwani hizi private zinajitegemea 100% kujiendesha…hizi za public…..zipo subsidized. Hivi Mwalimu Bana anadhani gharama halisi ya kumfundisha Phd student ni 2.5 Million kweli? Leo hii pale Faculty kwake, serikali ikiacha kuwapa subsidy za kulipia mishahara, umeme na staff development programme….ataweza kuendesha Faculty kwa ada ya 2.5 Million kweli? Is that the real unit cost za ku train mwanafunzi?


  Makosa ya aina hii ya Dk Bana hufanywa na watu wengi hasa policy makers kwa kutoa takwimu za juu juu bila kufanya in-depth analysis….ndio maana mtu anaweza kukutana na mfadhili akamuuliza ninahitaji kukusaidia ku trains wanafunzi wako 10, niambie gharama zake….mtu anakimbilia kutaja rate iliyo subsidized…mwishowe…anapewa pesa hizo, na zinamshinda kutrain watu hao kama alivyotakiwa kwasababu hakuzingatia gharama halisi.

  Mimi nadhani cha kutilia mkazo ni ‘STANDARDS’ shule zote, ziwe za public au Private lazima ziwe na viwango vya kuwawezesha kutoa elimu bora. Na ikibidi, kuna haja ya kuangalia upya utaratibu wa ku examine wanafunzi wetu…mfumo wa sasa ume prove failure. Hivi hatuwezi ku harmonize standards zetu na nchi zote za East Africa, na wanafunzi wetu wakatainiwa kwa kutumia mtaala mmoja…. Ninasema EAC kwasababu tunapokwenda huko mbeleni, products zetu ndio zitashindanishwa na wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi katika labour market…na kwa mfumo ulipo sasa, sidhani kama vijana wetu wapo prepared kushindana na wenzao.

  Aidha hizo Private Schools ziwe scrutinized kuhakikisha zinatoa elimu bora, na sio ubabaishaji, maana kama alivyokwishawahi kusema Mzee Mwinyi..unapofungua milango hewa iingie….hata inzi na mbu nao huingia….. Tu identify hao inzi na mbu, tuwatoe ndani ya mfumo.

  Mwisho, my advice to Mwalimu Bana, akiwa msomi mahiri, tena kijana…ajiwekee utaratibu wa kufanya research kabla ya kutoa matamko kwenye media....maana it seems yeye ni opinion leader katika media yetu...basi atutendee haki kwa kutoa matamko yaliyo balanced and well –researched na sio kukurupuka kama wanasiasa na kutoa simplistic arguments based on insight with zero analysis. He can take a cue from Late Prof Chachage na waalimu wengine makini kama akina Prof Shivji.

   
 2. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280


  Tukubaliane kwamba Jambo hili halihitaji utafiti wowote mkubwa. Hata hivyo siamini ktk maisha yangu kwamba kila utakapofanya utafiti basi umepata jibu.

  Kwa yeyote mwenye mtoto ktk shule hizi anfahamu fika kwamba hazitoi huduma. Ni biashara. Kwa nini hutaki biashara ilipe kodi?

  Ada zinazolipwa ktk shule hizi ni exorbitant. Ni sawa kwamba anayedhani ana uwezo kulipa ada hizo alipe. Fine! Lakini pia anayepokea fedha hizo lazima atozwe kodi.

  Naomba usiwatetee wakati wamiliki wakifahamu wanafanya biashara. Let them pay KODI. period
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Aina hii ya wasomi hasara tupu .. kuropokaropoka na uvivu wa kufikiri.
   
 4. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  ==========

  Walio karibu na Dr. Bana wamshauri afikirie upya juu ya matamko yake.
  Kwa maoni yangu, hana tofauti na Lyatonga Mrema kwa sasa. Inaonekana sasa kila jambo likitokea lazima aseme na mara zote anakuwa off point.

  Wastani wa karo za private kitaifa ni shs milioni moja kwa mwaka, yaani ukiunganisha zote nchi nzima. Tanzania ya leo, nani atakubali umlipe shilingi milioni moja, akusomeshee mtoto wako mwaka mzima? Humo kuna Chakula, malazi, matibabu, mafunzo, mishahara ya walimu, umeme, maji, n.k.

  Mi nadhani serikali inahitaji kufikiri haraka na kuzipa ruzuku ili ziweze kuboresha zaidi maana kama zikiondoka hapa nchini, ni sawa na hatuna tena elimu. Yeye Bana mwenyewe watoto wake wako huko.
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Apr 22, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,592
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Usimfananishe Lyatonga na Bana, Mrema kamuacha mbali kabisa Bana, wala Mrema usimweke kwenye hilo kundi please mpe credits zake is unsung hero, vizazi vijavyo vitamuita hivyo

  Ruzuku? pengine hujajua serikali yako haitakuja kufanya hivyo hata utimilifu wa dahari, however, RUZUKU kwa shule is one of the best idea ever! and I fully support it for 100% ,lakini tuondoe ruzuku kwenye vyama vya siasa!

  Ruzuku kwa mashule in direct impact au correlation na maendeleo ya nchi, wakati ruzuku kwa vyama is simply wastage of money
   
 6. p

  pareto 8020 Member

  #6
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu nakubaliana na hoja kwamba kila biashara lazima ilipe kodi. Hata hivyo, kuna circumstances nyingine kukawepo objectives nyingine na zenye manufaa makubwa kwa taifa sasa na baadaye ambazo zinaweza kupelekea ku forego malipo ya kodi in anticipation kwamba faida itakayopatikana kutokana na shughuli hizo ni kubwa zaidi. Nadhani hakuna anayebisha kwamba FAIDA ya elimu ni kubwa kwa taifa lolote lenye malengo ya kuendelea. Ndio maana leo hii kwa kutambua umuhimu wa maendeleo ya teknolojia, kompyuta ziko exempted kwenye tax....na faida yake kwa maendeleo ya teknolojia ni kubwa nchini...lakini that does not mean wale jamaa wa Computer Centre Ltd samora hawatengenezi profits....na haimaanishi kwakuwa wanafaidika, basi kodi irejeshwe kwenye computers.

  Ni umuhimu huo wa elimu, ndio unapelekea hata mataifa yaliyoendelea kama Marekani leo hii Maryland sio tu wanatoa tax exemption kwa Private Schools, bali wamefikia hatua ya kutoa ‘Tax Credits’ ambapo shule hizo zinaruhusiwa kufanya fundraising kwa makampuni makubwa ya hapa, then makampuni hayo yanaruhusiwa kulipa kodi less amount waliyo donate katika private school.

  Hata Uingereza napo Private Schools zao (Independent Schools) zina option ya kuwa na charitable status. Kwa mwaka mmoja shule hizo zinapata tax relief ya kiasi cha pauni za kiingereza £100 milioni. Wote hawa wanaona faida ya ELIMU. It is on the same reasoning hata Tanzania inatoa tax exemption kwa shule za binafsi. Ukiangalia difference ya fees ya hizo private schools za UK kwa mfano na public schools utapata picha- mfano mtu anayekwenda Private School UK, analipa Pound 3900 per term kwa day school na Pound 7748 kwa boarding school kwa term (source http://www.isc.co.uk/FactsFigures_SchoolFees.htm).. Gharama hizi kwa hali yoyote zipo juu, lakini zinazingatia costs ya kuendesha shule kwa viwango vya juu. Kwa upande wa Public Schools japo zinaonekana kuwa chini ya hizo za Private School, a large chunk of expense za shule za public ziko subsidized na serikali...amount ambayo ukijumuisha zote, cost hazipo mbali sana na hizo za private.
  That said, I agree zipo shule bogus zinazo over-kill kwa fees wanazotoza na kutoa substandard education....that is why ni lazima ziwe regulated na kuwa monitored uendeshaji wake. I think Wazazi na Serikali ndio watu wa kwanza wenye kutakiwa ku detect hiyo weakness .....utakuwa mtu wa ajabu unayekubali kutozwa pesa nyingi wakati unapata substandard service then ukaendelea kumpeleka mtoto wako katika shule za aina hiyo.......wazazi wakiondoa watoto wao......definately shule hizo bogus zita disappear zenyewe kwa kukosa wanafunzi...au kukiwepo mfumo mzuri wa kuzi regulate basi zitaweza kufungwa punde zinapobainika ni za ubabaishaji.
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Private schools ni biashara kabisa kama biashara zingine. Zitozwe kodi.
  Nakubaliana na Dr kwamba misamaha ya kodi imekuwa mingi kiasi kwamba serikali inapata mapato kidogo sana na inakuwa vigumu kupanga mipango yake ya maendeleo kwa hakika.
  Serikali ifunge macho. Kila mfanya biashara alipe kodi. Hii haina mjadala. Walipe kodi. Tunaitaji maendeleo na bila kodi tutapata maendeleo hayo wapi kwenye kila mtu kuhitaji msamaha?
   
 8. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  zitozwe kodi kwasababu gani? kwasababu nyingi zinamilikiwa na wakristo na watu wengine wivu unawajaa au nini?, badala ya kuongelea suala la kutoa subsidies zaidi, anaongelea kutoza kodi tena, msomi wa wapi huyo jamani. selikali imeshindwa kujenga mashule mazuri, watu binafsi wanaifundisha selikali naman ya kuendesha shule na watoto wakaelewa. ubavu huo selikali haina, cha muhimu ni kuhakikisha wanatoa ruzuku zaidi kwenye shule hizi ili zipanuliwe na kukua zaidi, kwasababu zinasomesha watoto wa dino zote bila kubagua. naongea hivi kwasababu hii issue imekuwa kwa muda mrefu ikijadiliwa kidini zaidi, na imeunganishwa na issue ya huduma zingine za jamii kama mahospitali etc, wengi walipiga kampeni vitu vyao vitozwe kodi, si kwasababu ni muhimu, ila ni kwasababu wanaamini kuwa vingi vya vitu hivyo ni vya wakristo. radio fulani za kidini zilikuwa zinalalamika hata hospitali ya mwanza tu, kwamba wakienda kulazwa hawataki kuona misalaba kwenye vitanda au vyumba, lakini ni hospitali ya wapenda misalama, wapenda mwezi na nyota hawana uwezo wa kujenga au kuchangia ujezi wa hospitali au shule. acheni wivu kwa lwakatale, acheni wivu wa mashule mazuri, acheni wivu wa kidini. kama ni shule, zinasomesha watoto wa dini zote, hospitali zinatibu watu wa dini zote. IMAGINE KAMA WAKRISTO WASINGEKUWEPO TZ, si pasingekuwa hata na hospitali bora moja, au hata shule bora moja, WATU WANGEKUWA WANAPANGA FOLENI KWA SHEE YAHYA TU. achana na kina muhimbili. acheni wivu bwana, pelekeni watoto shule wakafaidi, KAMA WEWE HAUNA UWEZO WA KUMPELEKA MTOTO WAKO SHULE YA HELA, nyamaza kimya, mpeleke buguruni shule ya bure. wenye uwezo wanapeleka shule za juu. wewe tafuta pesa ili watoto wako waende huko pia. usione wivu kwasababu watoto wa wenzio wanaenda shule bora, utakata muwe sawa, hiyo haiwezekani hata siku moja. imagine kama wakileta kodi zao, HAO WENYE SHULE WAKABADILISHA BADALA YA KUWA SHULE, WAKAAMUA IWE HOTEL, AU WAKAFUTA SHULE WAKAJENGA VITU VINGINE VYA KUPATIA PESA, UTAFAIDI NINI? acha fikra za kiujamaa, tupo kwenye capitalism sasahivi, hautakuja uwepo usawa hata siku moja. mwenye nguvu apata, asiye na nguvu atakosa, labda subirie fadhila za mwenye nguvu. period.
   
 9. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2010
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hii shool of thought ya kutumia kodi kama kivutio cha uwekezaji inanipa tabu sana. Essentially hii inaiweka nchi katika wakati mgumu sana kwa kuvuruga mfumo wa kifedha. Taasisi zinazolipa kodi na zisizolipa kodi zote zinafanya kazi ndani ya nchi moja, tena yenye uchumi dhaifu sana. Maana yake ni kuwa wale wanaolipa kodi wana-end-up kulipa makodi makubwa sana kwa sababu wengi wana sababu hii na ile ya kukwepa kodi. Ndo maana tunaelekea kwenye migomo ya wafanyakazi. Huu mzigo wa kodi unawaangukia wafanyakazi kwa sababu serikali imekuwa 'mama huruma kwenye kodi'. Taasisi za dini hazilipi kodi, Taasisi za kutoa misaada hazilipi kodi, Balozi zote hazilipi kodi, mashirika ya kimataifa hayalipi kodi, Viongozi wakubwa wa nchi wana misamaha kibao ya kodi, mapato makubwa ya wafanyakazi wa ngazi za juu na kati serikalini kupitia posho mbali mbali hayakatwi kodi, Migodi ya dhahabu hailipi baadhi ya kodi, Makampuni yanayoingia nchini chini ya sheria ya TIC halipi kodi kwa kipindi fulani, n.k.

  Hilo ni eneo kubwa sana la kodi kwa nchi maskini kama Tanzania ambayo haina viwanda vingi. sasa ni nani atalipa kodi?? Tunaiga nchi zenye viwanda na biashara kubwa kubwa nyingi ambazo zina wigo mpana wa kodi. Tunaiga kunya kwa Tembo. Matokeo yake ni kuwa wanaoangukiwa na rungu la kodi ni watu wachache sana hasa wafanyakazi tena wadogo wadogo. Wafanya biashara wachache waliopo wana njia nyingi sana za kukwepa kodi.

  Hali hii si nzuri kabisa. Kodi ndo mapato ya serikali. Serikali hii hutumia gharama kubwa kuwahudumia watu wanaolipa kodi na wasiolipa kodi. Nani sasa alipe kodi?? Ni lazima taifa hili liangalie hii balaa. Mlipa kodi ni yule yule kila mwaka na wengi wanazidi kutafuta jinsi kuingia kwenye misamaha ya kodi. Makampuni yanayosajiriwa chini ya sheria kama ya TIC kila baada ya miaka mitano hubadili majina au kuanza upya ili yaendelee kunufaika na misamaha minono ya kodi. Ninakubaliana na Bana, hali ni mbaya mno. Misamaha ya kodi ni mingi mno kiasi kwamba kulipa kodi Tanzania unaonekana ni Ujinga. Ndo maana hata wale wanaotakiwa kulipa kodi wanatafuta kila njia za kuikwepa!!

  Lazima tuwe makini. Tufute misamaha yote ya kodi. Mzigo kwa mlipa kodi itapungua. Zile taasisi tunazoona ni za muhimu sana kuwa haziwezi kuwepo iwapo tunazitoza kodi, ni afadhali zipewe ruzuku. Misamaha ya kodi itaiangamiza Tanzania.
   
 10. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Wakuu nadhani tunatakiwa tuwe makini sana kuangalia hali ya elimu katika nchi yetu na madhara yake huko mbele. Misamaha mingine yote kama alivyoorodhesha KipimaP hapo juu ingestahili iondolewe au ipunguzwe lakini mashule yaachwe yasiguswe na badala yake yasaidiwe zaidi. Mkwa mtazamo wangu kama serikali ikiweza kuhakikisha kuwa kodi inayokusanywa inakusanywa sahihi na kodi hiyo inatumika vizuri ipasavyo, siyo kununua mashangingi kila leo, ndege ya Raisi, Radar wananchi wanaambiwa hata tule majani lakini nini? ndege inunuliwe! kumbe ni madudu matupu! Kwanza tunataka "a strong system of collection and then a strict national budget committee". Tukiweza kuhakikisha hivyo basi tunaweza hata kujikuta tunayo surplus hata tusihitaji kuwa na hizo shule za private basi. Maana serikali itajenga nyingi na kuzihudumia vizuri nani atapoteza pesa yake basi kupeleka mtoto wake private? Kinyume chake wakitozwa wataongeza tena sehemu ya hiyo kodi kwenye ada. Kusema kweli tukijilinganisha na nchi zilizo jirani bado ada za shule Tanzania ziko chini sana tena sana. Na nadhani ni kwa sababu serikali imezipa msamaha wa kodi. Kwakweli hapa na mimi naona Dr. Bana hapa kakurupuka. Afanye utafiti wa kutosha atuletee hapa, aende shule mbili tatu awaombe kufanya utafiti wa gharama za kumsomesha mtoto kwenye shule yenye hadhi inayohakikishia mtoto at least a standard education atuletee hapa. Nadhani ataona aibu kurudi na kuendelea na madai yake. Tatizo kubwa sana nchini Tanzania kwa wasomi na hata wananchi wa kawaida, wanasiasa ndiyo zaidi, tunatoa mawazo au mapendekezo yasiyo na utafiti kwenye jambo lenye uzito mkubwa sana kitaifa pasipo kuzingatia utaalam. Mara nyingi inatokana na chuki binafsi, kero ya kipato kidogo, wivu au simply kujidhania kuwa watu hawana upeo kama wao na zaidi wa kutafakari mambo (wanasiasa hao).
   
 11. T

  Tom JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ruzuku kwa shule ni kitu kizuri sana, lakini jinsi nchi inapokua na uchumi mkubwa na uwezo wake kutoa ruzuku utakua, kwa hali ya uchumi tuliyonayo sasa vema hayo mashule yakatozwa kodi.

  Hivyo ili kuinua uwezo wetu wa kutoa ruzuku na basi tukuze uchumi wetu kwanza. Jambo la maana sana kuwafutia kodi exporters kwa njia ya KULIPA KODI KWANZA na KURUDISHIWA sehemu au yote baadaye baada ya malipo toka kwa mnunuzi kukamilika - mabenki yanajua hesabu zote. Mashine na mafuta kwa ajili ya migodi ya dhahabu walipe kodi kwani tunajua kabisa faida wapatayo, ambapo kama Mchuchuma itakuwepo na basi hao mtaji wao tunaweza samehe kodi kwa vipindi tukiangalia upepo. Ni kukabiliana na mambo kama hali inavyoruhusu ili kuhakikisha mapato yanakua, migodi inaendele kujengwa, nk.

  Sasa hivi shule zinaongezeka sana kuliko hata vitegauchumi, mwisho kila mtu atakua msomi wa kuranda randa tu, tuunahitaji na nguvu kazi vile vile.
   
 12. p

  pareto 8020 Member

  #12
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na Tom kwamba nchi inakuwa katika hali nzuri zaidi ya kutoa ruzuku inapokuwa na uchumi mkubwa…..lakini with or without uchumi mkubwa, kila nchi inalazimika kufanya baadhi ya mambo yenye kuleta chachu na ustawi wa maendeleo yake. Uwekezaji katika elimu, ni eneo moja ambalo kila nchi duniani (masikini kwa tajiri) zinawezeka ili kujihakikishia huo ustawi tunaoungelea. Actually, unapokuwa masikini ndio unatakiwa kuongeza juhudi mara mbili kuhakikisha elimu kuwa ndio chanzo cha kujikomboa.

  Sikubaliani na hoja yako kwamba SHULE ZIMEONGEZEKA SANA (which implies zimezidi), ukweli ni kwamba hata hizi zilizopo hazitoshi… we need more schools…. Kufuatia ile program ya serikali ya Primary Education Development Plan (PEDP) ua (2002-2006)….idadi ya wanafunzi wanaomaliza shule za msingi ni about 7.5 Million….. capacity ya shule za sekondari by the time program hiyo imekuwa full-swing ilikuwa ni kupokea wanafunzi 345,000…. Hii initiative mpya ya shule za sekondari za kata ndio ilikuwa projected kuongeza idadi ya capacity ya enrolment kufikia 2,000,000. Kwa hali hiyo bado kuna pengo la nafasi za sekondari zinazohitajika kama 5.5 Mil…. (ukitaka details zaidi ya takwimu hizi nenda kwenye site: http://webcache.googleusercontent.com/search?q=cache:cRN0uH-HyYUJ:www.cedol.org/cgi-bin/items.cgi%3F_rm%3Ddisplay_blob%26_data%3D200612191720372337+total+primary+school+enrollment+in+Tanzania&cd=3&hl=en&ct=clnk&gl=uk

  Under such circumstance, unakweza kudai kweli kwamba shule zimekuwa nyingi….zinatosha? Hapo kwakweli tutatofautiana….BADO TUNAJITAJI mashule zaidi na zaidi na zaidi…..wadau wengine kama makanisa, misikiti, watu binafsi, NGOs zinatakiwa kwakweli kuwa encouraged kuwekeza zaidi katika elimu sio tu katika mashule ya msingi na sekondari, bali pia kwenye Vocational Training na tertiary education ….na serikali iendelee kutoa incentive katika sekta hii ili wajitokeze wengi zaidi…we still have long way to go……
  Hivyo, vitega uchumi, Tom unavyoongelea, vinahitaji kuajiri wasomi….tusipowekeza katika elimu….wataishia kuja kuajiri wakenya na wanyarwanda..na sisi tutaishia kuendelea kulalamika….
   
 13. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naomba uangalie takwimu zako vizuri. Idadi ya Wanafunzi wetu wanaomaliza shule ya msingi kwa mwaka si 7.5M. Idadi yao kwa mwaka haifiki 1.2M.
   
 14. p

  pareto 8020 Member

  #14
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa kunisahihisha Sabi Sanda,,,,,what I meant ni total number of recruited student chini ya mpango wa PEDEP kwa kipindi kilichokuwa projected 2002-2006.... KWa hali hiyo output kwa kila mwaka itakuwa less than 1.2M kama ulivyo indicate...

  That said, bado hoja iko valid kwamba output katika primary education, hai match input katika secondary education na hivyo, investment katika mashule bado inahitajika kufanywa na wadau wote serikali, mashirika ya dini, watu binafsi na NGOs.... na incentive bado ni muhimu.

  Nashukuru kwa sahihisho.
   
 15. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,762
  Trophy Points: 280
  Personally sioni tatizo la hizi shule kulipa kodi. Tatizo linakuja pale tunapooanza kuulizana hiyo kodi imekwenda wapi na imefanya nini. Lets face it, Tanzania just like any other poor country, bila kupanua wigo wa kodi we aint going anywhere. Siku hizi kuna shule kumsomesha mtoto darasa la kwanza..ni zaidi ya gharama ya elimu ya University! na bado watu wanalalamika..Mimi naona shule kama hizo za akina "academies" (ambazo siku hizi ndo fashion kwa wenye uwezo) zitozwe kodi..na hiyo hela iwasubsidize watoto wa akina Masanja wanaosoma shule za Sikinde.

  Masanja
   
 16. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #16
  Apr 28, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Mkuu nimekurushia senksi yangu kuuubwa.
  Ukweli ni kwamba ni hela nyingi sana tunalipia watoto wetu huko St.mama yetu etc.
  Sasa kama ni hivyo haina budi nao walipe kodi pia.
  Kama mtu na nyumba yake ya kuishi anapaswa kuilipiaKODI iweje hayo mashule na mahotel na migodi isilipe?????
   
Loading...