Mhadhara wa Rais Sirleaf wazua jambo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhadhara wa Rais Sirleaf wazua jambo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 21, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]IJUMAA, JULAI 20, 2012 06:15 NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM

  MHADHARA uliofanyika juzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kuhudhuriwa na Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, ulichukua sura mpya, baada ya wanavyuo kutoka nje ya mada na kuelekeza hoja zao juu ya kukithiri kwa vitendo vya rushwa nchini.

  Kitendo cha kuelezea ufisadi na rushwa inayofanywa na baadhi ya viongozi ili kupata madaraka na kujilimbikizia mali, kilifanya wanyimwe kipaza sauti na kuielekeza kwa wahadhiri wanawake na wanaharakati.

  Mada husika, iliyokuwa mezani ni kujadili umuhimu wa mwanamke katika maendeleo ya Afrika na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

  Wananvyuo hao, walisema asilimia kubwa ya viongozi wa Afrika walio madarakani, wakiwamo wa Tanzania hawakutumia demokrasia kupata nafasi za kazi wakiwamo wabunge, zaidi ya kutumia rushwa na kumtaka Rais Sirleaf kueleza kwanini hali hiyo inashindwa kuzuiliwa.

  Kutokana na msimamo huo, mhadhiri mmoja wa kike alisimama na kusema hiyo si mada husika.

  Hata hivyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mkandala, aliamua kuachana na wanavyuo na kuelekeza vipaza sauti kwa wahadhiri pekee pamoja na wanaharakati.

  Katika mchango wake, Mkandala alisema kitendo cha Rais Sirleaf kutembelea UDSM na kufanya mhadhara ni historia ya kwanza katika chuo hicho.

  Kwa upande wake, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na pia ni Mhadhiri wa Kitivo cha Sheria wa Chuo hicho, Asha Rose Migiro, alisema maendeleo ya mwanamke katika Afrika yanazidi kukua kila kukicha.

  Alisema Tanzania kumekuwapo na sera nyingi za malengo ya MDGs hususan katika nyanja ya elimu, usawa katika ajira, mazingira, lakini utekelezaji wa kivitendo hauendani na mipango iliyopo.

  Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Ussu Malya, alisema ndani ya miaka 15 iliyopita, kumeanza kuonekana makundi mawili ndani ya jamii moja kutokana na mfumo uliopo wa kiuchumi.

  Akifanya majumuisho, Rais Sirleaf, alisema suala la usawa kwa wanawake barani Afrika bado halijafikiwa kiwango cha kuridhisha.

   
 2. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
  Hata wakificha maovu yao watanzania tumetambua,tumeelimika na tunajua haki zetu ni jambo la kusubiri 2015 hata watumie pesa zote walizonazo ni bure,njia wanazochakachulia tumezijua hakuna cha nec wala tiss-ni wachache wanufaikao na utajiri wa nchi yetu,Mungu anatupigania tuwashinde walanguzi,mafisadi,wa*aji,watesaji. Amen
   
Loading...