Mh Sumaye, Utamu wa Ngoma Ingia Ucheze... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Sumaye, Utamu wa Ngoma Ingia Ucheze...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hossam, Jan 7, 2012.

 1. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mh Sumaye,

  Ni imani yangu kubwa utaupata ujumbe wangu japo nina imani hautakaa sana hapa jamvini kwa kuwa ntatumia maneno makali kidogo.

  Nimekuwa nikifuatilia kauli zako siku nyingi bila kabisa kujua kama aidha ni kweli hayo yanatoka mdomoni kwako ama vipi. Kwa kifupi mkuu nchi hii tangu uache uwaziri mkuu kumekuwa na mabadiliko mengi ambayo nina hakika mengi huyatambui vizuri.

  Suala la posho ni sawa umesema kwamba litazua balaa kwa serikali ya JK lakini je una majibu gani kwa haya yafuatayo,

  1. Hakuna aliyeidhinisha posho mpya ya wabunge na wala Ikulu haijatoa tamko lolote kuhusu hilo, sasa je ni wapi wewe umepata uhakika kwamba posho mpya ziko payable hadi kupoteza muda kusema yasiyokuwepo?
  2. Wewe ulikuwa ni senior government officer, unajua fika ulivyokuwa unaheshimika na zaidk unajua namna nzuri ya kushauri mambo nyeti kama hili la posho za wabunge, je ulimshauri lini mheshimiwa rais kuhusu hili zaidi ya kulalama kwenye media!?
  3. Utata za posho za wabunge ulianzia hukohuko kwao, Makinda Mh, aliposema zinaanza kutumika Kashishila akasema hakuna kitu kama hicho, je wewe unapata wapi nguvu ya kuzusha mjadala na Nnauye ambaye kwa hakika halingani na wewe kwa ukada, siasa wala utambuzi wa hoja!
  4. Bunge ni mhimili na una itikadi na taratibu zake, je kwa kiongozi kama wewe kuendelea kulumbania hoja yake huoni kama unavuka mipaka?
  5. Taanzania ina madudu mengi mabovu, je wewe binafsi ni mangapi yamekukera na kuamua kutoa matamko kama kiongozi wetu?
  6. Suala la EPA, na Rada, na ndege ya rais je kwa mtazamo wako ni madogo kuliko posho za wabunge?
  7. CCM kwa mujibu wa Dr Slaa imejitengenezea report kwenda kwa wafadhili kuombaomba hela, wametoa mwenendo wa wizi wa EPA na marejesho ya wizi huo kinyume na maazimio ya kamati ya bunge, je hilo halifanyi wewe utoe tamko?
  8. Kwa makusudi kabisa, suala ya katiba mpya ya Tanzania limehujumiwa kutokea mwanzo, je wewe una maoni gani kwa hili? Ni dogo kuliko posho?
  9. Migomo na unyanyasaji wa wanafunzi vyuo vikuu na hata wale madaktari wa muhimbili hayana uzito kuliko posho?
  10. Ugumu wa maisha na huduma duni za afya hadi kufikia akina mama kujifungua kwa tochi za simu za kichina umeona hayafai tamko lako baba?
  11. Safari za rais zisizo na tija zaidi ya kusaga fedha za wavuja jasho unaona hazistahili tamko lako baba yangu?, mwisho
  12. Mdororo wa uchumi, uhaba wa ajira, mporomoko wa shilingi na ubadhilifu serikalini hasa wizara ya nishati na madini, wizara ya fedha, na maliasili utalii, haya hayastahili busara zako baba?

  Ndungai Mh, kaishia kusema huna uadilifu wa kutoa tamko la posho zao, kwa kifupi anamaanisha huna hadhi ya kukemea ubadhilifu katika hili, je tamko lako litakuwa ni kuzidisha malumbano katika hilo ili kumpa hard time JK ama utatetea uadilifu wako baba?

  Ukija na majibu ya haya, nitakuomba radhi kwa kukufikiria vibaya.

  Ni mimi,
  Pangu Pakavu
  Nawasalimia.
   
 2. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,593
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Kaka maswali yako ni ya msingi sana na hata lalamiko la Sumaye khs posho ni la msingi pia, tatizo nilililoliona kwa sumaye ni kaunafiki fulani hasa pale aliposema "wabunge mukidai nyongeza makundi mengine nayo yatadai hivo kumpa wakati mgumu rais"km ulivyouliza hakuna makubwa zaidi ya posho?jibu ni kwamba yapo ila mengi yatamgusa jk hivo ataonekana anamshambulia rais au akiongelea rada na ununuzi wa ndege ataonekana anamshambulia mkapa,hakuna wa kumnyoshea mwenzake kidole kwa sasa.
   
 3. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Kweli nyie ndo zao la degree za mkopo ,mnasoma menu za magazeti mnaanza kufumua ubishi,unajua kuwa sumaye hakuwa akihutubia? Alikuwa akijib swali la mwandish,alipoulizwa maoni yake juu ya posho za wabunge ulitaka ajibu mambo ya epa au meremeta?nenda kagomboe akili yako kwa waliokukopa kidegree chako ndo uanze kuwa mchambuzi wa siasa!!
   
 4. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Mkuu maswali yako ni ya msingi sana hata mimi ningependa kusikia majibu kutoka kwa Summaye, lakini hili sio tatizo la summaye, hili ni tatizo la waandishi wetu uchwala ambao nadhani huwa wamepangiwa kuuliza maswali na wale wanaohojiwa, laiti huyu mwandishi siku hiyo angemhoji haya maswali leo tungekuwa tunajua ukweli ama unafiki wa sumaye kuhusu mstakabari wa nchi yetu lakini kwa kuwa sumaye ndo aliyempangia mwandishi maswali ya kuuliza na ndio maana sumaye alitia timu pale, vinginevyo usingemuona pale na hili nina uhakika nalo kwa kuwa mpaka sasa hakuna mwanamagamba yeyote aliye na ujasiri wa kukaa mbele ya waandishi wa habari kwenda kujibu hoja juu ya mstakabari wa nchi.
   
 5. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  mzee sumaye ananikumbusha hadithi ya mchezo wa draft,katika mchezo huo mara nyingi ukiwa nje ndio unaona sana kete ya kucheza na kutoa maelekezo na lawama kwa wachezaji kwamba ungecheza pale ukale pale ukaingia kingi lakini ukikaa wewe pale then ukawa mmoja wa wachezaji unakua huziona kete za kucheza,zinakua ndogo kama njegere hazionekani!
   
 6. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hivi we Songoro, unakumbuka Dr Didas Masaburi alivyotoa msimamo wake wa jinsi mtu anavyoweza kufikiri??? Nina wasiwasi na wewe unafikiri kwa hayo...
   
 7. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni huyu sumaye enzi za maraka yake alisema "ukitaka biashara yako iende vizuri jiunge na ccm".
  LEO Anajifanya anaijua demokrasia.
   
Loading...