Wabunge na viongozi wapewe heshima zao pasipo kujali elimu zao. Pia elimu isiwe kigezo cha kumdhalau au kumdhalilisha mbunge au kiongozi. Ikumbukwe elimu inampatia mtu taaluma, kwa hiyo kama ni malumbano ya kitaaluma yajikite kwenye taaluma, sio mjadala hauhusu taaluma ya mtu unashambulia elimu yake.
Ubaguzi
Mijadala ya bunge ijadiliwe kwa weledi, pasipo kubagua mbunge kwa sababu ya chama chake au itikadi yake ya kisiasa. Lugha na kauli za kibaguzi ziepukwe.
Kukosa uzalendo
Mamlaka ziheshimike. Uzalendo kwa nchi ni pamoja na kuheshimu mamlaka ya nchi. Kiti cha spika kiheshimike kama kiti cha spika. Wabunge waepuke sana kuoanisha matatizo ya nchi na mtu binafsi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.