Mh. Spika, kwanini msitunge sheria ili kukabiliana na hicho unachokiona ni "ubabe" wa mtu mmoja kufukuza wabunge?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Ingawaje Chadema imewafukuza uanachama tu wabunge wake, lakini kwa mujibu wa sheria za nchi (siyo Chadema tena) wanakuwa wamepoteza nafasi zao za ubunge.

Sasa hoja yangu ni kuhusu kukataa utekelezaji wa kifungu hicho katika katiba kinachomnyima mtu aliyefukuzwa, ama kuacha uanachama wa chama chake, kwamba ubunge wake unakuwa umekoma.

Ingekuwa vema iwapo sheria hiyo ingesema wazi kuwa, iwapo Spika atajiridhisha kuwa mwanachana ambaye ni mbunge amefukuzwa kwa haki,au ataridhika kwamba wakati anaacha uanachama(kwa aliyeacha), aliacha kwa hiari yake bila kutishwa na mtu yeyote, basi atafanya taratibu za kumwandikia barua rasmi kuwa si bunge tena.

Hivi unavyofanya kwa sasa ni ubabe dhidi ya sheria na katiba ya nchi ambayo wewe ni sehemu muhimu ya walioitunga. Jambo hili halina afya na ni mfano mbaya.

Wengi hatujaridhika na hatua zilizochukiliwa na Chadema kuwahukumu bila kuwasikiliza. Maana wao walishambuliwa na wenzao nje ya vikao, kwa hiyo katika kujitetea wakaonekana wana kashfu viongozi na chama.

Hii si sahihi kabisa kwa Chadema. Ninaona wazi jinsi walivyoshindwa uongozi na kuwa mfano wa uongozi. Ni wazi Siku wakipewa ridhaa ya kutawala nchi hii, hawataacha kufanya wanayoyafanya. Ni lazima demokrasia tunayoihubiri itekelezwe kwa vitendo.

Ni mimi mwananchi mzalendo nisiye na chama chochote
 
Ingawaje Chadema imewafukuza uanachama tu wabunge wake, lakini kwa mujibu wa sheria za nchi (siyo Chadema tena) wanakuwa wamepoteza nafasi zao za ubunge.

Sasa hoja yangu ni kuhusu kukataa utekelezaji wa kifungu hicho katika katiba kinachomnyima mtu aliyefukuzwa, ama kuacha uanachama wa chama chake, kwamba ubunge wake unakuwa umekoma.

Ingekuwa vema iwapo sheria hiyo ingesema wazi kuwa, iwapo Spika atajiridhisha kuwa mwanachana ambaye ni mbunge amefukuzwa kwa haki,au ataridhika kwamba wakati anaacha uanachama(kwa aliyeacha), aliacha kwa hiari yake bila kutishwa na mtu yeyote, basi atafanya taratibu za kumwandikia barua rasmi kuwa si bunge tena.

Hivi unavyofanya kwa sasa ni ubabe dhidi ya sheria na katiba ya nchi ambayo wewe ni sehemu muhimu ya walioitunga. Jambo hili halina afya na ni mfano mbaya.

Wengi hatujaridhika na hatua zilizochukiliwa na Chadema kuwahukumu bila kuwasikiliza. Maana wao walishambuliwa na wenzao nje ya vikao, kwa hiyo katika kujitetea wakaonekana wana kashfu viongozi na chama. Hii si sahihi kabisa kwa Chadema. Ninaona wazi jinsi walivyoshindwa uongozi na kuwa mfano wa uongozi. Ni wazi Siku wakipewa ridhaa ya kutawala nchi hii, hawataacha kufanya wanayoyafanya. Ni lazima demokrasia tunayoihubiri itekelezwe kwa vitendo.

Ni mimi mwananchi mzalendo nisiye na chama chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
Unafahamu kuwa hao wabunge baadhi walishasema watahamia Nccr mageuzi? Wangekuwa ni wabunge wa CCM wametangaza hadharani kuwa wanampango wa kuhamia Chadema unafikiri wangefanywa nini?Hata hivyo wamevumiliwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom