Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo yupo chini ya ulinzi wa polisi muda huu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mh. Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo yupo chini ya ulinzi wa polisi muda huu. Kukamatwa kwake kuna kuja baada ya agizo la spika wa Bunge Job Ndugai kumhitaji afike kwenye kamati ya maadili mjini Dodoma kwa kile kinachoitwa na spika kusema uongo kuhusiana na kupigwa risasi Mh. Tundu Lissu.

Ikumbukwe Mh. Kubenea alikuwepo bungeni wiki hii, lakini akiwa ameshaondoka Dodoma yupo Morogoro akapigiwa simu ya kurudi Dodoma ndipo alipowaambia kuwa asingerudi Dodoma kwa ku...wa alikuwepo huko na walishindwa kumhoji.

Hayo yakiendelea Mapema leo gazeti lake la MWANAHALISI limefungiwa miaka miwili kwa kile kinachoitwa na serikali kuandika habari za kichochezi.
kubenea.jpg
 
Ukitaka kupata Tafsiri ya Ujanja ujanja, Utapeli na kubadili gia za angani kadri atakavyo Bosi wako Basi mfuatilie Saed Kubenea.

Mara ya kwanza walipokuwa wanajadili Namba gani itumike kupokea Michango ya Tundu Lissu lilipotajwa tu jina la Saed Kubenea kila Mtu kwny Kikao Aliguna mpaka walipobadili na kumpa Ester Matiku Hilo Jukumu
 
Kukamatwa viongozi wa ushindani ndio ingelikuwa kunaongeza viwanda.......ingelikuwa vyema.
 
Anataka awapangie kazi au sio??, yeye angeona umuhimu huo basi angejipeleka akawaulize km wanahitaji kumhoji chochote ama arudi zake Dar?? ..

Kama alidhindwa na wamemuomba amekaidi...basi acha watumie nguvu kumhoji wala hakuna shida.

Huu msimu si wa kupangiana majukumu, tuombe roho mtakatifu awe anatufungulia mambo yajayo...mfano siku nikienda songea kutembea kabla sijarudi Dar roho mtakatifu anikumbushe nikamsalimie RPC wa huko, RTO, RC, DC nk baada ya hapo nirudi zangu dar...huu mchezo hauhitaji hasira na utatengeneza Tanzania yenye upendo na mshikamano....

Ushauri tu na maoni yangu binafsi. Ukishindana najua hutoshinda, cha msingi tudumishe umoja!!!
 
Back
Top Bottom