Mh. Rais wangu mpendwa, tafadhali soma hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Rais wangu mpendwa, tafadhali soma hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chatumkali, Jan 8, 2012.

 1. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mh Raisi,salaam!
  Mheshimiwa nilifuatilia hotuba yako ya kufunga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2012.Kama kawaida hotuba ilikuwa nzuri.Ulieleza mambo mengi ya maana kwa mustakabali wa nchi yetu.Hata hivyo kuna suala moja uliligusia binafsi limenisikitisha sana.Sipendi kuwa mnafiki,lazima niseme ukweli kwamba kwa suala hilo ULINIKERA!Si jingine ila ni suala la MADENI ya watumishi yanayojumuisha madai ya fedha za malimbikizo ya mishahara,uhamisho,masomo,likizo,matibabu nk.Madai haya ya mabilioni ya shilingi za kitanzania yanawahusu walimu na watumishi wengine.
  Mheshimiwa ulinikera kwa sababu eti nawe ulionyesha kushangaa kwa nini madai haya HAYAKUKOMA wakati tayari ulishatoa maelekezo ya kukomeshwa kwa madeni haya!Raisi wetu unashangaa badala ya kuchukua hatua kali dhidi ya watendaji wazembe wanaofedhehesha serikali yako?Hivi unajua kwamba wakati wewe unashangaa sisi waathirika tunaumia?Hivi unajua kwamba wapo watumishi wamepandishwa vyeo hadi leo ni zaidi ya miezi 12 bado hawajarekebishiwa mishahara yao ili iendane sambamba na vyeo vyao vipya?na bahati mbaya hawaelewi hayo madai yao watalipwa duniani ama ahera!Mheshimiwa hawa watumishi wanamajukumu,wana watoto kama ulionao wewe hao akina Ridhiwani na akina Miraji na wengineo.Kwa nini usiwaonee huruma kwa kuwawajibisha mara moja waliosababisha kadhia hii?Badala yake wewe unashangaa!Unashangaa wakati Mkulo na Ghasia wako ofisini kama kawaida.Wasaidizi wao nao wako ofisini kama kawaida.Mheshimiwa kama haki za watumishi wa umma zinabinywa kiasi hiki na wasaidizi wako hivi hali ikoje kwa haki za makundi mengine kama mamalishe,machinga,wakulima wa mchicha nk?Ama tuamini kwamba wasaidizi wako wmekuona wewe kama mbwa koko?<samahani kwa kutumia hilo neno>.Si unajua tabia za mbwa koko?Ni fundi wa kubweka lakini hana ubavu wa kushambulia.Ukijifanya unaokota jiwe tu yeye huyoo mbio!Mheshimiwa ulitakiwa kuchukua hatua kali haraka kwa wote waliosababisha mrundikano wa madeni ya watumishi hata kabla ya kuja kutuhutubia huo mshangao wako.Mimi nimeamua kuwasilisha hisia zangu kwa mtindo huu,haijalishi kama utaamua kunibatiza majina ya ndege kama mbayuwayu,kunguru,mwewe nk!MODS muiache kidogo hii kitu mkuu aione.
   
 2. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...ni kawaida yake kushangaa mkuu. Si unajua wahisani hawajamwambia
   
 3. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  alivyokuwa msanii anaweza kukushangaa kuwa hajasema hivyo, we raisi anaulizwa kwa nini watanzania ni maskini anajibu kwamba hata yeye hajui sasa huyo ndoa ataweza kuwawajibisha watendaji wake
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Jk is a very Smart President that I have never seen. Rais hajui kwanini watu wake ni maskini! Shit!
   
 5. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tushakuwa na rais msanii hapa hamna jipya mpaka muhura wake uishe.
   
 6. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #6
  Jan 8, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Muda huu bila shaka atakuwa facebook. Ngoja nikamtonye kuwa kuna ujumbe wake hapa.
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  mida hii atakuwa yupo baa anapata moja moto
   
 8. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hata wewe uliyeandika atakushangaa vile vile
   
 9. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Matendo yake anakuwa kama ni Rais Kivuli!
  Eti na yeye analalamika, wananchi wafanyeje
  sasa?!
   
 10. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Chatu,

  Nachangia uzi wako japo sina hakika kama mods watauacha hadi kesho kwa kuwa lugha uliyotumia ni butu mno.

  Ujue kwamba rais ni alama ya amani, mshikamano na utaifa wa taifa lllote duniani, hili hata Zitto Kabwe analitambua. Suala la yeye kuonekana anashangaa matatizo ya msingi kana kwamba ni mgeni nchi hii linakera sana ingawa unapaswa kujua nini sababu sahihi ya yeye kushangashangaa tu kwa kila jambo nyeti.

  Katika kampeni za 2010 hata wewe ulitakiwa uonyeshe moyo wa kimapinduzi, uelimishe kuanzia familia yako, jamii yako na kama ungekuwa mzalendo hata taifa kwa ujumla, lakini ukakaz na wewe ukishangaa kwa nini hata kampeni za uchaguzi JK alifanyz yeye na familia yake huku akishangaa watanzania walivyokuwa wanamponda kila kona, na kwa makusudi kabisa tume ya taifa ya uchaguzi ikakushangaza na wewe ilipomtangaza kuwa kashinda, ukabaki na wewe unashangaa.

  Walimu na wafanyakazi wengine wakabaki wanashangaa kwa nini siku zote wao ndio husimamia uandikishaji wa wapiga kura huku wakiwashangaa watanzania wengine walipokuwz wakitakz ulaji huo, baadae wakashangaa kwa nini malimbikizo yao hayalipwi, kufumba na kufumbua na wewe ukashangaa kwa nini rais anashangaa hilo.

  Na mimi nakushangaa kwa kutotambua mfumo wetu wa kushangaashangaa katika kila jambo, ipo siku na mke wangu akinizalia mtoto wa kihabeshi ntashangaa. Kule mwanza si unakumbuka huyuhuyu JK alishangaa watu kula mapanki na sisi tukabaki tukimshangaa ati kwa nini hakujua hilo, mwisho na watu wa mwanza wakabaki wanashangaa kivipi rais wao anashangaa wao kula mifupa.

  Majuzi JK alipoulizwa kwa nini tz ni maskini alibaki anashangaa tu hadi yule aliyekuwa anamhoji na yeye akabaki anamshangaa rais wetu.

  Sisi tutaendelea tu kushangaa hadi nchi majirani zetu nao watushangae.

  Ni mimi,
  Pangu Pakavu,
  Nakushangaa kabisa.

  Tushangae tu mkuu.   
 11. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Alidai eti amewaamuru wahusika wampatie majibu ya nini kimesababisha hali hiyo!Anadhani ataendelea kutudanganya hadi lini?Kumbe ndio maana akina Jairo na Luhanjo walilikoroga hawakuchukuliwa hatua zozote.Makazini ari ya kufanya kazi watu inazidi kushuka yeye anashangaashangaa tu!Huyu mtu anamatatizo gani kichwani lakini?
   
 12. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Aisee Pangu Pakavu!

  Kumbe sasa hivi Taifa linapita kwenye wakati wa kushangaashangaa!Wacha tuendelee kushangaa shangaa kwa miaka hii minne iliyobaki ili 2015 tufanye maamuzi ya kushangaza ili tuwaache mabingwa wa kushangaashangaa kama JK wabaki wanashangaa!Kesho nakwenda kukabidhi barua yangu ya kupanda cheo kwa bosi wangu ili anishushe cheo.Siko tayari kuendelea kutumikia cheo hewa cha kipumbafu!Nadhani na yeye atabaki anashangaashangaa kama mkuu wao.FULL STOP!
   
 13. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Nashangaa!
   
 14. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #14
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Duh!! Namie nakushangaa aisee... Unashangaashangaa nini sijui?!! Hapa ni kushangaa tu, full kushangaa hadi watu watushangae...

   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Si ungemtuma Liziwani aongee naye tuu..
   
 16. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #16
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ngoja nishangae kinyamwezi,,, kaaahh!!!, aisee nashangaa kumbe na wewe umeshangazwa na cheo feki kisicho na malipo stahili, mweee,
  nimeshangaa kabisaa..


   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Jan 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hii nchi inshangaza sana aisee

  Nashangaa sana watu wanaomshangaa jk kwa kushangaa kila kits, Wakati nchi yenyewe Ina mshangao we kudumu

  Sie tushangaeshangae hadi 2015
   
 18. N

  NGONYA NM Member

  #18
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NGONYA NM, hii style ya uongoz ya mkuu wa nchi haipo kwenye style za uongoz dunian. Yeye huwa asiposhanga huwa ananyamazia swala lipite, watu wasahau bila utekelazi angali maazimio ya bunge la 9 kuhusu richmond na la 10 kuhusu Jairo na luhanjo kimyaaaaa! Kama vile hakuna chakutekeleza. TUSIRUDIE KOSA 2fanye maamuz mazur 2015
   
 19. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  tukiendelea kushangaa hiyo mishangao itatugeuzia kibao itaanza kutushangaa na yenyewe
   
 20. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  pigia mbuzi gitaa, labda anaweza akacheza.
   
Loading...