Mh.Rais Viongozi hawa wamefika muda wa kustaafu;

Kiroroma

JF-Expert Member
Feb 6, 2009
370
114
Mh,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.JM Kikwete, Naleta ombi langu kwako japo umechelea kufanya maamuzi juu ya viongozi hawa ambao umri wao wa kustaafu na bado wako madarakani!!

1.Katibu Mkuu wa CCM
2.Katibu Mkuu Kiongozi
3.Makatibu wakuu 9
4.Wakuu 10 wa Mikoa
5.Wakuu 18 wa Wilaya
6.Viongozi wa Taasisi 7
Idadi hiyo niliyoitaja hapo juu wamefika na kupitiliza umri wao wa kustaafu,Lakini bado hutaki kuwastaafisha wapishe vijana kuchukua nafasi.

Mh,Rais tunajua kabisa kuna gharama za kuwastafisha lakini ni ndogo sana ukilinganisha na hasara wanayolitia Taifa kwa sasa hivi.Mathalani KM Kiongozi mbali ya kukutia aibu kwa kukuteulia na kukushauri juu ya watendaji wabovu pia anachukua mlungula kwa sana.

Tunaelewa ni kwa kiasi gani wananchi wanaichukia serikali kwa sababu kama hizi.Kuna nafasi kibao za kujaza makatibu wakuu wizara mpya,Wakuu wa mikoa mipya na wale waliopata ubunge kisha uwaziri kama Lukuvi.Usikawie kufanya maamuzi katika haya kwani hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha.
Nashukuru kama utapokea ushauri wa mwananchi mmoja kama mimi kwani wengi hawawezi kukufikia na kukuambia haya.
 
Hawezi kuwaondoa hao maana hata yeye kimawazo keshapitiliza umri wa kufikiri angeanza kustaafu yeye kwanza
 
wapo wengi sana, mfano james msekela, jamani hizi ni zama za vijana, wazee ondokeni
 
Hawa wazee wana vyeti vya kuzaliwa kweli?yawezekana personal particulars zao zinaonyesha bado wanastahili kuwepo kazini.
 
Wapo wengi watu kama Cheyo kwake ishakuwa alasiri atuachie vijana.
 
Back
Top Bottom