Mwingereza
JF-Expert Member
- Jan 21, 2014
- 1,115
- 2,771
Nikita mtumishi wa umma, mashahara wangu hauwezi kukidhi mahitaji yangu ya kifamilia. Mwaka 2006 niliamua kuwa mjasiriamali. Nimekuwa nikifanya kazi na taasisi nyingi makampuni binafsi na hata Halmashauri. Mwaka jana October, 2016 Nilishinda tender ya ku supply vifaa kwenye moja ya Tasisis nchini. Ambapo niliagiza bidhaa kutoka nchini Japan Baada ya bidhaa kufika, TRA walinipiga uplift ya 50% kwani walidai hizo bidhaa ndio bei halisi kwenye soko na TBS nao wakanipiga 15% penalty kwa kutokukagua bidhaa. Nikajikuta gharama imekuwa kubwa kuzidi thamani ya tender.
Faida niliyoweka ilikuwa ni 20%. Lakini kuanzia tender board, Ugavi, uhasibu wote walikuwa tayari kukwamisha malipo yangu ambayo imechukua miezi mitano tangu nifikishe stakabadhi zote. cha ajabu, wiki iliyopita nilipewa malipo yangu, hapo nikakuta wamekata 10% zaidi. Nilipouliza, niliambiwa ni withholding tax ambayo ni lazima ikatwe. Ni maagizo ya serikali. Mbaya zaidi imefika hadi kukata mtaji wangu kwa 34.7%
Na wale watumishi wa Taasisi nao hawaelewi lazima uwalipe tena kwa ugomvi, vinginevyo ntazidi kusubiri pengine hadi mwaka kesho. Hii ni biashara kichaa.....Haiwezekani kama makampuni mengine, nimeamua kufunga biashara rasmi mwisho wa mwezi huu. Niliajiri watu 4 wanaonisaidia kwenye hii biashara. inabidi wakatafute kazi kwingine.
Hii ndio hali halisi. Kodi hazikamatiki, Ni kila aina ya kodi. Hakuna kupumua, wala hakuna faida. Hakuna atakayefanya kazi za hovyo. Ndio maana biashara zinazidi kufungwa, na hakuna mwekezaji mwenye akili timamu ataendelea kufanya biashara kwenye mazingira kama haya. Ukileta bidhaa kutoka nje, utajuta. Magufuli, hali si shwari. Bandarini na TRA kuna tatizo