Mh Rais unalipa kodi?

KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
880
327
Salaam wana jamvi.

Miaka michache nyuma kuliibuka mjadala watu wakitaka kujua mishahara ya viongozi. Wapo waliosema hairuhusiwi kisheria kuijadili lakini kwa bahati mbaya au nzuri mbunge Zitto kabwe alitaja mshahara wa waziri mkuu na wa Rais.

Siku chache baadae waziri mkuu wa wakati huo mh Mizengo Pinda alitaja mshahara wake akitofautiana na Zitto.

Leo sitapenda kujadili hiyo mishahara. Nina rai moja kwa mh Rais, sisi hatufahamu unalipwa kiasi gani lakini mimi binafsi ningependa kujua kama wewe unalipa kodi katika huo mshahara.

Nia na madhumuni ni kutaka utuongoze kwa mfano kama ulivyofanya Disemba 9 kwa kufanya usafi. Haitaleta picha nzuri kuhimiza ulipaji kodi kama ninyi viongozi wa juu hamkatwi kodi katika mshahara. Kama kuna sheria zinazozuia viongozi wetu wazalendo kukatwa kodi nafikiri ni wakati muafaka kuzibadilisha.

Maswali ya aina hii hayatakiwi kabisa kuulizwa kama kila kitu kingewekwa wazi lakini kwa bahati mbaya inaonekana kama dhambi kuhoji mishahara ya viongozi tunaowaweka madarakani sisi wenyewe. Inasikitisha kuona muajiriwa anajipangia mshahara ambao muajiri wake hajui ni kiasi gani.

Tukifanikisha hilo tuhamie kwenye posho za waheshimiwa wabunge, nafikiri wataiga uzalendo wako mh Rais.
 
Back
Top Bottom