Mh Rais, Taifa linahitaji tiba - Godbless Lema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Rais, Taifa linahitaji tiba - Godbless Lema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Henry Kilewo, Aug 26, 2012.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  Aug 26, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Mh Rais , Taifa linahitaji tiba . Godbless Lema

  Mh Rais , nakusalimu .
  Mh Rais na huu ni ushauri wangu kwako kama Mkuu wa Nchi na mtazamo wangu juu ya matukio yanayotokana na changamoto katika Sensa ya Taifa hivyo nakunifanya nikuandikie waraka huu.

  Mh Rais , Kama Taifa hili kwa miezi michache mbele inayokuja Siasa za Udini , Ukabila na ukanda utaendelea kushabikiwa katika kiwango hiki cha sasa , ukweli ni kwamba siku chache zinazokuja Taifa hili litaanguka na halitasimama tena, Propaganda zilizofanyika huko nyuma dhidi ya vyama vya upinzani mbali mbali zilifikiriwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kuviangamiza vyama hivyo tu na huku Watawala wakibaki salama, lakini leo tunaanza kuona lugha za Udini zikitawala katika Taifa letu kila siku na ule mpango wa kuangamiza Vyama hivyo umekwenda mbali zaidi na sasa unakaribia kuangamiza Taifa.

  Mh Rais Nchi hii haiko salama hata kidogo na pengine wahusika wanaopaswa kulinda usalama wa Nchi wanakupa ripoti za hofu na woga na hivyo unashindwa kupata taarifa kamili ya ukweli wa mambo yanavyoendelea katika Taifa letu, ukitazama suala la Sensa na changamoto zake kwa sasa utagundua kwamba sio faida hata kidogo kulazimisha jambo hili kwa kutumia nguvu kwani sio sahihi hata kidogo kujua tu idadi ya watu bila kuzingatia hofu ya watu hao na mashaka ambayo yamejengeka katika Imani.

  Mh Rais , Siasa chafu ambazo zimekuwa zikitafuta Madaraka bila kuangalia siku njema za baadae za Nchi ndio chanzo cha kinachotokea sasa, tulipokuwa Igunga Chadema ilifanyiwa propaganda za Udini sana na kwa bahati mbaya waliofanya hivyo walishinda uchaguzi na huku Watu wale waliofanya hivyo waliamini na kufikiri Siasa hizo za kibaguzi zitaishia Igunga tu na bila kutambua Dini ni Imani na lazima kutaendelea kuwepo na mpasuko mkubwa hata baada ya Uchaguzi.

  Mh Rais , Uhuru wa kweli sio Mtu kufanya kila anachotaka bali kile anachopaswa tena katika haki na kweli " Kama lengo la Watawala kubaki madarakani au kuongoza litafanywa kwa nguvu na namna yoyote hile hata kwa kuwagawa Watu kwa dini zao na kabila , basi siku chache zinazokuja Taifa letu halitaweza kutawalika tena na Mamlaka hayo yanayotafutwa hayataweza kuwa na faida kwa kizazi hiki na kizazi kinacho kuja na ukweli ni kwamba kwani kila aina ya ubaguzi wa aina yeyote unaofanyika ama kwa siri au hadharani hautaacha Jamii yetu kuwa salama.

  Mh Rais, Chama tawala siku zote wajibu wake katika kujibu hoja za wapinzani ipasavyo ni kutekeleza ahadi zake ambazo walizitoa wakati wa uchaguzi na huu ni wajibu mkuu katika kutawala kwa Chama tawala , lakini Chama kilichoko madarakani kinapoanza kuwagawa watu kwa dini na kabila ili mradi kifanikishe malengo ya kutawala basi ni lazima tutambue kuwa Viongozi wa Chama hicho wamekusudia kabisa kuipeleka Nchi yetu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

  Mh Rais , siku hizi katika forum mbali mbali zinazojadili mambo ya Siasa katika mitandao ya kompyuta hapa Tanzania , kumekuwepo na maoni mbali mbali na mitazamo haswa wakati wowote ule unapofanya uteuzi au kuchagua mtendaji katika Serikali , Mara nyingi , ghafla utaanza kuona watu wananza kuuliza Kabila au Dini ya mtu aliyeteuliwa au kupendekezwa, hii ni hatari kubwa kuwa na Taifa ambalo sifa ya Mtu ya kwanza kwa wachambuzi na wadadisi inajadiliwa kwa Dini au Kabila ya Mtu fulani , kwani hatuwezi kuongozwa kwa mlinganisho wa Kabila au Dini ili kupata utawala bora . Tabia hii wakati mwingine inapelekea kutafuta viongozi mbali mbali kutoka kila pembe ya Nchi ili kupata mlinganisho wa Ukanda na Kimkoa na hivyo kusababisha kuishia kupata viongozi pengine Viongozi wasiokuwa na uwezo kwa sababu ya kutafuta mlinganisho katika kupanga safu ya uongozi na utawala . Na kwa kweli huu nao ni ubaguzi uliojificha unaoendelea katika Taifa letu.

  Utawala thabiti mahali popote , Utazingatia , Uwezo , Sifa , Maarifa ,Uadilifu na Hekima ili Mtu kuchaguliwa kuongoza . Dini na kabila lake sio jambo muhimu hata kidogo katika uongozi, hivi ikitokea katika uchaguzi Dini moja tu na kabila moja ndio likahusika katika uchaguzi wakati wa mchakato wa kutafuta viongozi , je Serikali itaahairisha Uchaguzi kwa sababu watu wengine wa Dini na Kabila nyingine hawakuona umuhimu wa kushiriki Uchaguzi ? ni swali ambalo linaweza kuonekana halina msingi lakini kwa wanaona mbali watajua ni nini namaanisha ? hata hivyo tunakoelekea sasa tusipokuwa makini , tutanza kupokezana Madaraka na Utawala kwa kuangilia Udini na sio Uwezo na Uadilifu na tukifika hapo Taifa hili halitasimama tena.

  Mh Rais ni wajibu wako sasa kusaidia Taifa hili kwa Mamlaka uliyonayo ni Imani yangu hata wewe umekwishaona hili na ni matumaini yangu kuwa unalifanyia kazi . Mfano wa wazi ni pale Katibu Mkuu wa CCM Bwana Mkama , alipotaka kuleta Siasa za Kibaguzi katika Msiba wa Marehemu Bob Makani pale Karimjee wakati akitoa salamu za rambi rambi ambapo wewe mwenyewe ulikuwepo kama Kiongozi Mkuu wa Taifa na ulishuhudia upotoshaji wake huo ambao ulionekana kama lengo ilikuwa kuidhoofisha Chadema huku hakisahau kuwa dhambi ya ubaguzi aina mipaka.

  Mh Rais , Martin Niemoller , alisema maneno yafuatayo yalipomkuta " When Hitler attacked the Jews I was not a Jew, therefore I was not concerned. And when Hitler attacked the Catholics, I was not a Catholic, and therefore, I was not concerned. And when Hitler attacked the unions and the industrialists, I was not a member of the unions and I was not concerned. Then Hitler attacked me and the Protestant church -- and there was nobody left to be concerned"

  Mh Rais , Tatizo ni kubwa na ni vyema likashughulikiwa kwa nguvu zote sasa na kwa hekima , hata hivyo nafikiri waraka huu hautakukwaza kwani ni ukweli wangu juu ya hali halisi inayoendelea kujitokeza katika Nchi yetu na Mimi nikasema nisikae kimya ni bora niseme , Taifa linakwenda mahali pabaya kama dhambi ya ubaguzi isipodhibitiwa.

  Nakutakia Kazi Njema.

  " Only Time Will Tell "
  Godbless Jonathan Lema
  26/8/2012
   
 2. M

  Magesi JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera kamanada lema
   
 3. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Powerful and only the wise can understand a.d take action. Anaanza kuoa adha ya udini ambao alidhani utamsaidia.
   
 4. m

  majebere JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Siasa zake chafu si ndio zimeng'oa ubunge, huyu ndio anahitaji tiba,tena ya haraka sana.
   
 5. T

  Tiger One JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 569
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Utabaki kuwa jembe!!!
  Lakini kiongozi mbona umekuwa kimya mno? Wabaya wetu wanasema umekwisha. Naamini sio hivo ila wewe usipewew majukumu ya ofisini wewe ni wa kuzunguka nchi kuhamasisha m4c kamanda.
   
 6. M

  Martin Jr JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  " Kamanda namkubali sana , endelea na mapambano Lema ni ujumbe wa maana sana kwa CCM ndio chanzo cha migogoro yote inaoonekana leo
   
 7. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Nakukubali kamanda,..arusha'z 4 u
   
 8. a

  arusha 1 Senior Member

  #8
  Aug 26, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kamanda Lema , yuko Arusha na tiyari amefanya mikutano kata mbili zinazotarajiwa kuwa na mikutano Aruimeru na Arusha Mjini, na anaendelea kupambana kufanikisha issue ya M4C Mwanza ambayo anatarajia kuwa live on Tv on the mid of september
   
 9. m

  majebere JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Siku hizi hata vichaa wanashabikiwa.
   
 10. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Huu waraka ningeweze kuutuma kwa Ritz,nchemba,lusinde ,wassira na nanii na vile
   
 11. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  kAANDIKA TU NA KUUTUPA HAPA AU KAMTUMIA JK
   
 12. m

  majebere JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  JK atamsikiliza huyu kweli halafu sio ajabu hata haya maneno ameandikiwa na Zitto.
   
 13. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kamanda Lema umeutupia kwenye email ya ikulu@yahoo.com?mweke pia kwenye twiter wall yake.sikilizia sasa waajiriwa wa Nape watakavyo tokwa povu
   
 14. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Lema ni mbaguzi wa dini na jinsia, maneno yake hayaendani na matendo yake. Suala la siasa za ukanda ni imani ya baadhi ya viongozi wa CDM sasa sijui hilo nalo mnataka Mh rais aje atoe semina?
   
 15. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Majebere unaweza kumchukia mtu lakini siyo ukweli anaosema
   
 16. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  wakati mwingine unaweza kumpinga mtu kwasababu tu unamchukia lakini mwisho wa siku ukweli haujalishi unatoka kwa nani mpendwa au mchukiwa.Chunguza utabaini nani kinara wa kueneza propoganda za ukanda na udini
   
 17. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Thanks kamanda kwa ujumbe, ukweli husimama daima na kiukweli huu ni ujumbe mzito sana kwa dhaifu na dhaifu wenzake, nakubali kazi zako lema kama mpiganaji wa watu mithili ya malcom X na king Martin luther Jr, una confidence ni mtu wa watu, unapendwa na watu wanaojitambua, wanaojua historia, watu wenye dhamira safi lakin unachukiwa na mafala na majuha na hao wasikupe shida kwani chuki ya mwendawazimu ni furaha kwa mwerevu.

  LEMA go......................................!
   
 18. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #18
  Aug 26, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Bora umempa live huyu jamaa.
   
 19. C

  CAT5 Member

  #19
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ushauri mzuri na umezingatia uzalendo wako kwa Taifa lako.
  Ushauri wako jembe Lema vilevile unastahili kupokelewa na rika mbalimbali,
  viongozi mbalimbali wa kidini,kisiasa ili sumu hiyo isizidi kuenea.
  Kwa sehemu Mkuu jana alilisemea kuhusiana sensa hasa wale wachache waliotaka
  tuhesabiwe kwa kuwemo kipengere cha dini ambapo alielezea haya yalifanywa enzi ya mkoloni
  kwa lengo lake alilokuwa analifahamu,hinyo kwa leo halina mana kuwekamo kwenye mfumo.
  Wote kwa pamoja tutafakari kwa faida ytu na vizazi vyetu.TUCHUKUE HATUA.
   
 20. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Ujumbe mzuri kiukweli. Nimeipenda zaidi hii "Dini na kabila lake sio jambo muhimu hata kidogo katika uongozi, hivi ikitokea katika uchaguzi Dini moja tu na kabila moja ndio likahusika katika uchaguzi wakati wa mchakato wa kutafuta viongozi , je Serikali itaahairisha Uchaguzi kwa sababu watu wengine wa Dini na Kabila nyingine hawakuona umuhimu wa kushiriki Uchaguzi?"
   
Loading...