Mh Rais tafaadhali rudisha mali zote CCM ilizohodhi, Hadaa sio nzuri

Freeland

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
14,481
10,222
Mh Rais tafadhali bana.Tunahitaji utaifishe mali zote za CCM zirudi kwa wananchi.

CCM ilihodhi mali za wananchi na kujimilikisha kipindi cha transformation kwenda vyama vingi.Mali zote za CCM ziliibwa kutoka kwenye umma.

Kuna viwanja vingi vya mpira,maeneo ya wazi na majengo mengi ambayo ni mali ya umma ila chama chako CCM kimeyaiba toka kwa umma wa watanzania.

Ni aibu kusema unapambana na ufisadi wakati wenye mwenyewe ni kiongozi wa chama ambacho kinanufaika na mali za wizi.

Ifike mahali tuone aibu hata kwenda kanisani kudai eti tunamwomba Mungu...Mungu yupi huyo?

Kama una nia safi rudisha mali zote za CCM ambazo kabla ya mwaka 1992 Zilikuwa milki ya wananchi wote.

Pale Bukoba unatufanyia hadaa...Kabla ya kuirudisha ile shule serikalini ulipaswa kutuambia;
  • Ni kwanini umeamua kuirudisha shule ile peke yake na sio pamoja na zingine zote?
  • Ni kwanini umetumia michango ya wananchi kwenye tetemeko kukarabati shule ya CCM?
  • Hayo maamuzi umeyachukua kwa majadiliano yapi?
  • Kuna faida zipi serikali itazipata kwa kutaifisha hiyo shule?
  • Kwanini umemua kuichukua shule yenye madeni lukuki ili kuibebesha serikali jukumu la kulipa hayo madeni? ili kuisaidia CCM
Watanzania tunaweza kuwa waoga na wasio na uwezo wa kuthubutu kuchukua hatua...lakini walau kusema tutasema tu.Tafaadhali bana,hadaa sio nzuri ,Muogope Mungu .

Tanzania ni muhimu sana kuliko tamaa zetu za kisisasa...Nchi hii ni mali ya watanzania na kiongozi yoyote anayechaguliwa anawajibika kwa watanzania....Hakuna mtu awaye yote anayeweza kusema yeye ni mkuu kuliko wote.....ukichaguliwa wewe unakuwa mtumishi wetu...na tuna haki ya kukukosoa ,kukupongeza na kukuwajibisha.
 
Kwa watu wenye upeo mdogo wanadanganyika na maigizo yanayofanywa na bwana yule,lakini mtata kama mimi najua huwezi kupata kitu cheupe kwenye mkaa...nje ya mada,mods ondoeni alama ya xmas kwenye sura za watu,tunataka tutambuane kwa sura na sikukuu zimepita na watu wapo "broke"
 
Back
Top Bottom