Mh Rais pata muda wa kupumzika

Mh Rais pata muda wa kupumzika

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
677
Mh Rais pole na kazi za kututumikia Watanzania. Ninakupongeza kwa kazi kubwa unazofanya katika kuleta mapinduzi makubwa katika Taifa hili la Tanzania.

Kazi zako zinaonekana na zinaungwa mkono na Watanzania wengi. Wachache wanaokukosoa wanatimiza wajibu wao wa kukuimarisha katika majukumu yako.

Mh Rais ninajua una kazi nyingi na unakosa hata muda wa kupitia kwenye mitandao muda mwingine.

Pamoja na hayo ninaomba niandike haya machache ninaamini kupitia wasaidizi wako ndani ya Chama na Serikali watakufikishia.

Mh Rais afya yako ni muhimu kuliko mambo yote. Watanzania wengi tunafurahishwa na kazi unazofanya lakini pia wanakuhurumia kwa kuwa unaji overload.

Leo nimeshuhudia ukitoka Dodoma ukienda Chato. Ukiwa njiani umetumia muda mwingi kusikiliza kero za Watanzania waliokusimamisha njiani.

Umetumia muda mrefu kuzungumza na kutatua kero za wananchi kiasi ambacho umefanya zaidi ya mikutano 20 kwa siku ya leo.

Mh Rais ninatambua unakerwa na mambo mengi na ndiyo maana unalazimika kufanya kazi muda wote. Binafsi ninaamini Watanzania wanatamani kuendelea kukuona ukiwa Rais wao lakini ukifanya kazi kwa kiasi na kuuruhusu mwili kupumzika.

Umekuwa na mfululizo wa mikutano mingi tena ya kusimama muda mrefu. Shida za Tanzania hazitaisha kwa muda mfupi kwa kuwa zilitengenezwa kwa miaka mingi.

Ninatambua unafanya hivyo ili kujaribu kumaliza kero zote, lakini afya ni mhimu kuliko haya yote.

Mwisho nimalizie kwa kwa kukupongeza kwa kuendelea kuiongoza Tanzania ikiwa na umoja na utulivu mkubwa.

Mungu aendelee kukupigania ili unayotamani kuyaona katika kipindi chako yaendelee kudhihirishwa.
 
Unamuonea hurumu mtu anayezunguka nchi nzima huku akila upepo wa ma v8,helikopta,per diem full ulinzi,kwani amekwambia ana shida gani?

Wewe endelea kupumzika kwny hayo majani sijui majaruba kama ulivyo hapo kwny avatar yako,
 
Mizunguko ambayo haina impact ,Ndio maana kila Leo kila mahali zinaibuliwa kero zile zile

We need strong, efficient and effective institutions
Kuwaziba midomo watu ndio kwanza unawaibua million 10 wengine
 
Kama kawaida vjana kupiga mapreizi ili wapate vyeo sasa unaweka namba ili nani akugie upate uteuzi? Swai nnnn
 
Mh Rais pole na kazi za kututumikia Watanzania. Ninakupongeza kwa kazi kubwa unazofanya katika kuleta mapinduzi makubwa katika Taifa hili la Tanzania.

Kazi zako zinaonekana na zinaungwa mkono na Watanzania wengi. Wachache wanaokukosoa wanatimiza wajibu wao wa kukuimarisha katika majukumu yako.

Mh Rais ninajua una kazi nyingi na unakosa hata muda wa kupitia kwenye mitandao muda mwingine.

Pamoja na hayo ninaomba niandike haya machache ninaamini kupitia wasaidizi wako ndani ya Chama na Serikali watakufikishia.

Mh Rais afya yako ni muhimu kuliko mambo yote. Watanzania wengi tunafurahishwa na kazi unazofanya lakini pia wanakuhurumia kwa kuwa unaji overload.

Leo nimeshuhudia ukitoka Dodoma ukienda Chato. Ukiwa njiani umetumia muda mwingi kusikiliza kero za Watanzania waliokusimamisha njiani.

Umetumia muda mrefu kuzungumza na kutatua kero za wananchi kiasi ambacho umefanya zaidi ya mikutano 20 kwa siku ya leo.

Mh Rais ninatambua unakerwa na mambo mengi na ndiyo maana unalazimika kufanya kazi muda wote. Binafsi ninaamini Watanzania wanatamani kuendelea kukuona ukiwa Rais wao lakini ukifanya kazi kwa kiasi na kuuruhusu mwili kupumzika.

Umekuwa na mfululizo wa mikutano mingi tena ya kusimama muda mrefu. Shida za Tanzania hazitaisha kwa muda mfupi kwa kuwa zilitengenezwa kwa miaka mingi.

Ninatambua unafanya hivyo ili kujaribu kumaliza kero zote, lakini afya ni mhimu kuliko haya yote.

Mwisho nimalizie kwa kwa kukupongeza kwa kuendelea kuiongoza Tanzania ikiwa na umoja na utulivu mkubwa.

Mungu aendelee kukupigania ili unayotamani kuyaona katika kipindi chako yaendelee kudhihirishwa.
Hata mimi nilikuwa nawaza hivyo, RAIS apate muda wa kupumzika. Kazi anazozifanya zinaonekana
 
Back
Top Bottom