ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,950
- 6,981
Nimeangalia matokeo ya mtihani wa upimaji darasa la nne, kwa kweli hali ni mbaya sana.
Kuna shule ilikuwa na wanafunzi 250+, kati yao 75 wamefeli kabisa na hivyo wanatakiwa kukariri darasa la nne.
Moja ya sababu zilizofanya wafeli, ni kukosa waalimu tangu wakiwa darasa la kwanza.
Wakati unaingia madarakani, ulikuta kuna program zilizolenga kukabiliana na upungufu wa walimu, ukazisitisha kwa kuwa hazikufuata mlolongo sahihi wa elimu.
Sasa kuna waliomaliza tangu mwaka juzi, hawajaajiriwa, wako mtaani wakati tangu kipindi hicho kuna walimu wamefariki, wameacha kazi na wengine wamestaafu kwa mujibu wa sheria. Hivyo upungufu wa walimu ni mkubwa sana.
Elimu Bure imekuja na mfumuko wa wanafunzi haijawahi kutokea. Sasa unakuta darasa la kwanza lina limeandikisha watoto 400+, halafu kulingana na upungufu wa walimu, wanapangwa walimu wawili tu kufundisha watoto 200+ kila mmoja.
Je, iwapo mtu atafika darasa la nne bila kujua kusoma na kuandika, nani alaumiwe?
Mh. Rais, tafadhali okoa watoto wa wakulima, wanyonge wenzetu ambao hawawezi kupeleka watoto English medium.
Basi angalau ikama ya waalimu isome 1:60 angalau itasaidia waalimu kuwachunguza wanafunzi wao lkn ikifika standard ya 1:45, itakuwa njema kabisa.
Tafadhali mh, tusaidie