Mh Rais Magufuli saidia kumpunguzia majukumu RC wa Simiyu maana yatamzidia

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,863
Mh.Rais John Pombe Joseph Magufuli.Tunakutakia kazi njema,katika safari ya maendeleo ya Taifa uliyoiomba bila shuruti.

Wakati unapoendelea kutimiza majukumu yako,sisi wakaa pembeni tunazidi kukumbusha ktk mambo madogo na makubwa uliyoahidi kusimamia.

Kubwa na la mwanzo ulilowahi kutuahidi,ni kuhakikisha kuwa katika uongozi wako hakuna kiongozi atakayekuwa na "kofia mbili za uongozi" iwe ktk serikali au nje ya serikali.

Umeyafanya hayo kwa Nape Nnauye,kwa kuchukua ukatibu uenezi na kumuachia Uwaziri,umefanya hivyo kwa Polepole,kwa kuchukua Ukuu wake wa Wilaya na kumpa Ukatibu Mwenezi wa chama.Hii ni kwa sababu unaamini ktk vyeo viwili ufanisi unapungua.

Msaidie Anthony Mtaka,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuweza kumpunguzia cheo kimoja.Mtaka ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na pia ni Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania.

Hii inapunguza ufanisi,inaleta uzito ktk kutimiza majukumu katika kofia moja ya uongozi.Kutumikia siasa na michezo kwa wakati mmoja inaleta "fujo" za mipango na kimkakati.

Wakati huu kuelekea [HASHTAG]#OlympicTokyo2020[/HASHTAG],tunahitaji kujiandaa na kuwandaa kina Simbu vizuri na kiushindani.Harakati hizi za kuelekea Tokyo2020,London Marathon nk,tunahitaji watu wenye kujitoa kwa muda na hali.

Wakati Mtaka kama RC wa Simiyu akiwa ameelekeza nguvu nyingi kwenye kampeni yake ya "Wilaya moja,Kiwanda Kimoja",tunaamini nguvu hizo hawezi kuzigawanya na kuzielekeza kwenye ustawi wa riadha Tanzania.

Mtaka anakimbizana na kasi yako JPM kuelekea 2020 na huku akijiandaa pia ktk harakati za kugombea ubunge Jimbo la Musoma Vijijini mwaka 2020.Apunguze cheo kimoja ili kuuachia uongozi wa raidha nafasi nzuri.

Inajulikana tu,cheo cha Urais wa Riadha inaweza kuwa njia ya kutafuta "political Milage" kutoka 2010 kuelekea 2015,katikati yake akakutana na Ukuu wa Wilaya ya Mvomero,Hai na hatimaye Ukuu wa Mkoa wa Simiyu.Njia hizi walitumia kina Idd Azan na chama cha mpira Kinondoni kuelekea Ubunge wa Kinondoni,kina Rage na Uenyekiti wa Simba kuelekea Ubunge wa Tabora Mjini nk.

Ni ombi zuri,kuelekea [HASHTAG]#OlympicTokyo2020[/HASHTAG],kofia hizi mbili za RC Simiyu,moja ikabidhiwe kwa mwingine,na kama itakupendeza Mh.Rais,basi utusaidie kuipunguza kofia moja ili kutoa nafasi ya ufanisi na kuenenda na kauli yako ya kupunguza kofia moja ya uongozi kwa kila mteule wa Serikali yako.
Medali za dhahabu,shaba na fedha zitapatikana katikati ya mikakati isiyo na harufu ya kisiasa.Uongozi aa michezo unaosukumwa na kutafuta "ngazi ya kisiasa" inaweza kutufanya tuendelee kuwaongelea kina Filbert Bayi wa zamani bila kuzalisha wale wa kizazi cha sasa.
[HASHTAG]#TununueChakiZaMaswa[/HASHTAG]
[HASHTAG]#WilayaMojaKiwandaKimoja[/HASHTAG]
[HASHTAG]#RiadhaTanzania[/HASHTAG]
[HASHTAG]#AchiaCheoKimoja[/HASHTAG]
 
Ivi Rais wa Shirikisho la Riadha naye huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
kama jibu ni hapana basi wajumbe na wadau wa riadha mna haki ya kumvua huo urais sio mpaka Rais atengue uteuzi wake.
alafu haya mambo ya michezo si ata Nape anaweza yamaliza?
 
Kama watu wa kwenye michezo huko anao waongoza wakiona haendani na kasi yao si ndiyo wana paswa kumtoa!? Nadhani hiyo ndio ingekuwa njia rahisi
 
Ivi Rais wa Shirikisho la Riadha naye huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
kama jibu ni hapana basi wajumbe na wadau wa riadha mna haki ya kumvua huo urais sio mpaka Rais atengue uteuzi wake.
alafu haya mambo ya michezo si ata Nape anaweza yamaliza?
Au njia rahisi ni Rais kumpunguzia kile cha Ukuu wa Mkoa
Ili abakie na Urais wa Riadha....Nape anapata kigugumizi sbb huyu ni kada
 
Au njia rahisi ni Rais kumpunguzia kile cha Ukuu wa Mkoa
Ili abakie na Urais wa Riadha....Nape anapata kigugumizi sbb huyu ni kada
Mbona Rais yeye ana vyeo kibao.
mara amiri jeshi, mara mwenyekiti wa chama tena bila kusahau ndo Rais.
Tumwache mkuu wa mkoa nae afaidi japo tuvyeo tutatu ivi kakiwemo na ka mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.
 
Kumbe huyu jamaa ndio Rais wa Riadha?
Aliwahi kuwa mwanariadha ktk maisha yake?Au ndio zile za kuchukua vyeo ili utumie kupata jukwaa la kisiasa??

Mzee wa misifa,Watendaji Simiyu wanamtaja kama RC mwenye dharau na majigambo sana!!Vyeo vinawazidi hawa watoto...

Huyu hata huko Fb ukiona ameandika ujumbe,basi ni herufi kubwa mwanzo mwisho!!Herufi kubwa hovyo hovyo ni sawa na kupiga kelele!!

Wakati mwingine maandishi husadifu uwezo wa mtu kichwani na fikra zake!!
 
Back
Top Bottom