Mh. Rais wa JMT, historia inaonyesha kwamba polisi pengine huacha "akili" zao majumbani mwao wakiwa kwenye utekelezaji wa kuzuia maandamano. Mambo wanayofanyaga hayawezi kufanywa na binadamu yeyote yule aliyekamilika.
Polisi huwa hawachagui nani anahusika na nani hahusiki; wanapiga kila mtu, kila sehemu, mpaka kichwani. Uwe ni mgonjwa, mlemavu, mzee, wao wanapiga tu.
Polisi husimamisha magari (ambayo hata hayahusiki na maandamano) na kuvunja vioo, kupiga abiria waliyo ndani ya gari, na huenda hata huwa wanasababisha upotevu wa mali za abiria (raia).
Kwahiyo, Mh. Rais, ili kuondoa usumbufu kwa raia watakaokua wanakwenda kazini, shuleni, vyuoni, au kwenye shughuli mbalimbali, ifanye Septemba mosi 2016 kuwa siku ya mapumziko.
Hii itasaidia wale wasiyo na nia ya kwenda kwenye maandamano kubakia majumbani mwao.