barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Leo Mh.Rais wakati akiwaapisha maafisa wa Polisi wa vyeo mbalimbali amenukuliwa kwa kusema haya;
"Niliipinga hii dhana ya Polisi jamii tangu nilipokuwa waziri wa uvuvi, ifike kipindi Polisi aheshimiwe, ifike kipindi ukikutana Polisi na Raia Polisi AOGOPWE, yani umkute Jambazi alafu usimkamate kisa polisi jamii, Polisi AOGOPWE"
Rais akaendelea kusema kuwa Polisi hatakiwi kubembeleza,huwezi ukawa polisi una bastora kiunoni na bunduki mkononi halafu unashangaa shangaa tu kwa kigezo cha Polisi Jamii,akaendelea kusema kuwa kuna wakati huko Chato watu walivamia kituo cha Polisi,wakachoma moto kituo na kutoweka halafu mkuu wa kituo akawaacha tu kwa kigezo cha "Polisi Jamii"."Hii Polisi Jamii ndio nini??" ,Rais anasema ilitakiwa kwa tukio kama lile polisi "wawalaze chini raia".
Huwezi kuwa Askari halafu unashindwa kutumia silaha,unakuta polisi yupo ndani ya ziwa,anakutana na jambazi wanaanza kujadiliana kwa kigezo cha Polisi Jamii badala ya "kumlaza chini" jambazi,ukimlaza chini hata ndugu yangu kwenye tukio kama hili hata mimi nitakupongeza anasema JPM.
Kauli hii ya Rais haiwezi kupita hivihivi bila kujadiliwa,hasa ukizingatia kuwa kauli ya Rais ni kama sheria.Kuubeza mfumo wa Polisi Jamii si jambo lenye afya,hasa ukizingatia kuwa aina hii ya mfumo imesaidia sana kufichua majambazi na wahalifu mtaani.Polisi Jamii imeleta "urafiki" wa kweli na usio na mashaka kati ya polisi na raia.Hii hali ya kutaka kurudisha jeshi la polisi liwe kama la mkoloni,kwamba ukimuona polisi basi unamkimbia au kujificha halitaleta ufanisi wa pamoja katika kuzuia uhalifu.
Mamlaka zinapaswa kujuwa kuwa hawa polisi ni watoto wetu,vijana wetu,baba zetu,wajomba,shangazi na mama zetu,kujengeana mazingira ya "kuogopana" ni kurudisha juhudi na mafanikio yaliyofikiwa sababu ya ubora wa Polisi Jamii.Hawa Polisi ni wapangaji wetu na ndio wakopaji wa sukari na unga kwenye maduka yetu,tuachwe tuwe nao kwa pamoja ili tusiwaogope na kuacha kuwakopesha unga na sukari.Tukilazimiahwa kuwaogopa polisi basi tutalazimika hata kuogopa kuwapangisha na hivyo kukosa makazi sabbu ni ukweli kuwa "Police barracks" hazitoshi.
Polisi Jamii imesaidia sana kufichua uhalifu na aina zote za ujambazi huku mitaani.Juzi imekamatwa mitambo na mihuri bandia eneo la Buguruni na Kamanda Sirro akasema hayo yote yamewezekana sbb ya Polisi Jamii,sasa Rais anapoikataa hii dhana ya Polisi Jamii watu kama Kamanda Sirro kwanini wanakaa kimya?bila dhana ya Polisi Jamii wale watu waliovamia kituo cha Polisi Stakishari wasingegundulika kukaa katika msitu wa Kisarawe kama si wananchi chini ya dhana ya Polisi Jamii.
Uhalifu mwingi unaobainika huku mitaani ni kwa sababu ya dhana ya polisi jamii,kitengo hiki kimekuwa na manufaa makubwa mpaka kuundiwa ofisi makao makuu ya jeshi la Polisi ambapo CP Mussa Alli Mussa anakiongoza kitengo hiki.
Haijapita mwezi Rais alifungua kitengo cha "Police Call Centre" kwa ajili ya watu kutoa taarifa za uhalifu kwa jeshi la polisi na hii ndio dhana ya "Polisi Jamii"...Sasa Rais anapokuwa haoni umuhimu huu je kuna nini na maana gani kufungua hizi "call centre" ambazo msingi wake ni dhana ya Polisi shirikishi ambayo ni polisi jamii??
Tusiibeze Polisi Jamii,inaweza kufikia wakati raia wanasikia au kujua mipango ya wahalifu kuwavamia polisi au vituo vya polisi na wasitoe taarifa,sababu Rais kaagiza tuwe "TUNAWAOGOPA POLISI" na Polisi wasiwe na "urafiki" na raia.
Tunampenda Rais wetu,tuna imani nae,lkn hatutaacha kumkumbusha pale tunapohisi kuwa kauli zake zitaleta mkanganyiko.
Mungu ibariki Tanzania,Mungu libariki Jeshi la Polisi.