Mh Rais amefanya mazuri je amefanya? Hili ndio swali gumu

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,221
Ndugu zangu watanzania mm sipendi Kuwa mnafiki pamoja nampongeza Rais wangu Magufuli ila naumia Sana ninapo wasikilizaupinzani hata kama nichizi au umelamba benders za chama kuna msg nzito Sana hawa jamaa wanatupa Sisi watanzania na Taifa Kwa ujumla.

Watu hatuelewi na watu tumekuwa kama watu walio ktk mapango na hili linaibuwa maswali magumu na mazito Kwa muktadha wa Taifa. Hili.

Mzee Mmoja akiwa na malengo na shabaha kubwa kuijenga familia yake aliwekeza pesa na mitaji ktk maendeleo na akasahau familia yake mke na watoto walikuwa Wana muhitaji Yani ule umoja wa familia aliongoza familiaa yake vizuri akajenga magorofa na magari akanunua ila hakuwahi Kuwa na muda na familia yake mke na watoto wakajadili vipaumbele vyake na Kule Wana elekea. Watoto walisoma ila hawakuwa na furaha ya Mali Baba Yao kapata magari yapo ila hata mke haendeshi wala watoto hawayagusi. Mbaya walikula Kwa shida na wakati mwingine maisha Yao na ya Baba alie onekana nimwenye uwezo hayakuwa yakifanana. Nakila wakitamani kuuliza. Baba huwa mkali na mwenye kufoka Jambo hili liliwakwaza watoto Sana nakujiona wasio na thaman pamoja na utajiri Baba Yao alikuwa nao. Baba mkali asie na huruma wala muda na familia.

Miaka ilienda na watoto walikuwa na Mungu akawapa maisha Yao ila amino usiamini hawakuwa na muda na Baba Yao hata SIM japo mama walimpenda na kumkumbuka hata wakati mwingine kumuita wakae naye. Mzee alipo tamani kuwaona watoto walimtumia pesa ila hawakwenda kumuona Mzee Yule akiwa ktk majumba yake akashuka ghorofani aka kaa chini maana hakuwa na uwezo kipanda ngazi tena nyumban ulikuwa pweke na magari alinunua hakuna hata mtoto alitamani kuendesha maana walikuwa na ya kwao ndipo siku moja Mzee akavunja ukimya nakuwauliza wanae jamani kwanini hamji kuniona, watoto wakamjibu Baba he ulipokuwa ukitafuta uliwahi Kuwa na muda na Sisi,? Mzee alibubujika machoz ila miaka ilipozid kwenda Mungu akamchukua Yule Mzee amino usiamini malizake watoto walipiga mnada kweupe Kwa uchungu maana walipoziona walikumbuka ubeberu wa Baba shida na mateso walipita.

Ndugu zangu Taifa nisawa na familia na kamwe usije danganyika eti Taifa linatofaitiana na familia . Mh Rais amefanya mengi Sana ila amefanyaje ndio swali gumu litautesa utawala wake Kwa miaka mingi ijayo. Watu watasema amefanya kile na kile ila tukumbuke watu wameishi Kwa dhiki kuijenga Taifa kama kuna MTU hajapata ajira wala kuongezwa mshara kisa tunakenga nchi Kesho mtoto wake hatosema mazuri ya Yale utakuwepo. Habari za watu wasio julikana kubanwa Kwa vyombo vya habari na kutwezwa utu wa watu just because ni Rais kasema kutaigarimu Sana serikali yangu ya ccm na utawala huu.
nilikuwa mahalo MTU akasikia mkuu kamtumbuwa MTU akawa Hana hata muda kusikia maana umekuwa kawaida nilazima tujenge umoja wakitaifa tutake ama tusitake maana Taifa lisilo na umoja nimakazi ya shetani.

Watu wanasema nini kimetokea Libya watu waliokuwa wakipata kila kitu nakufurahia KAZI nzuri ya Rais wao. Watu walikuja kugunduwa wanatafunana wenyewe Kwa wenyewe na Kwa kipindi kirefu wakaja gunduwa anaye waongoza ndie anawala. Why Usimseme vibaya Ghadafi umepotea hii hali ikatengenezewa chuki Kali na mwisho Libya pakawa mahali pa vita.

Ndugu zangu hivi kweli watanzania wakifungua waone habari moja Tu ccm na hawapati taarifa nyingine mnategemea nn kitatokea? Hivi kweli ktk kila watu Mia alie msema vibaya Rais atapotea na kupigwa vibaya nini raia watatafasiri?
Tumejenga miundo mbinu yes we do makini tumejenga je na hapo ndipo kipimo cha serikali kipo ubabe na vitisho kamwe havijengi Taifa ila vinalibomoa nakuliangamiza.
Hayo ndio Naomi yangu.
 
Ujenzi wa Roma, Ulaya na Amerika haukufanikiwa bila watu kuteseka na vita nyingi tu zilitokea na kuwatenganisha watu.
Jambo zuri la maendeleo ya kudumu linakuja na changamoto zake nyingi sana.

So far, So good, So fresh, So clean, Magufuli is doing great job in shrewd manner.
 
Baada ya Lisu kurejea na kupata halaiki za watu, baadhi ya wanaccm wachache wanaanza kukiri ukweli, japo kwa kuchelewa. Ni hali ya kujiuliza sana kiongozi uongoze watu kwa miaka mitano hutaki mtu yoyote aongee tofauti, uwafanyie vibaya wapinzani wako wote wa kweli, wapambe wako wakusifie tu. Mara atokee mpinzani uliyejiaminisha na kuaminisha umma kuwa ni mtu mbaya, kisha apate mashabiki lukuki, tena wawe wanamkubali mchana kweupe. Hiyo hali kama una akili timamu lazima ujiulize unakwama wapi, na tatizo hasa na nini.

Ukweli ni kuwa watu wanataka mabadiliko, na hawajayapata huko ccm. Hivyo isidhaniwe miundombinu ndio mabadiliko, bali miundombinu ni mahitaji halali ya walipa kodi, wala siyo hisani au tiketi ya kuhujumu upinzani. Kuumiza, kuteka, kufunga ama hujuma yoyote dhidi ya wapinzani wako, hayawezi kuzuia mabadiliko yanayotakiwa.
 
Ubinafsi unakutafuna huwezi kuona Tanzania ya leo na kesho, wewe ni miongoni mwa mnaoombea wazazi wafe mapema mpate urithi. MPUMBAVU!
 
Ngoja Uchaguzi upite maana naona nahau zimekua nyingi kupitiliza.
 
Ameeeen
Watawala wangefikiri hivi wangekuwa wapole kuliko ilivyo sasa kila mtu anaonyesha umwamba
Nape ana jeuri leo
Hii nchi ni yetu sote
 
familia yenye uwezo wa kifedha na mali nyingine haimaanishi kuna amani ndani yake.

nikupe mfano wa familia 2....

kila familia ina mume 1 na mke 1 na watoto 3. familia ziko kwenye generation moja, familia marafiki.

familia ya kwanza baba ana uwezo wa kuwapeleka watoto shule Ulaya (kuanzia primari hadi univesiti). life style yake pia iko daraja la juu.
familia ya pili ni tia maji tia maji... watoto wanasoma hapa hapa bongo shule za huko mtaani bei poa. life style yake ni chips dume.

baba wa familia ya kwanza anaishi kwa uhalifu ikiwemo ngada, ujambazi wa kuua watu. mama wa familia tumbo joto kila siku!
baba wa familia ya pili anafanya kazi ya umeneja kwenye kampuni ya Wadosi. mama wa familia ana amani.

baadhi ya watu wanaozijua familia hizi lakini bila kujua undani wa chanzo cha kipato cha kila familia, wanamnanga sana baba wa familia ya pili kwamba eti ni mzembe kwa nini hana mafanikio kama baba wa familia ya kwanza. kwa upande mwengine kuna baadhi ya watu wanaoujua undani wa vyanzo vya vipato vya familia zote 2 - hawa wamekuwa wakiwaasa wale wanaomnanga baba wa familia ya pili kwa kuwafahamisha kuwa baba wa familia ya kwanza kipato chake anakipata kwa njia ya uhalifu na mauaji.

awamu ya 5 ni kama familia ya kwanza. hofu kwa wananchi!
vyama mbadala ni kama familia ya pili. amani kwa wananchi!

UTAJAZA!
 
Ujenzi wa Roma, Ulaya na Amerika haukufanikiwa bila watu kuteseka na vita nyingi tu zilitokea na kuwatenganisha watu.
Jambo zuri la maendeleo ya kudumu linakuja na changamoto zake nyingi sana.

So far, So good, So fresh, So clean, Magufuli is doing great job in shrewd manner.
Anayetwambia tuteseke yeye yuko na uhakika wa watoto wake kupata elimu nzuri,kulala pazuri,watoto wake&ndg zake kupata kazi nzuri sehemu yoyote ile waitakayo,ana uhakika wa matibabu bora kabisa,ana uhakika na mafao yake siku tu amestaafu wkt wanyonge wanasubiri hata miaka mitatu hawajapewa mafao yao baada ya kustaafu.

Yaani anaewaambia watu wavumilie yeye hajui hata maumivu wanayopitia wananchi maana yeye na seniors wenzake serikalini wanaishi kama malaika.

Unafiki ni hatari sana aisee.
 
Yaani nape ni takataka, kwanza mwanaume akishakuwa na maneno kama muimba taarabu tu basi tunamtoa maana
Ameeeen
Watawala wangefikiri hivi wangekuwa wapole kuliko ilivyo sasa kila mtu anaonyesha umwamba
Nape ana jeuri leo
Hii nchi ni yetu sote
 
Back
Top Bottom