Mh. Pombe Ahadi zako vip??

Aug 22, 2016
34
125
Me ni mmoja wa watu ambao huwa sipigii kura mgombea wa CCM, kwa kuamini Chama cha Mapinduzi sio cha kuaminika, na hakina lengo la dhat la kumkwamua mtanzania wa hali ya chini...

2015 kwa bahat tu ukatokea J. Pombe Magufuli, binafsi sikukupigia kura sababu sikuwa na iman na wewe, nilipoanza tu kufuatilia kampeni zako...

ila kwa Ahad zako tamu ambazo nyingi zilifanana na zile za UKAWA, pia kutokana na Makeke yako hasa jukwaani watanzania ambao wengi wao ni maskini wa kipato na fikra licha ya kuchoshwa na chama chako cha CCM wakaamua kukuamin wewe, wakaamin kweli una lengo la dhati la kuleta mabadiliko..

Ukashinda uchaguzi..japo kwa nguvu ya ziada..

Me niliamua kukupa Hongera, mana ndio siasa za Africa!

Sasa Mheshimiwa sana naamini Hao ma hohe hahe wenzangu na mie waliokupigia kura, walikupigia tu sabab ya ahad zako, si ndio? Bas fanya iwe Simple tu Timiza ahadi zako! Sio kila siku kutusomea umepata mahela kias gani, wakat sie tunalia njaa...

Ukumbuke Watanzania wengi walipoteza Muda wao kupanga foleni siku ya uchaguz wakakupigia kura sabab waliamin katika ahad zako...

Miez, mara miaka inakatika sasa bado tu...unafikir tunaishi vip?...wale vijana uliowaahid ajira unataka uwape ajira uzeeni???

Au Mheshimiwa bado una miaka mingi ya kuwa madarakani hivyo tusiwe na presha ..utatekeleza ahadi zako mwaka 2040??

Ujue Sitaki kuamin kwamba uliahid vitu ambavyo hauwezi kuvitekeleza km kawaida ya CCM.!

Sasa Mheshimiwa em fanya kweli aysee....kumbuka ulipiga had push up kutuomba KULA, ukacheza mpaka bongo fleva jukwaani bas Timiza ahadi zako bana wapinzani wakose cha kusema 2020!!!
Au la Tangaza umeshindwa, ujue msema kweli mpenzi wa Mungu.....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom