Mh.pinda utakuwa na majibu ya papo kwa papo katika hili?

Mujuni2

Senior Member
Jun 11, 2008
142
3
Mh. Waziri mkuu, Miizengo Kayanza Peter Pinda, umekuwa mwepesi wa kutoa majibu ya papo kwa papo kwa maswali yanayohitaji uchunguzi wa kina. Sasa hili la Gongo la Mboto natarajia utatumia umahiri wako Mungu aliokujalia kutoa majibu ya papo kwa papo. Ila Mh. kama ulivyonyoosha kidole kwa wale uliowatuhumu ni waanzilishi wa vurugu za Arusha , basi nategemea kidole hicho hicho kitaelekezwa kwa WAHUSIKA wa Mabomu ya Gongo la Mboto na nina hamu kusikia nani atawajibika? Mungu aendelee kukupa ujasiri kama aliokupa alhamisi ile ukiwa bungeni Dodoma.
 
Anawajua wahusika wa mabomu ya g/mboto si wale maaskari waliokuwa wanahifadhi mabomu ni chadema damu kwa hiyo ndo maana wamesababisha umwagaji damu.
 
Pinda keshaingia usanii hakuna tena kazi ni starehe na picha na maneno ya uongo kwa wananchi....
images

Ngoja jinsi gani atageuza hiyo picha juu kutoka hapa (only Pinda can do it)
images
 
Back
Top Bottom