Mh Pinda na Mh Luhanjo nani mwenye mamlaka zaidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Pinda na Mh Luhanjo nani mwenye mamlaka zaidi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jul 28, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,471
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Bado najiuliza jamani kuhusu swala la jairo
  mh pinda alidai bungeni kwamba kama yeye ameshapata majibu ya swala hili
  lakini utokana na mtu huyo kuteuliwa na rais anaitaji kusubiri mapaka rais
  aje na akiwa anasubiri rais kikwete kufika mh luhanjo akatangaza kumpa mh
  jairo likizo ya malipo

  swali langu huyu waziri mkuu na mh luhanjo nani mwenye mamlaka nahisi
  tuna bomu la waziri mkuu asiejua mamlaka alionayo...nimefika kujiuliza hiki
  na kuendeelea na mambo mengine kusubiri siku kumi za jairo
   
 2. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rostam
  mix with yours
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Tumuulize Juji Mkuu, labda katiba itatupa jibu halisi, maana hili ni suala la katiba. kama katiba haina jibu, basi anajua Kikwete
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Tumuulize Jaji Mkuu, labda katiba itatupa jibu halisi, maana hili ni suala la katiba. kama katiba haina jibu, basi anajua Kikwete
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  Luhanjo anateuliwa na Rais kusimamia shughuli za ikulu.

  Waziri Mkuu anateuliwa na Rais kusimamia serikali nzima na zaidi lazima aidhinishwe na Bunge ambacho ni chombo cha juu kabisa cha kutunga sheria za nchi na ni moja ya mihimili ya dola:

  Hapo jibu umeshapata.
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  futa basi hiyo post ya kwanza sawa mkuu..
   
 7. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Unanikumbusha sakata la ole sendeka na mkuu wa mkoa.
  Hapa nchini kwetu UKIJIAMINI wewe ndio zaidi.
   
 8. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Luhanjoooooo!
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo sasa ndipo kuna mchanganyiko mkubwa!! PM anasimamia serikali nzima na anapitishwa na Bunge (wawakilishi wa wananchi) cha kushangaza ni kwamba sheria hazimpi meno hata ya kumsimamisha kazi naibu katibu makuu achana na waziri yeyote! PM anaweza kuwasimamisha kazi (si kuwafukuza) wahasibu na wakurugenzi wa Halmashauri tu basi (Kumbuka Bagamoyo). Kwa upande mwingine yupo Katibu Mkuu Kiongozi ambaye kwa mujibu wa sheria ni mkuu wa utumishi wa umma. Huyu anateuliwa na Rais na hapitishwi na Bunge lakini ana nguvu (Kisheria) za kuwasimamisha kazi watendaji wa serikali walioteuliwa na Rais ispokuwa Mawaziri na Manaibu waziri. Hapa unaweza kuona kwamba Waziri Mkuu ambaye anasimamia shughuli za serikali hana meno japo ya plastiki, mwenye meno kwa watumishi wa umma ni Katibu Mkuu Kiongozi! Kwa mantiki hiyo basi Katibu Mkuu Kiongozi ana Mamlaka zaidi! Au hutaki?
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Luhanjo ni Katibu Mkuu Kiongozi na si Katibu Mkuu wa Ikulu!! Hashughulikii masula ya Ikulu tu anashughulikia utumishi wa umma kwa ujumla wake. Inabidi katiba ijayo inyooshwe ipasavyo.
   
 11. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Mkuu nadhani hili ndilo jibu kamili nimelikubali, maana hata RA ndio alikuwa zaidi hata ya Kikwete.
   
 12. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hapa umepotosha Mkuu si hivyo hata kidogo kuna kitu hujakijua hapo.

  Waziri Mkuu ana meno na ndio Mtendaji Mkuu katika serikali pia anaweza kuwasimamisha kazi hao wote uliowasema kama akiamuwa ila kwa ajili ya kuheshimu Protoko ndio maana alisema anamsubiri Rais, lakini kwa taarifa yako PM ana nguvu kuliko hata Makamu wa Rais katika nchni kwa mujibu wa katiba ya nchni hii; swala la Jairo inaonekana ni Kikwete alipindisha sasa waziri Mkuu hawezi tena kuja kwenye public kutangaza kitu tofauti na kile alichokisema awali ndio maana wakatumia Luhanjo, Luhanjo hana meno kuliko PM ila ndio Mamlaka ya Nidhamu kwa Makatibu wakuu wote na pia Usalama wa taifa wanaripo kwake (Ni kama useme kuwa Katibu Mkuu wa wizara ana nguvu kuliko Waziri si kweli) kama sehemu ya muundo wa serikali kuu ila siyo decision maker Waziri Mkuu ana mamlaka ya Makuu katika Decision na ndio maana katiba inatambuwa kuwa hata uteuzi wa mawaziri Rais anapaswa kuunda baraza kwa kushauriana na PM.
  Luhanjo ni kama team Leader kwa wataalam ambao kazi yao kuu ni kuishauri Decision team ambayo ndio yenye mamlaka yote na Maamuzi yote juu ya serikali; Decision team ni Rais na Waziri Mkuu wakisaidiwa na Mawaziri wao.
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hakika nakuambia Waziri Mkuu hana meno kama unavyofikiria. Kama si mamlaka ya nidhamu ya nidhamu anawezaje kuchukua hatua za kinidhamu kwa watendaji? Kufukuza mtu ama kumsimamisha ni hatua za kinidhamu mkuu. Angalia vizuri muundo wa serikali ili ujiridhishe na mapungufu yake. Nakumbuka wakati wa Mkapa kulikuwa na Waziri mmoja ambaye alikuwa na nguvu sana serikalini na kuna wakati alimvimbia waziri mkuu akimwambia kwamba yeye ni mteule tu wa rais kama ilivyo kwake yaani wote ni wateuliwa wa Rais. Hakika nakuambia Waziri Mkuu hana meno.
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hebu mkuu kwa kunielimisha tu naomba uniambie Waziri Mkuu ana uwezo wa kumfukuza mtumishi gani wa serikali?
   
 15. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Ni wazi yule aliyethubutu kumsimamisha Jairo ndiyo ana mamlaka.
   
 16. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii inaenda bila kusema Luhanjo yuko juu ya pindo
   
 17. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Hujui maana ya mamlaka ya nidhamu ndio kitu kinachokusumbua hapo na pia CS hana mamlaka ya kufukuza mtu yeyeto kazi kama hujui hilo. Tafuta maana ya hilo neno linalokusumbua utaelewa.

  Kila Mfanyakazi anapaswa kufukuzwa kwa mujibu wa sheria na taratibu kama hujui. Tofauti ni kuwa Kama umefanya kosa ambalo si la jinai (makosa ya kiutendaji) Mamlako yako ya nidhamu inakuchunguza na kubaini kilichopo alafu inashauri kwa mamlaka ya maamuzi ambayo kwa kesi ya Jairo Mamlaka yenye maamuzi juu yake ni Rais na PM.

  Kama umefanya kosa la jinai mamlaka yako ya Nidhamu haina nguvu tena vyombo vya dola vina mamlaka ya kukuchunguza na kumkabidhi DPP Jalada lako kwa hatua za kufikishwa Mahakamani na hiki ndicho walichokikwepesha hapa ambacho watanzania wengi hawajui. Katika kesi ya jinai hata mamlaka ya Maamuzi haina uwezo wa kimamlaka ya kuzuia husichunguzwe ila wanaweza kuzuia kufikishwa kesi Mahakamani kupitia kwa DPP, maana DPP ana mamlaka yake pia ya kuzuia kesi hisiperekwe Mahakamani kama haina maslahi kwa taifa.
   
 18. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kwani Jairo kasimamishwa? Jairo kapewa likizo ya lazima, na hilo liko ndani ya uwezo wa Katibu mkuu kiongozi. Kuwa likizo ya lazima maana yake unaondolewa ofisini lakini utaendelea kupata mshahara kama kawaida. CS hana mamlaka ya kumsimamisha kazi Katibu mkuu wa wizara ila yeye anamshauri Rais ambaye ndo mwenye mamlaka hayo. Ila masuala ya nidhamu kama vile uchunguzi CS ndo mwenye mamlaka hayo ili baadaye imsaidie kumshauri Rais hatua za kuchukua.
   
 19. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 448
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa mara nyingine tenna ni mpango wa jk kumfanya pm aonekane hana nguvu. Jk is negatively smart. Alishindwa nini kumwambia pm amwajibishe jairo baada ya kumpa taarifa? Kama inavyompendeza rais, akaamua kumpa jukumu hilo luhanjo ili lisifike tena mikononi mwa pm. Lakini kama siku ile mlimsikia vizuri luhanjo. Alisema, 'mimi ndiye mwenye mamlaka ya kumwajibisha mtumishi wa umma...'
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu sikubaliani na wewe hapo kwenye wekundu. PM hana meno juu ya Katibu Mkuu ama Waziri yeyote. Naomba kifungu tafadhali
   
Loading...