Mh. Noni anaendelea kutanua huko tib au vipi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Noni anaendelea kutanua huko tib au vipi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Dec 25, 2010.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tangu Noni ateuliwe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIB benki hiyo imekuwa inategewa fedha za kutosha kwenye bajeti. Katika bajeti ya mwaka huu ilitengewa fedha eti za kukopesha kwaajili ya kilimo. Kwa mtu mwenye akili lazima ujiulize, inakuwaje kwa benki kama TIB ambayo haina mtandao wowote hapa nchini, ikapewa jukumu la kutoa mikopo kwaajili ya kilimo, kwa wakulima walio sambaa nchi nzima ? Mbali na hayo, kuna hili suala la madeni sugu. Hivi sasa wadaiwa wote, waliokopeshwa na serikali katika mazingira yenye utata, yalihamishiwa yote TIB. Hii ni pamoja na fedha zilizolipwa na Benki kuu kwaajili ya mikopo ya makampuni iliyokuwa imeyatolea mdhamana k.m ililipa takribani bilioni 10 kwaajili ya kampuni ya mbunge wa zamani wa Sumbawanga Mh. Mzindakaya. Vivyo hivyo ililipa karibu shs bilioni 100 kwaajili ya Kagera Sugar. Hii ni mbali na mikopo ya pembejeo na import support ambayo yote kwa pomoja inakimbilia kwenye trilioni ya Tshs. Sasa swali langu, hivi hiyo mikopo ilihamishiwa TIB ili iweje?
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ili iwe mitamu zaidi!
   
 3. U

  Uswe JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  TIB = Tanzania Investment Bank, it is the only development bank in the country, sijui kama unalijua hili.

  kuna tofauti kubwa saaaana kati ya commercial banks, ambazo motive kubwa ni kumaximize profit, na development bank ambayo motive kubwa ni kuchochea maendeleo ya uchumi nchini, ndo maana benki kama tib inatoa mikopo ya muda mrefu kwa miradi ya maendeleo kwa riba nafuu na crdb wanatoa mikopo ya muda mfupi kwa mfanyabishara anayetaka kwenda kununua mzigo china aje auze harakaharaka, sijui ka unasaidika baada ya maelezo haya
   
Loading...