Mh. Ngeleja ameomba Kanisa Kumuombea ili kutatua Matatizo ya Umeme Nchini!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Ngeleja ameomba Kanisa Kumuombea ili kutatua Matatizo ya Umeme Nchini!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KING COBRA, Jan 2, 2012.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Wakati wa Salamu za Mwaka mpya Waziri wa Nishati na Madini Willium Ngeleja alisisimama Mbele ya Kanisa lake jimboni kwake na kueleza baina kuwa anaomba Askofu na Waumini wamuombee ili Matatizo ya Umeme yaweze kuisha.
  Alisema kuwa anashukuru Mungu kwa sasa umeme unawaka lakini amekubwa na matatizo hayo kwa mda mrefu sasa ambapo umeme hauwaki sehemu mbalimbali za nchi.

  NB.
  Mwaka jana Mh Engineer Stella Manyanya alimuuliza swali Mh Ngeleja Bungeni , kuwa umeme wa 132kv lini ya Askofu Kakobe hauwaki kwa sababu za Hoja za Kakobe.
  Mh Ngeleja alijibu Kwamba ni kweli umeme huo hauwaki na kwamba kuna matengenezo katika Nguzo namba 19 na namba 20 kwenye eneo la Kanisa la Kakobe lakini akakanusha kuwa matengenezo hayo ni ya kawaida na suala la umeme ni la Kisayansi na wala si la Kiroho , hivyo hoja za Askof Kakobe (Hoja za Kiroho kwa maana ya kuomba Mungu kuingilia kati) hazipo.

  Tarehe 15/12/2011 Ngeleja alianza tena matengenezo kwenye nguzo hizo hizo ambapo mafundi walitumwa hapo na Winchi lao kuzimika wakati fundi amepanda katika nguzo 19 kwa Kakobe.

  Sasa ni jambo la ajabu Ngeleja asiyeamini Nguvu za MUNGU kushughulikia umeme aombe tena msaada wa kanisa lake kumuombea!!!

  Pia ni kwa nini mradi ambao unagharimu 34bils ushindwe kuzinduliwa huku matengenezo yasiyoisha yakiendelea kwenye nguzo mbili tu!!!

  Katika matengenezo ya Nguzo hizo Wamefukuzwa mafundi wanne kwa Tanesco kwa hisia kuwa wanahujumu matengenezo hayo!!!.

  Umeme huo ulipangwa kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete mwezi wa kumu mwaka 2010 kwa kauli ya Ngeleja mwenyewe lakini mpaka sasa tar2/1/2012 haujazinduliwa!!
   
 2. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  source ; gzt mwananchi leo pg5
   
 3. M

  Mhabarishaji JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,001
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ngeleja, uwe na msimamo thabiti! Umeme ni Sayansi! Tumia wataalam wengi wa Sayansi, ulio nao katika Wizara yako. Achana na mambo ya kiroho! Sayansi, na mambo ya kiroho, wapi na wapi!
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  haya ngoja tuone mwisho
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,862
  Trophy Points: 280
  huu ni utaahira kama hawezi ni hawezi hata kama watu wafunge kwa maombi
   
 6. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Bunge:Luhanjo, Jairo waondoke
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 19 November 2011 21:00 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] LASEMA NGELEJA, CAG NAO WACHUKULIWE HATUA KALI

  Neville Meena, Dodoma
  KAMATI teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza uhalali wa utaratibu wa Wizara kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni, imewasilisha taarifa yake huku ikimkangaa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini aliyesimamishwa, David Jairo na Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo.

  Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Injinia Ramo Makani, aliliambia Bunge kuwa wengine wanaopaswa kuwajibishwa ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na, Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Ludovick Uttoh .

  Makani alisema baada ya kufanya uchunguzi wake uliowezesha kuwahoji watu 146, imebainika kuwa utaratibu uliotumiwa na Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kutoka katika taasisi zilizoko chini ya wizara hiyo kwa ajili ya kusaidia upitishaji wa bajeti bungeni, haukuwa wa kawaida na kwamba ulikiuka taratibu na sheria za fedha.

  “Fedha zilizokusanywa zilikuwa kwa matumizi ambayo yasingehitaji uchangishaji kwa sababu yangeweza kugharamiwa na kasma zilizopo za wizara,” alisema Makani na kuongeza:

  “Uchangishaji huo ulisababisha taasisi hizo kubebeshwa mzigo kwa kuwa hazina kasma mahususi kwa ajili ya kuchangia wizara kwa ajili ya maandalizi ya uwasilishaji wa bajeti bungeni”.

  Alisema utafiti ulibaini kwamba Jairo akiwa Katibu Mkuu aliomba fedha kiasi cha Sh180 milioni kutoka taasisi nne ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lililoombwa Sh40 milioni, Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) Sh40 milioni, Wakala wa Umeme Vijijini (REA) Sh50 milioni na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Sh50 milioni.

  Hata hivyo, kiasi kilichochangwa ni Sh140 milioni tu kutoka Tanesco, REA na TPDC wakati Ewura waligharamia chakula cha mchaka wa siku tatu pamoja na tafrija iliyokuwa imepangwa kufanyika baada ya kupitishwa kwa bajeti ambayo iliwagharimu Sh9.7 milioni.

  Makani aliongeza kuwa uchunguzi zaidi ulibaini kuwa mbali na fedha hizo, kulikuwa na kiasi kingine cha Sh428.8 milioni kilichotoka katika Idara mbili za Wizara hiyo ambazo ni Idara ya Uhasibu Sh150.7milioni na Idara ya Sera na Mipango iliyotoa kiasi cha Sh278 milioni kwa ajili ya kusaidi upitishaji wa bajeti.

  Alisema fedha zote hizo jumla yake ikiwa Sh568.8 milioni, ziliingizwa kwenye akaunti ya taasisi ya GST iliyopo mjini Dodoma lakini akasema kati ya hizo, Sh150.7 milioni zilikuwa kwa ajili ya gharama za vikao na semina na kiasi kilichokuwa mahususi kwa ajili ya uwasilishaji wa bajeti bungeni kilikuwa ni Sh418.8 milioni.

  Makani alibainisha kuwa maelezo waliyopewa na Wizara husika, walifikia uamuzi wa kuomba fedha hizo kutokana na fungu ambalo hutumika kwa ajili ya shughuli za bajeti kubakiwa na Sh35 milioni tu kati ya Sh207 milioni zilizokuwa zikihitajika.

  Hata hivyo, alisema Wizara haikuzingatia kanuni husika za fedha katika kuomba fedha hizo, na kwamba Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo alipohojiwa na kamati hiyo, alisema utaratibu uliotumiwa kwamba si halali.

  “Sababu zilizoifanya Wizara kuchangisha fedha haziwezi kutiliwa maanani kwa sababu hadi kufikia Juni 25, 2011 Wizara ya Nishati na Madini ilikwishakupata mahitaji yote ya fedha za uwasilishaji wa bajeti baada ya kupokea Sh171.5 milioni za matumizi mengineyo (OC) kutoka hazina,” alisema Makani.

  Kughushi nyaraka
  Kamati Teule ya Bunge pia ilibaini kwamba kulikuwa na vitendo vya kughushi na udanganyifu katika hesabu za gharama za uendeshaji wa semina ya wabunge ya Juni 26, 2011 ambayo iliendeshwa na Wizara ya Nishati na Madini.

  Kamati hiyo ilibaini kuwa ili kufanikisha semina hiyo, Jairo aliziandikia tena taasisi nne ambazo ni REA, Ewura, TPDC na Tanesco kutoa Sh22 milioni kila moja na fedha zote zilikusanywa na kufikia kiasi cha Sh88 milioni, fedha ambazo zililipwa kwa mhasibu wa wizara, Hawa Ramadhani.

  Alisema kwa mujibu wa barua hiyo, Jairo aliainisha kwamba bajeti ya semina hiyo ni gharama za ukumbi Sh39 milioni na posho kwa wabunge Sh46 milioni, hivyo kufanya mahitaji kuwa Sh85 milioni tofauti na kiasi cha Sh88 milioni kilichochangishwa.

  Alisema maelekezo yaliyotolewa na Ofisi ya Bunge kuhusu malipo hayo ni viongozi wa Bunge kulipwa Sh250,000, Wabunge Sh110,000, Wakuu wa Idara Sh80,000, Maofisa Sh50,000 na Watoa huduma nyingine Sh20,000.

  “Kamati Teule ilibaini kwamba baadhi ya viwango vya posho vilikuwa tofauti na maelekezo ya Ofisi ya Bunge. Kwa mfano wakati wabunge walilipwa Sh110,000 kila mmoja, ilionekana kuwa mtumishi wa ngazi ya mhudumu alilipwa Sh120,000, badala ya Sh20,000, wakurugenzi walilipwa Sh180,000 badala ya Sh80,000 na maofisa wengine Sh150,000 badala ya Sh50,000," alisema Makani.

  Alisema utata huo uliilazimisha kamati kumhoji Mhasibu aliyelipa posho hizo kutoka Wizarani na sababu za kutofuata mwongozo wa Ofisi za Bunge na kwamba, jibu la mhasibu huyo ni kwamba alipewa maagizo ya mdomo na mmoja wa wakurugenzi kwamba aongeze kiasi cha Sh100,000 kwa malipo wahudumu na maofisa wengine.

  Makani alisema hata hivyo walibaini kwamba malipo hayo yalighushiwa kwa kuongeza namba 1, mbele ya Sh20,000, Sh50,000 na Sh80,000 na kuzifanya kuwa Sh120,000, Sh150,000 na Sh180,000 kwa malipo hayo sawiya hali iliyosababisha upotevu wa kiasi cha Sh13.9 milioni.

  "Malipo ya nyongeza yaliyoongezwa kwa kila mtumishi ya Sh100,000 si halali bali ni ya kughushi. Kutokana na kughushi huko jumla ya kiasi cha Sh39 milioni ambazo ni asilimia 15 ya jumla ya fedha zilizokusanywa (Sh88 milioni) ni malipo hewa," alisema.

  Alisema kiasi cha Sh39milioni zilizotengwa kwa ajili ya malipo ya ukumbi pia ni dhahiri hayakutumika, kwani ukumbi uliotumika ni wa Bunge (Pius Msekwa) ambao ni wa bure kwani hauna malipo na kwamba watumishi wengine wanaotajwa kulipwa hawakuwapo Dodoma.

  Kamati Teule ilibaini kwamba Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa na watumishi 243 wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma, hivyo kuitaka Serikali kutoka mwongozo wa idadi inayostahili kwa wizara wakati wa bajeti.

  Ngeleja na Luhanjo

  Kamati hiyo ilisema Serikali ichukue hatua zinazofaa kwa Waziri Ngeleja kwa kuzingatia mwongozo wa wa Baraza la Mawaziri ambao unamtaja kuwa ndiye msimamizi mkuu wa Wizara na kwamba suala la uchangishaji wa fedha halikupaswa kufanyika bila yeye kujua.

  Makani alisema licha ya kutokuwa na uthibitisho moja kwa moja uhusika wa Waziri au Naibu wake katika uchagishaji uliofanywa na Katibu Mkuu, lakini hilo halimwondoi Waziri katika nafasi ya kuwajibika akiwa msimamizi mkuu wa Wizara.

  Kutokana na hali hiyo, Kamati hiyo imekosoa kanuni na taratibu za utendaji wa Wizara, ambazo ilisema zinatoa mamlaka makubwa kwa Makatibu Wakuu wa Wizara ambao huruhusiwa kufanya uamuzi mkubwa kuhusu masuala ya fedha bila kumshirikisha waziri husika.


  Kwa upande wake, Luhanjo anatakiwa kuwajibika kwa kile Kamati ilichosema kuwa ni kumsafisha Jairo kwa kuficha ukweli wa Taarifa ya Ukaguzi Maalumu uliofanywa na CAG mara baada ya kutolewa kwa tuhuma hizo bungeni.

  Makani alisema Luhanjo katika uamuzi wake ambao aliutoa mbele ya vyombo vya habari Agosti 23, 2001 hakuzingatia taarifa nzima ya CAG na badala yake alizingatia sehemu tu ya taarifa hiyo akilenga kumsadia Jairo kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe.

  Kadhalika taarifa hiyo ya Kamati Teule ya Bunge inabainisha kuwa, Luhanjo alikosea kutoa taarifa ya uchunguzi wake wa awali kwenye vyombo vya habari pasipokuwasiliana na Waziri Mkuu ambaye ndiye kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni na kwamba kwa kufanya hivyo alimfedhehesha kiongozi huyo.

  “Kitendo hiki hakikumtendea haki kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, kwa kuwa alikuwa ametoa kauli bungeni kuwa atalifikisha suala hili kwa mamlaka za juu na Bunge lilikuwa bado linasubiri majibu yake,” alisema.

  Alisema kauli ya Luhanjo kwamba Jairo angeweza kwenda katika vyombo vingine vya sheria kushtaki au kudai haki zaidi ni dhahiri kwamba alikuwa akishawishi kuvunjwa kwa Ibara ya 100 ya Katiba ya nchi hivyo kuingilia haki na madaraka ya Bunge.

  Uttoh na Jairo
  Makani alisema: “Kamati imesikitishwa sana na jinsi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alivyoshindwa kutekeleza wajibu wake kikamilifu, hususan katika kutoa ushauri na hitimisho katika ripoti yake na jinsi alivyotoa taarifa yake kwenye vyombo vya habari”.

  “Kwa kufanya hivyo ameshindwa kulisaidia Bunge na Umma kwa ujumla, badala yake amekuwa sehemu ya kuficha maovu. Hivyo Kamati Teule inapendekeza Serikali ichukue hatua zinazofaa kwa CAG kwa upotoshaji huo,”alisema Makani.

  Alisema kasoro ya taarifa ya CAG kwa vyombo vya habari, ambayo haikujibu hadidu zote za rejea alizopewa na badala yake alijikita katika hoja iliyokuwa imetolewa Bungeni kuhusu idadi ya taasisi zilizochangishwa na kiasi cha fedha Sh1 bilioni kilichokuwa kimedaiwa kukusanya.

  “Hatua hii ilikuwa ni upotoshaji mkubwa kwani taarifa nzima kwa ujumla wake ilikuwa na maudhui ambayo yangeweza kuonyesha makosa ya kinidhamu kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,”alisema Makani.

  Kuhusu Jairo, Makani alisema Katibu Mkuu huyo ambaye hivi sasa amesimamishwa, anapaswa kuchukuliwa hatua kwa matumuzi mabaya ya madaraka kwa kukusanya na kutumia fedha za umma na kuruhusu matumizi mbaya ya fedha za umma.

  “Vilevile Serikali iwachukulie hatua za kinidhamu, kwa mujibu wa sheria watumishi wote wa Wizara ya Nishati na Madini waliotajwa kwenye taarifa hii kushiriki kwa namna moja au nyingine katika uchangishaji na matumizi ya fedha hizi za umma,”aliongeza mwenyekiti huyo wa Kamati Teule.

  Miongoni mwa watumishi waliotajwa kwenye taarifa hiyo ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo ambaye alitoa ushauri usiofaa na wa upotoshaji wa kwa Katibu Mkuu kuhusu kuchangisha fedha huku akijua kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.


  Michango ya wabunge


  Wabunge wa CCM na wale wa upinzani,jana waling'aka wakitaka Serikali ichukue hatua kali dhidi ya waliotajwa katika taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Jairo kuchangisha fedha isivyo halali.

  Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema ubadhirifu huo ni matokeo ya mfumo mbovu wa utawala ambao unawalinda wezi wa mali ya umma pia kuwepo kwa mfumo wa malipo ya posho ambayo yanatoa mwanya kwa watendaji serikalini kufanya ubadhirifu.

  Mbunge wa Simanjiro (CCM),Christopher Ole Sendeka alisema Katibu Mkuu Kiongozi, Luhanjo na Jairo mbali na kuchukuliwa hatua za kinidhamu, wanastahili kufikishwa katika vyombo vya sheria ili washtakiwe.

  Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR Mageuzi), Mosses Machali yeye alisema lazima Serikali ichukue hatua kali kwa watendaji waliohusika na kwamba wasipofanya hivyo.

  Machali aliwataka Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima wajiuzulu ili kulinda heshima yao, hoja ambayo pia ilitolewa na Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli na Ezekia Wenje ambaye ni Mbunge wa Nyamagana (Chadema).

  Bunge lilipitisha maazimio ya Kamati Teule ambayo Serikali kupitika kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe ilisema itayafanyia kazi mapema iwezekanavyo na kurejesha taarifa bungeni katika mkutano ujao wa sita.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 7. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nimefuatilia , Ngeleja ni muumini wa Kanisa la AICT la Mlimani Mjini Sengerema linalo ongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Geita aitwaye Mussa Magwesela.
  Kwenye ibada ya mwaka mpya Ngeleja aliwangukia waumini wa Kanisa Lake na Kuwaomba Wamuombee Matatizo yake hasa tatizo la Umeme.

  Ngeleja alisema tangu Rais Kikwete amuteue kuwa Waziri wa Nishati na Madini amekuwa akikumbana na matatizo mengi likiwemo tatizo la umeme kutowaka !!!

  "Wizara yangu inachangamoto kubwa zinazotishia nafasi yangu ya uwaziri ni Vita kubwa ninahitaji maombi kwa mwenyezi Mungu ili kushinda vita hii.

  Baada ya Kusikiliza Maombi ya Ngeleja Askof Magwesela alisema Changamoto hizo zinatokana na ibirisi kutaka kupokonya mamlaka ya Ngeleja katika nafasi ya Uwaziri na serikalino na kuamuru maombi mazito!!!


  Wakati Ngeleja anafanya anahitaji maombi hayo January Makamba amemtaka Ngeleja ajiuzulu kutokana na kushindwa kazi
   
 8. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Sasa kunamuumini mmoja aliyekuwepo kwenye ibada hiyo alisimulia kuwa anasimulia kuwa Ngeleja amekuwa akiwamini sana Waganga wa Kienyeji na sasa Waganga Wote wameshindwa na kwamba kwenye Familia yake Wote wamezaliwa Albino isipokuwa Ngeleja Pekee!!!!!!!!!!
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Miaka hamsini ya uhuru waziri anafikiria kwa mawazo mgando namna hii. Je mzee wa kijijini aliyeishia class four atakuwa na mawazo mgando namna gani?
   
 10. g

  great vision Senior Member

  #10
  Jan 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Biblia inasema kumbuka ni wapi ulipoanguka ukatubu, bila kujua source ya tatizo ni vigumu kupata uvumbuzi, sasa kama umeme uliopita katika Kanisa la Kakobe, je wewe Mh.Ngereja huoni ni source of problems? je unaona tatizo gani kuomba msamaha kwa Bishop Kakobe,mimi ninaamini bila shaka atasikia kilio chao.na ndiyo ukristo wa kweli
  sasa kwanini unapiga chenga? na kusema ni tatizo la kisayansi halafu mara unakwenda kanisani kuhitaji maombi
   
 11. g

  great vision Senior Member

  #11
  Jan 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Biblia inasema kumbuka ni wapi ulipoanguka ukatubu, bila kujua source ya tatizo ni vigumu kupata uvumbuzi, sasa kama umeme uliopita katika Kanisa la Kakobe, hauwaki. je wewe Mh.Ngereja huoni ni source of problems? je unaona tatizo gani kuomba msamaha kwa Bishop Kakobe,mimi ninaamini bila shaka atasikia kilio chao.na ndiyo ukristo wa kweli
  sasa kwanini unapiga chenga? na kusema ni tatizo la kisayansi halafu mara unakwenda kanisani kuhitaji maombi
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,862
  Trophy Points: 280
  si amwambie Kakobe amuombee?
   
 13. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Maamuzi ya kupitisha Umeme Kwa Kakobe yalitokana na Kikao Cha Ngeleja na Rais Kikwete tar 5mach 2010 siku ya ijumaa baada ya kuwahusisha Philimon Luhanjo, David Jairo,Bashir Mlindoko, Dk Kafumu na wenzake.Hata hivyo tar7 mach Ngeleja alitoa kauli ya Rais Kikwete kuwa umeme utapita kwa Nguvu za dola na kuagiza kanda maalumu Kusimamia ambapo polis walifika na SMG huku wakibomoa mabango.Ngeleja aliwambia Waandish kuwa Rais Kikwete angezindua mradi huo Oct2010 na kwamba Kakobe ndiye aliyechelewesha kwa siku77.Sasa wahusika wote kama munavyojua wamekwishapata mapigo makubwa na wapo walioanza toba.Ngeleja hajui kuwa wenzake wameanza toba siku nyingi!Suala la Mbinguni ni la mtu binafsi ndio maana wanaokwenda India si Wabunge wote!.Ngeleja angalia Mungu aliyekufanya uwaze kumwangukia Askof wako badala ya kumufuata Kikwete ama Rostam.Ukitaka kupata toba ya kweli mfuate uliyemkosea. Angalia tatizo la umeme hukuanza wewe ameanza Richmond na wenzake.Na hao wote wa Richmond si umewaona wanahangaika na Kutafuta toba Makanisani mpaka wanakwenda Nigeria?Je wewe nizaidi ya Mabosi wako?Kumbuka hata Rostam amekuwa anakimbilia Makanisani Mpaka Tapeli Mtikila akamkatisha tamaa! je wewe ni nani hata ushindwe kutafuta toba kwa mtu uliyemkosea?Unafikiri Mungu amesahau maneno uliomlaghai Askof Kakobe mpaka media ikaandika kuwa Ngeleja amutosa Kakobe? je unaona hilo ni jema?Je umemwambia Askof wako Wa Sengerema ulaghai huu ?.Nakushauli Kimbilia Kwa Kakobe upesi kwani Mungu amekupa neema ya kuuona mwaka 2012 ili ukatubu usiwe na moyo mugumu.
   
 14. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Maamuzi ya kupitisha Umeme Kwa Kakobe yalitokana na Kikao Cha Ngeleja na Rais Kikwete tar 5mach 2010 siku ya ijumaa baada ya kuwahusisha Philimon Luhanjo, David Jairo,Bashir Mlindoko, Dk Kafumu na wenzake.Hata hivyo tar7 mach Ngeleja alitoa kauli ya Rais Kikwete kuwa umeme utapita kwa Nguvu za dola na kuagiza kanda maalumu Kusimamia ambapo polis walifika na SMG huku wakibomoa mabango.Ngeleja aliwambia Waandish kuwa Rais Kikwete angezindua mradi huo Oct2010 na kwamba Kakobe ndiye aliyechelewesha kwa siku77.Sasa wahusika wote kama munavyojua wamekwishapata mapigo makubwa na wapo walioanza toba.Ngeleja hajui kuwa wenzake wameanza toba siku nyingi!Suala la Mbinguni ni la mtu binafsi ndio maana wanaokwenda India si Wabunge wote!.Ngeleja angalia Mungu aliyekufanya uwaze kumwangukia Askof wako badala ya kumufuata Kikwete ama Rostam.Ukitaka kupata toba ya kweli mfuate uliyemkosea. Angalia tatizo la umeme hukuanza wewe ameanza Richmond na wenzake.Na hao wote wa Richmond si umewaona wanahangaika na Kutafuta toba Makanisani mpaka wanakwenda Nigeria?Je wewe nizaidi ya Mabosi wako?Kumbuka hata Rostam amekuwa anakimbilia Makanisani Mpaka Tapeli Mtikila akamkatisha tamaa! je wewe ni nani hata ushindwe kutafuta toba kwa mtu uliyemkosea?Unafikiri Mungu amesahau maneno uliomlaghai Askof Kakobe mpaka media ikaandika kuwa Ngeleja amutosa Kakobe? je unaona hilo ni jema?Je umemwambia Askof wako Wa Sengerema ulaghai huu ?.Nakushauli Kimbilia Kwa Kakobe upesi kwani Mungu amekupa neema ya kuuona mwaka 2012 ili ukatubu usiwe na moyo mugumu.
   
 15. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Kanisa la African Inland (AICT) Jimbo la Geita ( anakosali Mh Ngeleja) limewataka Waumini wake kuutumia Mwaka mpya kuondokana na makundi yaliyosababisha mgawanyiko miongoni mwao wakati wa Uchaguzi mwaka2010.

  Mch.Kileo Marobo anayeongoza kanisa hilo alitoa kauli hiyo mbele ya Askof Mussa magwesela wakati wa misa ya kuukaribisha mwaka mpya.

  Alisema Uchaguzi mkuu uliopita Waumini wengi wa kanisa hilo waligawanyika ikiwa ni pamoja na kupandikiziana chuki miongoni mwetu na kusababisha malumbano ndani ya kanisa, kutokana na itikadi za Kisiasa hasa wakati wa kura za Maoni ndani ya CCM ambapo Mh Ngeleja alipita bila Kupingwa!!

  "Ndugu Uchaguzi mkuu uliopita wa 2010 ,ambao ulikuwa wa urais na wabunge ulituletea majeraha makubwa ya chuki zilizo pandikizwa na Wagombea wa nafasi hizo kwa maslahi binafsi." Hivyo ninawaomba turudi kundindini upya tujenge nchi yetu.'

  Mhe Ngeleja naye alipata nafasi katika Ibada hiyo ambapo aliwaomba waumini na wachungaji wamuombee ili matatizo ya umeme yaishe nchini.

  Aluisema hivi sasa umeme hauwaki hivyo naomba maombi Mungu aingilie Kati.

  Source : Majira pg18 leo.
   
Loading...