Mh. Ndugai, Refa anayeweza kushushwa daraja?

Hon.MP

Senior Member
Jul 15, 2012
153
86
Moja ya kazi kubwa ya Spika / Naibu Spika / Mwenyekiti Bungeni au kamati ya Bunge ni kuhakikisha kuwa Wabunge wanajikita katika mjadala ulioko mezani na pia muhimu sana kama ilivyo kwa mwamuzi ni kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa wachezaji wote yaani wabunge kupewa nafasi stahiki sawia bila kuvunja kanuni husika za majadiliano Bungeni.

Baada ya Mh. Lukuvi kuruhusiwa kuanika ‘uwongo’ wa Mh. Mch. Msigwa hadharani bungeni juu ya Kiongozi wa CCM anayesemekana kuhusishwa na ujambazi / wizi mkubwa wa nyara za Serikali kwa muda wa kutosha na vielelezo; je, haikuwa halali pia Mh. Job Ndugai (Naibu Spika) kumpa nafasi Mch. Msigwa ama aendelee kutetea ‘ukweli’ aliokuwa ameuwasilisha kwa uthibitisho au kuondoa kauli yake ya awali na kuomba msamaha katika jukwaa hilo hilo lililotumika kumwaibisha / kumuumbua?

Kama Naibu Spika hakutaka hayo yajadadiliwe Bungeni, kwa nini asingemkatiza Mh. Lukuvi na kumwomba ayaweke maelezo yake kimaandishi ili baadaye yapelekwe kwenye Kamati ya maadili ya Bunge?

Kila wakati tusisitiza kuwa, hakuna haja ya kuminya haki ili uweze kumwaibisha mtu anayeongopa lakini ni kweli pia kwamba, kamwe matumizi ya nguvu ya kiti au vifungu vya miongozo haviwezi kutumika kuzuia jambo lolote kujulikana na sisi Wananchi kama ni la kweli au hata kama lina chembe ndogo ya ukweli.
Ndugai, wakati unapumzika nyumbani, tafakari ulichokifanya kabla hujashushwa daraja na wananchi.

Ulichokifanya leo Bungeni ni sawa na Refa aliyeingilia pambano akamkamata mikono mpiganaji mmoja na kumvuta huku akiruhusu mpinzani wake akiendelea kumrushia masumbwi mazito aliyevutwa toka kwenye pambano. Na mwishowe Refa bila hata kutoa onyo wala karipio kwa aliyeendeleza shambulizi au kumpunguzia point, anamalizia kwa kusema, si kazi yangu kusema chochote, Majaji (kamati ya Maadili) wanajumlisha na kuona nani ameshinda kwa point nyingi.

Hii ni karne nyingine!
 
Aiseee baba yangu mi nilichojifunza kwenye nchi maigizo hakuna haki ukisikia jambo linapelekwa kwenye kamati ya maadili ujuwe magamba wamekosea hivyo hawataki wananchi wajue makosa yao

aiseeee mama shirima niongeze mbege nyingine yeeeeeeuuuuuiiiii
 
Ukweli ni kwamba, hawa jamaa wote wanajulikana misheni yao ya kuegemea upande wa serikali ya chama chao, MAKINDA, NDUGAI, MABUMBA, atleast MHAGAMA na ZUNGU kidogo huwa wana-play fare kiasi chake. Cha kufurahisha ni kwamba wananchi wameshaisoma vizuri sana mood ya bunge letu. baadhi ya wananchi ambao katika hali ya kawaida usingewatarajia, utawakuta wanasema kabisa kwamba kiti hakitendi haki kwa wapinzani. ukiona hivyo ujue kuna kiwango fulani cha jamii kimeshaushitukia mchezo. na hii ni CREDIT kwa wapinzani hasa CDM, kwani inaonesha kabisa wamekubalika kwa kiwango kikubwa na wananchi. NA KUMBUKA MWISHO WA SIKU HAKIMU WA DEMOKRASIA NI MWANANCHI.
 
Kwani ilikuwa ni session ya asubuhi, au mchana? inawezekana alikuwa amepitia pembeni kidogo kulamba au kuvuta ile kitu.
 
Back
Top Bottom