mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,480
- 6,833
Mh Waziri hustahili kuendelea kubeba dhamana hiyo uliyokabidhiwa. Matukio haya siku za karibuni yamenikumbusha matukio mawili ya kuuawa watanzania wenzetu zaidi ya 50 huko Kagera mwezi wa tisa mwaka jana.
Mkuu kwa makusudi uliamua kufumbia macho au niite kupuuzia kuuawa kwa watanzaia hao. Nakumbuka ulienda Kagera na baada ya kuthibitisha kutokea kwa matukio hayo uliahidi kulifatilia na kulitolea ufafanuzi kama serikali.
Inasikitisha watanzania wale 50 walipotea kama kuku na wewe uliamua kulipotezea mpkaleo hii. Najua ulikaa kimywa kwa madai ya kuogopa kibarua kuingia mchanga (silisemi ila wewe unajua).
Tunajua una malengo makubwa na safari ndefu ya kisiasa katika nchi hii ndio maana hata sasa huzungumzii lolote kuhusu yanayowatokea wananchi kwa madai hutaki kuonekana uko upande fulani ili uendelee kuaminika,ila nikwambie tu hauminiki tena kwake na wananchi hatukuamini tena.
Umetaka yote umekosa yote, hustahili madaraka makubwa zaidi katika Taifa hili kwa sababu huna uchungu na sisi raia bali una uchungu na political career yako.
Mwisho Mkuu ni kweli huwezi kufanya kazi za walio chini yako, ila wewe ndio kauli ya serikali. Wananchi wakipatwa na sitofahamu au taharuki ni wajibu wako kutoa kauli kwa niaba ya serikali yao.
Serikali haijatolea ufafanuzi mpaka leo vifo vya Watanzania karibu na mpaka wa nchi ya Rwanda?