Mh. Msomi, MB Tundu Lissu, anajua kujenga hoja WanaJamvi! Soma alivyowaumbua Mafisadi wa CCM Bungeni

ihs

Member
Jul 24, 2012
93
68
[h=3]MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA[/h]
MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU (MB.)
KUHUSU

MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KWA MWAKA 2014/2015
(Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)

UTANGULIZI​

Mheshimiwa Spika,
Ofisi ya Waziri wa Katiba na Sheria imeanzishwa kwa mujibu wa kipengele cha 12 cha Nyongeza ya Waraka wa Rais uliochapishwa kama Tangazo la Serikali Na. 494 la tarehe 17 Desemba 2010. Majukumu ya Ofisi hii yameainishwa katika Tangazo la Ukasimishaji wa Majukumu ya Kiuwaziri la mwaka 2010 (The Ministers [Assignment of Ministerial Functions] Notice, 2010) lililochapishwa katika Gazeti la Serikali kama Tangazo la Serikali Na. 494A la tarehe 17 Desemba 2010. Kwa mujibu wa Nyongeza ya Pili ya Tangazo hilo, pamoja na mengine, Ofisi ya Waziri wa Katiba na Sheria imekasimiwa majukumu ya masuala ya kikatiba, uendeshaji na utoaji wa haki, uendeshaji mashtaka na haki za binadamu.
Mheshimiwa Spika,
Majukumu haya ni mazito katika hali ya kawaida, kwani mfumo wa kikatiba, haki za binadamu na utoaji haki katika nchi yenye kufuata mfumo wa kidemokrasia ndiyo roho ya mfumo mzima wa utawala. Mfumo wa kikatiba na wa utoaji haki ndio unaotofautisha dola iliyoparaganyika (a failed state) na dola inayoongozwa kikatiba (a constitutional state) na utawala wa sheria (rule of law). Majukumu haya ni mazito zaidi katika nchi ambayo, kama ilivyo nchi yetu, inatengeneza Katiba Mpya. Hapa, vile vile, mfumo unaotumika kutengeneza Katiba Mpya ndiyo utakaotofautisha nchi hiyo kuwa a failed state, au kuwa nchi yenye mfumo imara wa kikatiba na wa kisiasa. Kwa sababu hiyo, kwa vyovyote vile, majukumu ya Wizara ya Katiba na Sheria ni mazito na yenye umuhimu mkubwa.
BUNGE MAALUM NA HARUFU YA UFISADI​
Mheshimiwa Spika,
Vyombo vya habari mbali mbali hapa nchini vimemnukuu Waziri wa Fedha Mh. Saada Salum Mkuya akisema kwamba, hadi kuahirishwa kwake, Bunge Maalum limetumia zaidi ya Shilingi bilioni 27. Kama kauli ya Waziri wa Fedha ni sahihi, kiasi hiki cha fedha kitakuwa kikubwa kuliko fedha za matumizi ya kawaida ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Divisheni ya Uendeshaji Mashtaka na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa ujumla wao kwa mwaka unaoisha wa fedha. Hiki sio kiasi kidogo cha fedha katika nchi kama yetu ambayo shughuli mbali mbali za huduma za jamii zimekwama kwa kukosa fedha.
Mheshimiwa Spika,
Mwaka jana wakati Bunge lako tukufu linajadili makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2013/2014, Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala iliagiza kwamba bajeti ya Bunge Maalum “… iletwe Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa.” Kamati ilitoa agizo hilo kwa sababu wakati Wizara ilikuwa imewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, yaani Fungu 08, hakukuwa na Fungu lolote linalohusu Bunge Maalum. Hii ni licha ya ukweli kwamba hadi kufikia mwaka jana, tayari ilikuwa inajulikana kwamba kutakuwa na Bunge Maalum, kwa sababu vifungu husika vya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba vilikwishapitishwa na Bunge lako tukufu.
Mheshimiwa Spika,
Agizo la Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala lilipuuzwa mwaka jana kwani Serikali hii sikivu ya CCM haikuleta makadirio ya mapato na matumizi ya Bunge Maalum kwa ajili ya kujadiliwa na kuidhinishwa na Bunge lako tukufu. Na hata mwaka huu agizo hilo limepuuzwa kwani hakuna makadirio ya mapato na matumizi ya Bunge Maalum ambayo yameletwa kwa ajili ya kujadiliwa na kuidhinishwa na Bunge lako tukufu.
Ili kuhalalisha vitendo vyake vya kupuuza agizo la Bunge lako tukufu, Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, alidai mbele ya Kamati kwamba “… masuala yote ya Bunge la Katiba yapo chini ya Bunge Maalum la Katiba ambapo fedha kwa ajili ya Bunge hili zinatolewa na Mfuko Mkuu wa Hazina.” Kwa jibu hili, Waziri alitaka kuiaminisha Kamati kwamba hakukuwa na haja ya fedha za Bunge Maalum kujadiliwa na kuidhinishwa na Bunge lako tukufu kwa sababu tu fedha hizo zilikuwa zinatoka kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.
Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, baada ya kuonyeshwa kwamba fedha zinazolipwa kutoka kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina hazina budi kuidhinishwa na sheria iliyotungwa Bunge na matumizi yake kuidhinishwa na Sheria ya Matumizi ya Serikali, sasa Waziri amebadili kauli na kudai kwamba fedha za matumizi ya Bunge Maalum ziliidhinishwa na Bunge lako tukufu!
Katika Majibu yake ya Hoja za Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Wakati wa Kupitia Makadirio ya Wizara kwa mwaka wa Fedha 2014/2015, Mheshimiwa Waziri amesema yafuatayo: “Bajeti ya Bunge Maalum ya shilingi bilioni 24.4 ilipitishwa na Bunge katika mwaka wa fedha 2013/2014 kupitia Fungu 21 – Hazina kwenye kifungu cha ‘Special Expenditure.’ Serikali ilifanya hivyo kwa kutambua kwamba Bunge Maalum lingeanza kazi zake katika mwaka huo wa fedha. Wakati huo mahitaji halisi ya uendeshaji wa Bunge hilo yalikuwa hayafahamiki.”
Waziri ameongeza kusema kwamba “kwa kutumia uzoefu uliopatikana katika uendeshaji wa Bunge hilo, Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 20.0 kwenye Fungu 21 – Hazina kwenye kifungu cha ‘Special Expenditure’ katika mwaka wa fedha 2014/2015 ili kukamilisha kazi zilizosalia.”
Mheshimiwa Spika,
Kauli za Waziri wa Katiba na Sheria juu ya masuala yote yanayohusu bajeti ya Bunge Maalum hazina ukweli wowote. Kwanza, kuhusu kiasi cha fedha kilichokwishatumika kwa ajili ya Bunge Maalum. Kauli ya Waziri kwamba kiasi hicho ni shilingi bilioni 24.4 inapingana moja kwa moja na kauli iliyotolewa na Waziri wa Fedha ndani ya Bunge Maalum.
Kwa mujibu wa Taarifa Rasmi (Hansard) ya Majadiliano ya Bunge Maalum ya Kikao cha Ishirini na Tisa cha tarehe 24 Aprili, 2014, Mheshimiwa Saada Mkuya Salum, alisema yafuatayo kuhusu matumizi ya Bunge Maalum: “Mheshimiwa Mwenyekiti, inasikitisha kwamba hatutumii fursa hii, nasikitika tumechukua fedha, yaani kodi ya wananchi ambayo kila siku wanalia na wameweza ku-sacrifice tunakwenda kwenye twenty seven billions kwa ajili ya session hii, tumeweza ku-sacrifice kupeleka umeme kwa wananchi, hususan vijijini.”
Mheshimiwa Spika,
Kiasi kilichotajwa na Waziri wa Fedha kinalingana na kiasi kilichotajwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Utaribu na Bunge, Mheshimiwa William Lukuvi, aliyeiambia Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala kwamba hadi linaahirishwa tarehe 25 Aprili mwaka huu, Bunge Maalum lilikwishatumia takriban shilingi bilioni 27.
Mheshimiwa Spika,
Bunge lako tukufu linahitaji majibu ya kuridhisha kuhusu mkanganyiko huu katika kauli za Waziri wa Katiba na Sheria na Mawaziri wenzake wa Fedha na Sera, Uratibu na Bunge. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali hii ya CCM ilieleze Bunge lako tukufu ni kauli ya Waziri yupi kati ya hawa watatu ndiyo iaminiwe na kuchukuliwa kuwa ndiyo kauli sahihi na Bunge lako tukufu.
Aidha, kama itajulikana kwamba mmojawapo kati ya mawaziri hawa watatu ametoa taarifa za uongo kwa Kamati ya Bunge lako tukufu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka mamlaka ya uteuzi wao, yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano, awawajibishe kwa kuwafukuza kazi. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba Waziri anayedanganya Bunge lako tukufu au Kamati zake sio tu analidharau Bunge, bali pia anaidharau mamlaka ya uteuzi wake, yaani Rais. Vinginevyo Bunge lako tukufu liambiwe kwamba Waziri huyo ametumwa na Rais kuja kudanganya Bunge.
Mheshimiwa Spika,
Uongo wa pili wa kauli ya Waziri wa Katiba na Sheria unahusu madai yake kwamba bajeti ya Bunge Maalum iko kwenye Fungu 21 – Hazina. Uthibitisho wa uongo huu uko kwenye Kitabu cha II cha Makadirio ya Matumizi ya Umma ya Huduma za Mfuko Mkuu kwa mwaka wa fedha 2013/2014 kilichowasilishwa Bungeni mwaka jana; na Kitabu hicho hicho kilichowasilishwa Bungeni mwezi huu kwa ajili ya mwaka wa fedha 2014/2015. Katika Vitabu vyote viwili hakuna kifungu chochote kinachoitwa ‘Special Expenditure’ au kasma yoyote inayohusu Bunge Maalum.
Aidha, hakuna kifungu chochote chenye makadirio ya matumizi ya shilingi bilioni 24.4 kwa ajili ya Bunge Maalum au kwa ajili nyingine yoyote katika Kitabu cha mwaka 2013/2014; na wala hakuna makadirio ya matumizi ya shilingi bilioni 20.0 kwa ajili ya matumizi ya Bunge Maalum katika Kitabu cha mwaka 2014/2015. Na hata kwenye Vitabu vya Makadirio ya Matumizi ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2013/2014 na mwaka wa fedha 2014/2015, hakuna kifungu chochote kinachoitwa ‘Special Expenditure’ au chenye kiasi cha fedha kilichotajwa na Waziri wa Katiba na Sheria.
Mheshimiwa Spika,
Kama hakuna vifungu vyovyote vya ‘Special Expenditure’ kwa ajili ya Bunge Maalum, na kama hakuna kiasi chochote kilichoonyeshwa kwenye Vitabu vya bajeti, maana yake ni kwamba Bunge lako tukufu halijaidhinisha bajeti yoyote kwa ajili ya Bunge Maalum. Kwa kifupi, Waziri wa Katiba na Sheria amelidanganya Bunge lako tukufu, na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni itaona ajabu sana endapo Bunge lako tukufu litaamua, licha ya ushahidi wote huu, kufunika kombe ili wanaharamu wapite!
Mheshimiwa Spika,
Katika Maoni yake juu ya hotuba ya Waziri Mkuu Kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2014/2015, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman A. Mbowe aliliambia Bunge lako tukufu kwamba: “Fedha zote zilizotumika kwa ajili ya gharama mbali mbali za Bunge Maalum hazikuidhinishwa na Bunge lako tukufu. Ukweli ni kwamba hadi sasa Bunge lako tukufu halijui bajeti yote ya Bunge Maalum, halijui fedha kiasi gani zimetumika kwa ajili ya matengenezo mbali mbali ya miundombinu ya Bunge hili, au kwa ajili ya posho, mishahara na stahili mbali mbali za wajumbe na watumishi wa Bunge Maalum hadi lilipoahirishwa tarehe 25 Aprili, 2014. Aidha, Bunge lako tukufu halina ufahamu wowote juu ya gharama za Bunge Maalum pale litakaporudi tarehe 5 Agosti, 2014, kuendelea kujadili Rasimu ya Katiba Mpya.”
Katika hali hiyo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alitaka maswali yafuatayo yapatiwe majibu:
(i) Je, bajeti ya matumizi ya Bunge Maalum ni kiasi gani na kwa ajili ya matumizi gani?
(ii) Je, ni kiasi gani cha fedha hizo kimeshatumika hadi sasa na kwa ajili ya matumizi gani?
(iii) Je, ni nani aliyejadili na kupitisha bajeti hiyo?
(iv) Je, ni Sheria gani iliyotungwa na Bunge lipi iliyoidhinisha matumizi haya ya fedha za umma?
(v) Je, ni lini na kwa waraka gani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliidhinisha matumizi haya?
Mheshimiwa Spika,
Maswali haya hayajapatiwa majibu yoyote. Badala yake, Waziri wa Katiba na Sheria amelipa Bunge lako tukufu sababu za kuuliza maswali mengine yafuatayo:
(a) Je, ni ukurasa upi kati ya kurasa za 55-60 zenye makadirio ya Fungu 21 – Hazina kwenye Kitabu cha II ambapo kuna kifungu cha ‘Special Expenditure’ chenye makadirio ya matumizi ya shilingi bilioni 24.4 kwa ajili ya Bunge Maalum kwa mwaka wa fedha 2013/2014?
(b) Je, ni ukurasa upi kati ya kurasa za 68-73 zenye makadirio ya Fungu 21 – Hazina kwenye Kitabu cha II ambapo kuna kifungu cha ‘Special Expenditure chenye makadirio ya matumizi ya shilingi bilioni 20.0 kwa ajili ya Bunge Maalum kwa mwaka wa fedha 2014/2015?
(c) Je, kati ya kauli yake kwamba hadi linaahirishwa Bunge Maalum limekwishatumia shilingi bilioni 24.4, na kauli ya Waziri wa Fedha kwamba Bunge hilo limekwishatumia shilingi bilioni 27, ipi ndiyo kauli ya kweli?
(d) Na mwisho, kama itajulikana kwamba kauli yake kuhusu masuala yanayohusu bajeti ya Bunge Maalum ni ya uongo yuko tayari kulinda heshima yake iliyobaki kwa kujiuzulu au atasubiri mamlaka yake ya uteuzi imwajibishe kwa kumfukuza kazi kwa kulidanganya Bunge?

Source: Bunge la Budget, JMT
 
Tundu lisu hakika unastahili sifa hasa kwa kuitwa mpambanaji pekee unayeweza kulikomboa taifa hili kutoka midomoni mwa mafisadi
 
Pesa imesundwa pembeni kidogo ikaenda kwenye posho ya wajumbe ila wakasahau kubalansisha vitabu! Mwizi hawezi kuiba asiache trace ya kumkamata!
 
Wizi ni kazi ngumu sana! Kuchukua hela ni rahisi sana ila kuhakikisha hujaacha trace ndo inakuwa haiwezekani! Unaona wanavyokanyagana!
 
Ipi sasa budget kivuli ambayo ingekuwa ndio njia mbadala kupayuka tu hakuwezi leta tofauti yeyote.
 
Ccm wanatafta hela za kampeni kwa mguvu.wanaiba kila panapoibika.yaan ni shida.bt za mwizi harobaini na ndo inatimia maana kila wanapotia kono wanaibuliwa.
 
TL is a real great thinker.Huyu hauwezi kumlinganisha hata na wanasheria wa vyeti kama Mwakyembe.Huyu ni miongoni mwa wanasheria wachache akiwemo mzee warioba ambao ni tunu kwa taifa letu.Good MWANA wa TANZANIA bwana TUNDU A. LISU.
 
Back
Top Bottom