Nyamemba
JF-Expert Member
- Nov 3, 2011
- 845
- 447
Mbunge wa Kibamba John John Mnyika amewatelekeza wananchi wake, kwa muda mrefu sasa Mnyika amekuwa haonekani jimboni kwake kusikiliza kero za wananchi wake na badala yake wananchi tunajutia kumchagua kuwa mwakilishi wetu. Miongoni mwa kero kadhaa zinazowakabili wananchi wake ni hii barabara ya kutoka Kimara mwisho - Michungwani-King'ongo-Njiapanda ya Goba - Kwa Komba - Matosa yenye takribani km 4. Barabara hii ni mojawapo ya barabara mbovu kuwahi kutokea nchi hii na mbunge amekuwa akikwepa kuja huku kila tunapomuita ili aje kusikiliza kero zetu. Kabla ya bunge hili la bajeti kuanza tulikwenda ofisini kwake hatukumkuta na tukaacha ujumbe lakini haukushughulikiwa, hata anapopigiwa simu yake ya mkononi anapopokea akikuuliza unakaa mitaa gani ukimtajia mitaa hii anakata simu na kulock namba yako. Kupitia jukwaa hili tunaomba msaada either serikalini itusamehe kwa kuchagua vibaya au kwa uongozi wa Chadema kumshinikiza mbunge huyu aje huku kujionea hali halisi ili aweze kuitatua. Narudia kero zetu ni nyingi ila hii ni zaidi ya kero ndo maana leo nimekuja na hii kwa kuanzia. Chonde Chonde uongozi wa jf msiondoe uzi huu kama ilivyo kawaida yenu mkiona thread ambazo zinawalenga viongozi wa Chadema.