Jamani wa Tz mmemsikia waziri wa fedha Mgimwa kuwa noti za aina mbili mpya na za zamani zitaendelea kutumika hadi hapo wananchi watakapotoa maoni yao kuwa wanataka zitumike noti za aina gani.
Je, ni kweli walishawahi kupita kwa wananchi hata siku moja na kuuliza ni noti za namna gani wanataka zitumike?
Kwani hata leo wakipita jibu liko wazi kuwa tunataka za zamani na siyo hizi mpya kwani mimi binafsi sioni kama kweli ni mpya kwani ndo zinaonekana za zamani kuliko zilizokuwepo hapo awali.
Hivyo basi Mgimwa sema ukweli wako tu kuwa pengine mkakati wenu haukufanikiwa katika hili na kwa njia hiyo taifa limepoteza mabilioni ya shilingi kuchapisha fedha ambayo hatujafaidika nayo hata kidogo.
Maoni yangu je, kabla ya kuzichapisha hizo fedha hawakujua ya kuwa zina ubora wa chini? na kama walijua je, waliotufikisha hapa tulipo watachukuliwa hatua gani za kisheria?