Mh. Masha hii imekaaje... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Masha hii imekaaje...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shadow, Apr 14, 2009.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Unless mwandishi awe amekosea ila kama ndiyo reasoning ya polisi wetu hiko hivi mbona tumekula hasara! mwizi kashikwa na ngozi unasema ana tabia nzuri? Mh. Hebu tuambie manake najua unapokea briefing kutoka kwa walio chini yako kila siku.


  Polisi akamatwa na risasi 35 mwenzake wadai ni mtu mwema
  Na Mwandishi Wetu


  ASKARI polisi mmoja wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ameiba risasi 35 za bunduki na kuzihifadhi katika duka moja la dawa baridi la Alpho lililopo Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

  Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana, zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 3, mwaka huu katika duka hilo la dawa na kufahamisha kwamba, askari huyo alikwenda katika duka hilo akiwa na mzigo huo na kuomba wamhifadhie hadi saa 2:00 usiku atakapokwenda kuuchukua.

  Mmiliki wa duka hilo, Norbert Marealle aliliambia gazeti hili jana kwamba, askari huyo alifika dukani kwake na kumkuta mfanyakazi wake mgeni akamuomba amhifadhie mzigo huo hadi saa 2:00 usiku atakapokwenda kuuchukua.

  Alidai kuwa askari huyo alimweleza mfanyakazi huyo mgeni kwamba, amtaarifu mwenzake anayeitwa Mariam Abdul ambaye hakuwepo wakati huo.

  Marealle alidai kuwa baada ya Mariamu kurejea aliambiwa juu ya mzigo huo ambao ulikuwa umefungwa ndani ya mifuko miwili ya Rambo na kwamba alipouona alishituka na kuamua kuufungua ili waone kilichomo.

  Alidai kuwa walipoufungua ndani walikuta kasha mbili ambazo walizifungua na kukuta zimesheheni risasi, wakaamua kumpigia simu (Marealle) na kwamba; kwa vile alikuwa mbali na eneo hilo aliwaambia wakatoe taarifa haraka katika Kituo cha Polisi Oysterbay.

  “Walienda kule na kupewa askari kanzu sita ambao walienda kuweka doria ili wamtie mbaroni mhusika lakini siku hiyo, hakutokea,” alisema Marealle.

  Alindelea kusimulia akisema: “Kesho yake askari hao waliendelea kuweka doria lakini hakutokea na wakafanya hivyo kwa siku mbili na siku ya tatu (Aprili 5) askari doria wakiwa hawapo, askari huyo alifika kuuchukua.

  “Ikabidi mmoja wa wauzaji wangu aingie chumbani na kuwapigia simu polisi na walipofika wakamtia mbaroni. Polisi walikiri kuwa wanamfahamu mtuhumiwa huyo na kwamba ni askari mwenzao kisha walimchukua na kuondoka naye kwenda kituoni,” alidai Marealle.

  Alidai kuwa siku hiyo usiku, mkewe alikwenda kituo cha polisi Oysterbay na kutoa maelezo na kuhifadhiwa kwa kumbukumbu namba OB/RB/6137/2009.

  Alidai kuwa baadaye waliarifiwa na polisi kuwa asiwe na wasiwasi kwa sababu askari aliyebambwa hana historia mbaya ya kikazi na hazikuchukuliwa hatua zozote.

  Hata hivyo, Marealle alisema alipata wasiwasi juu ya maelezo hayo ikizingatiwa kuwa suala la risasi ni nyeti na si jambo la kawaida kwa polisi kwenda kuzihifadhi kwa raia, hivyo aliamua kutoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ambaye alimpigia simu mkuu wa kituo hicho cha polisi ambaye alimjibu kuwa hana taarifa.

  Baadaye mkuu huyo wa kituo akaomba kuonana na mmiliki wa duka hilo la madawa ambaye alipofika alimwambia ampe maelezo ambayo aliyaandika.

  Mwananchi lilipowasiliana na Kamanda Kova, alikiri kupewa taarifa za tukio hilo na mmoja wa wanafamilia ya Marealle, lakini akamtaka awasiliane na Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Kindondoni.

  “Ni kweli kuna mama mmoja aliniambia juu ya tukio la namna hiyo nikamuelekeza awasiliane na RPC. Sasa nashangaa hadi sasa hajaenda kumuona,” alisema Kova na kusisitiza kuwa atalifanyia uchunguzi suala hilo na kulitolea taarifa.

  Gazeti hili lilipowasiliana na RPC wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye kutaka ufafanuzi wa suala hilo, akajibu kuwa ofisi yake haina taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo.

  “Sina taarifa hiyo,” alisema Kalunguyeye ambaye huwa hapendi kuzungumza na waandishi wa habari. Hata katika tukio la hivi karibuni la kuuawa kwa dereva teksi, kwa kupigwa risasi na polisi maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam, alipoulizwa na gezeti hili alijibu kuwa hana taarifa ya tukio hilo.

  CHANZO: Gazeti la Mwananchi
   
 2. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2009
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Inawezekana hii ikawa ni njia mojawapo wanayotumia kujiongezea kipato
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hapo kwa mtazamo wao (polisi), mwenye tatizo ni huyo raia mwema (mwenye duka la dawa) ambaye anafuatilia mambo yasiyo muhusu. Hapo ajiandae kubambikizwa kesi au hata kufanyiwa hujuma za ajabu ajabu. Hata Kova hastuki kwa tukia hilo kuonesha kuwa ni jambo la kawaida tu. Wote wanaona linakuzwa tu! Kazi ipo kweli kweli!
   
 4. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sasa kama wamemkuta nazo boss wao hizo risasi watampeleka kwa nani tena!!!!!! Ndiyo mwisho wa kesi kwa Tz!!!!!
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Dark City: Iko kazi kweli kweli hasa mtu kama Masha ndiyo mkuu wa kitengo hicho cha mapolisi. yeye Masha alikuwa tayari kumbambikizia mambo Reginald Mengi -- sembuse wale wa chini yake?
   
 6. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pathetic! Huyo ashikiwe bango. Polisi kama huyo ni hatari kwa usalama wa raia na mali.

  Hizo risasi bahati mbaya wakaweka sehemu panapo pata joto, kwa mfano nyuma ya firiji, kuna uwezekano wa kulipuka na kujeruhi.

  Vilevile amekiuka sheria kwa kutoka na risasi kituoni(sina uhakika kama alikuwa na gwanda)

  Polisi kama huyo yawezekana akawa na uhusiano na majambazi-hakuna cha uzuri wake-ni mhalifu.!

  Kuhusu Mh. Masha na hayo yaliyofanyika...nafikiri huu ni uchinjaji wa kisiasa, sidhani kama hii subject title hapo juu inaendana na Habari yenyewe!!!
   
 7. e

  eddy JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,374
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya mwandishi hakusema alipoenda ofisini kwa masha mwema RO alijibiwa nini! sioni masha anaingiaje kwenye hii mada! jeshi la polisi linautaratibu wake ikiwemo mahakama ya kijeshi, sasa huyo mama alikuwa anatafuta nini kwa kova? huyo askari hakuwa mpumbavu lazima kunakauhusiano na mmiliki wa duka.
   
 8. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Nashukuru kwa sababu kidogo umetaka kiungia kwenye akili zao(sina uhakika kama wewe nawe ni Polisi na ndiyo mtazamo wenu). Mtazamo huo ni butu. tatizo la kuwa na majambazi toka Polisi bado lipo, halijaisha. huwezi ukasema huyu ni mtu mwema wakati anachukua risasi hizo zote. Wakubali tu kwamba wanataka kulindana. Na hapo kuna mtandao mpana; mtunza risasi, mtoa risasi, mchukua risasi na mtu aliyekusudiwa kupelekewa ni nani.

  Utakumbuka mwaka jana miezi ya mwishoni (ikiripotiwa na Radio WAPO, kipindi cha YALIYOTOKEA) ulitokea wizi Kigamboni-Dar. Mfanyabiashara aliyeibiwa alisema waliwaona hao majambazi wamevaa sare za Polisi. Wakatiwanafanya uharifu wao, wananchi walipiga simu polisi, Kituo cha Kigamboni lakini hawakufika sehemu ya tukio. Siku iliyofuata walifika, baada yakupata maelezo Mkuu wa kituo cha Polisi Kigamboni akawaambia wasiseme wamevalia mavazi ya jeshi la Polisi bali ya jeshi la Wananchi, ukazuka mgogoro mwingine wa kupindisha ukweli unaofanywa na Mkuu wa kituo cha Polisi.

  Hebu angalia yanapotokea matukio ya ujambazi yakahusisha matumizi ya nguo za za jeshi la Wananchi jinsi wakuu wa polisi wa mikoa au kanda maalumu wanavyoshabikia kwa jinsi wanavyowasilisha taarifa kwa jamii. Tena picha zake huwa kurasa za mbele.

  Huyo ni jambazi, Kova akitetea naye yupo katika huo mtandao.
   
 9. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  The whole story smells fishy to me,ilikuwaje askari aende kwenye hilo duka in particular? na kwa nini alitaja jina la huyo binti,ina maana wanafahamiana au kama ni deal ina maana huwa wanafanya pamoja?where does that leave the owner of the shop? au tuseme mmiliki wa duka alitoa maagizo vijana waende polisi baada ya kugundua mfanyakazi asiyehusika kajua kilichokuwa ndani ya mfuko? questions,questions,questions.........
   
 10. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Yaani jamani hii nchi yetu inaelekea wapi?? Yaani askari akafiche risasi za moto dukani kwa raia halafu useme eti hajawahi hana historia ya uhalifu. Nani kakwambia jambazi ana historia ya uhalifu kabla hajakamatwa?? Kwa mara ya kwanza jambazi akikamatwa hata kama ameshafanya matukio 100 ya ujambazi bila kukamatwa, then siku anakamatwa ndipo historia yake ya ujambazi inaanza!!! Kwanza watueleze hizo risasi zilikuwa zinapelekwa wapi, na aje kuzichukua siku ya tatu!!!!! Wasitupe kichefuchefu hapa.

  Ila tu ndugu Marealle, unatakiwa sasa uishi kwa machale makubwa na ya hali ya juu sana. Hawa jamaa watakuwashia moto mkubwa sana. Watakuandama kama si kifo basi ni kwa kesi kubwa sana ya jinai, mpaka uje prove innocent utakuwa umekwisha kabisa.

  Hakikisha una vibali vyote vya dukani (ikiwemo cha pharmacy, tra, tfda. etc). Haki ya nani,, Tanzania mambo kiholela tu. What is the implication??? Does it mean that our viongozi watukufu ni holela?? No, not at all, naamini tuna viongozi imara!!! If that is the case, tunataka haki itendeke.

  Masha naye vipi?? Au anaugulia mapigo ya media??? The guy is a sleeping giant?!!! Wizara ya mambo ya ndani ya nchi is too heavy to him!!!!
   
 11. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  LOL. Acheni umbea. LOL
   
 12. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #12
  Apr 14, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inamaanisha orodha ya mapolisi wahalifu ambao wako kwenye kazi za kipolisi wanayo na huyu polisi hayumo,sio? makubwa
   
 13. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ahh Masha atakuwa anasubiri ofisi yake iletewe maombi rasmi ya kuchunguza hili tukio..!!
   
 14. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  hiyo ni network ndefu tu, kwa sababu swali la kujiuliza aliwezaje kuchukua hizo risasi kutoka amari, alisaini vipi, au m2 anayetunza store alimkubalia vipi?
  tunakuwa tunajiuliza hawa majambazi wanapataga silaha wapi lakini inaonyesha kabisa kwamba hii ndio njia wanayotumia, na kwa mkuu kusema huyo ni askari mzuri si ajabu kwamba hao wakubwa ni kama wakina Zombe ambao wanakuwa na vijana wao wa kazi, wa aidha kufanya wao wenyewe mauaji au kugawa silaha kwa majambazi
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu Mnyamahodzo, sijaona wapi maoni yangu yanatofautiana na yako. Tofauti ni uandishi mkuu! Kwa hiyo siona kama ulikuwa na haja ya kunishambulia. Hata kama mimi ni polisi lakini maoni yangu yako wazi kwamba hapo walikuwa wanajaribu kuficha ukweli na kwamba kuna uwezekano wa kumwandama huyo raia. Kama sikueleweka ungejaribu kuniuliza badala ya kuamua kunipa kazi ambayo sijawahi kuiwazia. Hata hivyo sina tatizo na maoni yako kwa sababu ndiyo raha ya uhuru wa maoni.
   
Loading...