tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,863
- 3,851
Mh. Makonda unatumia nguvu nyingi kuliko akili.
Kuna vyanzo vingi tu vinavyoweza kutoa takwimu ya kile unachokitaka.
Kama ni idadi ya watu.
Nenda Ofisi ya Takwimu watakupatia Idadi nzima ya watu. Haujapita muda tangu zoezi la kuhesabu watu kufanyika hivyo data hazijabadilika sana.
Kama ni kujua kazi za wenye umri wa miaka 18 na Zaidi basi nenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwani wakati wa uandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura kulikuwa na kipengere cha kazi ya anayejiandikisha. Nenda huko wakupe data.
Kama ni idadi ya wafanya biashara nenda TRA na Halmashauri wakupe idadi wa wanaojiandikisha TIN na Leseni au Ushuru wa Masoko.
Kama ni idadi ya Wanafunzi na Wanavyuo, basi nenda Mashuleni na Vyuoni utapewa data.
Kama ni idadi ya Wafanya kazi nenda kwenye Idara, Taasisi na Mashirika yote watakupa data.
Baadae sasa wape kazi walioko Chini yako wakufanyie data analysis (Uchambuzi wa Data). Bahati nzuri kila Ofisi ya Mkoa ina Ofisi ya Takwimu. Wanao utaalamu huo.
Au kama huwaamini basi fanya simple mathematics za kutoa na kujumlisha. Kwa kuhusianisha vyanzo vyote vya data.
Tumia Akili kuliko nguvu na uwaache Polisi walinde Raia na Mali zao.