Mh.Makonda tumia fursa hii adhimu ipasavyo

Augustino Fanuel Massongo

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
1,278
666
Kwako Mh.Makonda pokea ushauri huu mfupi lakini maridhawa kwako ktk kipindi hiki unapopitia hali tete dhidi ya tuhuma za kugushi/kutumia cheti bandia zinazoendelea ktk jamii kinyume nawe.

Jambo la msingi usimjibu mtu yeyote kupitia microphone za wanahabari mbinu hii itafeli na kukuza tu malumbano badala yake waburuze mahakamani wote hasa wale waliokutuhumu hadharani kama Askofu Gwajima kwa kosa la kukudhalilisha, kukuchafulia jina na hadhi yako mbele ya jamii ukizingatia kuwa wewe ni kiongozi mkubwa wa serikali,

Hii itakusaidia mambo makuu mawili mosi utapata nafasi ya kujisafisha kwa kuweka wazi vyeti vyako halali (ambavyo naamini kwa vyovyote vile unavyo) mbele ya vyombo vya haki dhidi ya tuhuma za uongo wa adui zako lakini pia ni fursa nyingine maridhawa kwako kiuchumi kwani utadai na kulipwa fidia nono, ndio maana nashauri anza na Askofu Gwajima maana yuko ktk nafasi nzuri ya uwezo wa kiuchumi wa kukulipa mamilioni.
 
Back
Top Bottom