Mh Makonda, barabara Kitunda, Kivule & Magole

Mh Makonda, barabara Kitunda, Kivule & Magole

Charles Mkubya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2009
Posts
206
Reaction score
161
Nianze kwa kukupongeza Mh Makonda kwa juhudi zako katika kufuatilia kero za wananchi wako. Baada ya kuonekana taarifa ya Bw. Amos wa Kivule akizungumzia kero ya barabara ya Kitunda - Kivule, nimeona umetembelea na kuongea na wananchi wa eneo husika. Hii ndio ilitakiwa kufanywa na watendaji wako hata kabla hujaja wewe sababu si mara ya kwanza kusemea kero hii.

Pale ulipotembelea, kuna barabara nyingine ya Kitunda kwenda Magole. Wananchi wa Magole pia wanapitia adha hiyo ulioiona hapo na hasa kipindi hiki mvua zinapoanza huwa inakua karaha zaidi.

Unafanya kazi nzuri sana, hongera kwa hilo. Natamani kuona viongozi wa chini yako wakitoa msaada zaidi badala ya kusubiri issue kama hizi zije kufanyiwa kazi na RC. Bado tuna tatizo la usimamizi wa majukumu. Sitegemei uwe wazungukia miradi yote mkoa mzima wewe tu ilihali kuna watu ambao wangeweza kusaidia hili.
 
Hata kipande cha kitunda mpaka buza kupitia Mwanagati wakipige lami tu itawasaidia sana raia
 
Back
Top Bottom