OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,102
- 114,689
Wakuu ni mwezi sasa umepita tangu matokea ya kidato cha nne yatangazwe na NECTA. Matokeo haya yaliionyesha Dar Es Salaam kushika mkia katika matokeo ya ujumla kwani shule zake sita zilikuwa miongoni mwa shule kumi zilizoshika mkia
Tumeona wakuu wa mikoa mbalimbali na wadau wa elimu wa mikoa yao wakifanya makongamano ya kujadili kwa pamoja sababu za kufanya vibaya kwa shule zao pamoja na kuibua maazimio na mapendekezo ya namna na kukabiliana na changamoto
Hali ni tofauti kwa mkoa wa Dar Es Salaam na Mkuu wa Mkoa wake. Ukimya umetanda kana kwamba wameridhika na halo mbaya ya shule zao sita kushika mkia. Ikimbukwe kwamba Mkuu wa Mkoa Mh.Makonda wakati akishika ofisi ya Wilaya ya Kinondoni na hatimaye Mkoa alikuwa shirikishi na wazi katika kupambana na changamoto za walimu na elimu.
Nini tamko la Mkuu wa Mkoa Makonda kwa ma-zero haya waliyopata watoto hawa ambayo yanahitaji mjadala mpana kuweza kuiondolea mkoa aibu hii