domokaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2010
- 3,546
- 1,725
Sehemu ya kiwanja cha Shule ya Msingi Tabata Kisukuru kimevamiwa na matajiri na tayari bonge la mjengo umesimikwa ukiwa katika hatua za mwisho za ujenzi. Kiwanja hicho kilichotolewa na serikali na wananchi kuja kukabidhiwa na aliyekuwa makamu wa Rais Marehemu Dr Omari Ali Juma kilitengwa na shule hiyo kwa ajili ya michezo na sasa shule hiyo haina uwanja wa michezo. Nimetafuta mawasiliano ya Waziri Lukuvi bila mafanikio, yeyote mwenye kuweza kuwasiliana nae naomba amfikishie hizi habari ikiwezekana aje ajionee mwenyewe ukweli wa mambo