Mh Kangi Lugola:Madereva wote watapimwa kilevi kila penye mzani mpaka mwisho wa safari

Madereva haswa wa safari ndefu wapimwe macho na wawe wanalazimishwa kupumzika kila wakiendesha zaidi ya masaa kumi kwa magari yenye mizigo.
 
Huko ni kuwapa ulaji trafiki tu na kusumbua MADEREVA!Sikubaliani na hilo na kachemka sana!
 
Hili swala limeshajadiliwa sana humu na hakuna kiongozi mwenye political will to make things happen.Huyu waziri wangu wa mambo ya ndani kaanza na vituko na maagizo ya kukurupuka,yafuatayo yatapunguza sana ajali;barabara zetu bado ni mbovu mno,ukarabati unahitajika na alama za barabarani ziwekwe na ziwe rahisi kuonekana kwa watumiaji,magari yote lazima yawe na roadworthly certificate kabla ya kuruhusiwa kuwa barabarani,speed cameras za kudumu zijengwe ili kudhibiti mwendo,matuta yote kwenye freeway ways yaondolewe(hasa pale mbugani Mikumi) na badala yake waweke speed cameras zinazopima muda ambao gari inasafiri kutoka point A to B,zijengwe ARRESTER hasa kwenye miteremko mikali kama kitonga au Wami,driving licences zitolewe na traffic dept.na ziwe ndani ya systems ambao inaongea nchi nzima to each other,Demerit system ianzishwe kwa madereva wote,visiable policing iwepo sio police kujificha vichakani na vitoi vyao;ruhusu mabasi ya abiria kusafiri usiku na mchana ili kupunguza msongamano wa magari barabarani,mizani zote za kupima uzito wa magari ondoa (zinachangia msongamano usio wa lazima) badala yake tutumie technoloji kupima uzito wa magari(unaweka monitoring devices barabarani zenye uwezo wa kupima uzito wa gari linapoingia kwenye zone yake na kupeleka taarifa kwenye control room);sehemu kama milima ya pale Mbeya,Kitonga,Wami,Saranda tujenge line special ya magari makubwa ambayo yakifika sehemu hizo yanapita kwenye line hiyo na btn unaweka stop signs ambazo madereva watasimama,hii itasaidia kudhibiti mwendo wa gari linaposafiri kwenye maeneo haya .matambiko,ibada,Amiri za ajabu hazitapunguza ajali,tuelewe ajali its someone faulty sio mapenzi ya Mungu.
 
I see. Bila shaka kutaimarisha foleni na kuongeza muda wa safari. Lakini, kupima kilevi madereva ni jambo zuri na la kheri. Ila, napingana na huo utaratibu unaotaka kutumika kwa hizo sababu za foleni kubwa na kurefusha muda wa safari. Waziri anaweza kuomba na kupata ushauri wa wadau.
Hii ndio style yetu ya maisha siku hizi, kila kauli tutaikosoa. hebu fikilia angesema hivi.

1.Waziri: wapimwe mwanzo wa safari
Wakosoaji: Sasa si atasubiri apimwe zen anakunywa safari nzima
2. Waziri: wapimwe katikati ya safari.
Wakosoaji: mbona miaka yote wanapima haijasaidia chochote.
3.Waziri: wapimwe kilevi mwisho wa safari.
Wakosoaji: Sasa mwisho kama ni ajari si itakuwa imeisha tokea tayari wanazuia nini sasa.

4.Waziri: wapime kila kituo cha mizani
Wakosoaji: watasababisha foleni

Anyway ndio maisha tuliochagua na tumeambiwa kupinga na kukosoa ndio kazi ya upinzani na kazi yenu mnaifanya sawasawa.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh Kangi Lugola akiongea na East Africa Redio asubuhi kwenye kipindi cha Breakfast ameagiza kupimwa kilevi kwa kila dereva wa ambaye gari yake inapitia kupimwa uzito kwenye mizani mpaka mwisho wa safari na kurekodiwa ktk log book.


Shida haipo huko wanakotazama, shida ipo kwa wanaokabidhiwa majukumu hayo ya usalama barabarani, je ni waadilifu? hivo vipimo vitakuwa vinasoma centrally Dsm au askari ndiyo wanakuwa na matokeo?

Vyanzo vya ajali ni rushwa kila kona
 
Hii ndio style yetu ya maisha siku hizi, kila kauli tutaikosoa. hebu fikilia angesema hivi.

1.Waziri: wapimwe mwanzo wa safari
Wakosoaji: Sasa si atasubiri apimwe zen anakunywa safari nzima
2. Waziri: wapimwe katikati ya safari.
Wakosoaji: mbona miaka yote wanapima haijasaidia chochote.
3.Waziri: wapimwe kilevi mwisho wa safari.
Wakosoaji: Sasa mwisho kama ni ajari si itakuwa imeisha tokea tayari wanazuia nini sasa.

4.Waziri: wapime kila kituo cha mizani
Wakosoaji: watasababisha foleni

Anyway ndio maisha tuliochagua na tumeambiwa kupinga na kukosoa ndio kazi ya upinzani na kazi yenu mnaifanya sawasawa.
Yaani wabongo ni shida sana aiseee .....hawana dogo kabisa....
 
Kusema ni rahisi ila vitendo ndo kazi. Kipimo kimoja kwa mtu mmoja na hairuhusiwi watu wawili kutumia kipimo kimoja kwa sababu za kiafya. Najiuliza kama zoezi hili litakua endelevu ikiwa ukienda polisi kufuata loss report unapewa karatasi ukatoe photocopy ndo wakuandikie wataweza kwa vipimo hivi kwa madereva wote kila siku.
 
Back
Top Bottom