mh! Hii kitu ni balaaa!!

mh! Hii kitu ni balaaa!!

holygrail

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2012
Posts
1,303
Reaction score
597
usiombe ukakutana na haya majaribu yaan very unbearable!!..hii ni kwa hisani ya muke ya muzungu!!

"Nimeolewa huu ni
mwaka wa pili sasa
nashukuru Mungu
mume wangu
tunaelewana vizuri
kusema ukweli ni mwanaume anaejua
nini maana halisi ya
mapenzi ana utu anajua
thamani ya mwanamke
tunashirikiana katika
kila jambo,

kabla hatujaoana tulikua
kwenye uhusiano kwa
muda wa miaka 2 na
baada ya kuoana kwa
hii miaka 4 yote
hajawahi kubadilika hata kidogo.wakati
tunafunga ndoa
tulikubaliana kua baada
ya ndoa tutafute mtoto
haraka kwani sote
tulikua na hamu kubwa ya kupata mtoto.

baada
ya miezi kadhaa bila
mafanikio niliamua
kwenda hospital
kucheki afya
yangu ,nilikutwa na matatizo madogo
madogo ambayo
nilitibiwa nikapona
kabisa hapo mume
wangu alikua na mimi
bega kwa bega kuhakikisha nakua
sawa hospitali alikua
akienda na mimi na
kufuatilia kila
hatua.baada ya mimi
kumaliza matibabu tulishauriana na yeye
afanye
uchunguzi,mume
wangu hakusita hata
kidogo tuliongozana
kama kawaida yetu vipimo vikafanyika
majibu yalipotoka
hayakuridhisha

daktari
alisema kipimo cha
kuweza kutoa mbegu
za kuzalisha kiko chini tulishauriwa kurudia
vipimo tena ikawa hivo
hivo akafanyiwa na
upasuaji ili ijulikane
kama kuna mishipa
imeziba inayosababisha kuzalisha mbegu zenye
uwezo lakini mwisho
daktari akatoa jibu kua
hakina tatizo kwenye
mishipa ila tu ndivyo
alivyo zaliwa na hataweza kupata mtoto
maisha yake
yote.

kusema ukweli
ndugu zangu usiombe
kupata majibu kama
hayo.tuliishiwa nguvu na kurudi kwetu kimya
kimya.mume wangu
alikosa raha tangu siku
hiyo ingawa hapo
mwanzo alikua
anawajibika vizuri kitandani sasa akawa
hataki tena hata mwezi
unapita yupo kimya
nikajua ni msongo wa
mawazo ,nilijitahidi
sana kumuonyesha kuwa nipo nae katika
kila jambo ilikua ni
kipindi kigumu sana
kwangu kwani nilikua
na kazi ya
kumuonyesha kuwa hakuna
kitakachobadirika
katika maisha yetu.

kwa
kiasi kikubwa naona
nimejaribu mume
wangu ameanza kurudisha uchangamfu
na kuwa mwenye
furaha tena kama
zamani.maisha
yanaendelea na
mapenzi yetu yako pale pale kama kawaida
familia imenitolea
macho na kuanza
kunisema sema chini
chini kua sizai mi sijali
nampenda sana mume wangu na siko tayari
kutafuta mwanaume
mwingine nje.

ila sasa
tatizo najiuliza
itakuwaje na haya
maisha ya bila mtoto nikikaa na wanawake
wenzangu wakianza
kujisifia watoto roho
inaniuma sana siku
nyingine nakesha nikilia
ila siwezi kumuonyesha mume wangu kuwa
nina uchungu kiasi
hicho nalia kwa
kujificha.nimeanza
kujifikiria swala la
kupata mtoto kwa kupandikiza mbegu
japo naskia ni gharama
ila si tatizo pesa
tunaweza kuzichanga
changa zikapatikana ila
sina ujuzi sana juu ya jambo hili na sijui
atalipokea vipi
nikimwambia.kwa
kweli nateseka sana na
hili na sijawahi
kumwambia mtu yeyote hata ndugu
zangu wa damu
naogopa wasije
wakaanza kumshusha
na kumdhalau
mume wangu.na siko tayari kuachana nae na
siko tayari kuwa na
mwanaume mwingine
tofauti na
yeye.

Mh mambo hayo wapendwa. Mpeni ushauri dada yetu.
 
Ama hakika wewe ni mwanamke wa shoka,hongera sana na una mapenzi ya kweli,hayo ni maisha yenu na si wengine,kwanini msiasili mtoto?wajuzi watakuja kukushauri zaidi,pole sana...
 
watafute mtoto wa kupandikiza kama wanazo pesa.Au waje kwangu ninao watatu nimezaa nje mama zao wananichuna tu, bora niwape hao wawalee kwa mkataba maalum kwa kuwatambua kama wazazi walezi,ila mimi mzazi hasa heshima yangu iwepo ingawa nitaruhusu waende nae ulaya.
 
Ama hakika wewe ni mwanamke wa shoka,hongera sana na una mapenzi ya kweli,hayo ni maisha yenu na si wengine,kwanini msiasili mtoto?wajuzi watakuja kukushauri zaidi,pole sana...

mh hapo hujamsaidia dada yetu. Ingekuwa wote wabovu sawa!
 
watafute mtoto wa kupandikiza kama wanazo pesa.Au waje kwangu ninao watatu nimezaa nje mama zao wananichuna tu, bora niwape hao wawalee kwa mkataba maalum kwa kuwatambua kama wazazi walezi,ila mimi mzazi hasa heshima yangu iwepo ingawa nitaruhusu waende nae ulaya.

mh! Hii ngumu kumesa! Dada yetu hawezi hii.
 
Mungu aliyajua yote hivyo kualini kuwa ni kama ajali tu na mkubaliane na hali ilivyo tu
 
jamani aishi tu hivyo namapenzi na mumewe tu ndo ivyo tena
 
Pole sana dada, hakuna linaloshindikana kwa maulana wew zidi kuomba
 
bado nipo nipo kwanza namalizia togwa yangu na binti wa kimanyema
 
Hii ni ngumu. Sina uhakika kama hapa kwetu kuna utaratibu wa kuchangia mbegu za kiume. Najua tu kuna utaratibu wa akina mama kuchepuka na kupata mtoto bila baba kujua. Katika mila zetu za kale kulikua na utaratibu una mfix mdogo au kaka mtu bila yeye kujua kwa kushirikiana na mama mkwe. Hii ilikuwa inafanyika bila mume kujua.

Kwa kuwa mume anajua tatizo sasa inabidi mkubaliane njia ya kufanya. moja wapo kati ya hizi
1. Kuchukua watoto kwenye vituo vya yatima
2. Kwa pamoja Kutafuta mtu wa kuchepuka naye akupe mimba. bila yeye kujua mchezo

Lakin
 
Mkuu hiyo no 2 ni lazima ajue kwasababu yeye tayari ana tatizo la kutosababisha ujauzito.
Hapo bwana wakubaliane tu kama jamaa ana mdogo wake au ndugu/rafiki wa karibu amfanyie hiyo kazi,nnachokiona hapo nikua mwanamke anataka zaidi kuzaa japo vitu vingine vinawezekana,ushauri huu maana yake ni kwamba mkubali kutenda dhambi dah wape pole sana.
 
Back
Top Bottom