TAWA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 3,673
- 1,571
Baada ya waziri wa fedha uchumi na mipango mheshimiwa Mpango kuwasilisha kile ambacho serikali ilidhani kwamba ni mpango wa serikali wa miaka mitano, mwenyekiti wa bunge mh. Andrew Chenge alimwita mwenyekti wa kamati ya bajeti mgeshimiwa Hawa Ghasia ili atoe maoni ya kamati.
Katika hali isiyo ya kawaida mwenyekiti wa kamati ya bajeti alitoa maoni yake bila kufahamu serikali pale haikuleta mpango wa miaka mitano kama ilivyotakiwa na badala yake ulikuwa ni muundo wa kamati wa mpango.
Kilichonishangaza zaidi ni pale mh. Hawa Ghasia aliposema NAUNGA MKONO HOJA.
Jioni serikali iliondoa hoja yake mezani kwa kukiri kwamba walikosea. Sasa ndugu huyu alisema vile kwa mazoea kwamba ukiwa mbunge wa ccm lazima uunge mkono hoja yoyote ya serikali hata kama mbovu na haina maslahi kwa taifa?
Au naye alighafilika kama ilivyo kwa serikali?