Mh. Elibarick Kingu - DC Igunga

Mh. Elibarick Kingu - DC Igunga

mambomoto

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
326
Reaction score
236
Huyu ni DC na kada wa CCM ambaye pia katabia ka ufisadi amekuwa nacho tangu akiwa chuoni pale mzumbe nakumbuka alivyokula pesa za serikali ya wanafunzi (MUSO) akiwa kama Vice President. Jamaa huyu ni hatari sana kwenye issue ya pesa. Kuwa kada wa CCM naona yupo uwanja wa nyumbani kabisa.

Elibariki Kingu said:
Mimi Elibariki Kingu Mkuu wa Wilaya ya Igunga,nimesikitishwa na tuhuma zilizotolewa dhidi Yangu kuwa nilipokuwa Makamu wa Rais katika serikali ya wanafunzi(Muso).Mzumbe kwamba niliwahi kula fedha zilizochangwa na wanafunzi

Napenda ifahamike kuwa nimeitumikia ofisi ya wanafunzi (Muso) kwa vipindi viwili mfululizo na nimefanya kazi pale kwa ufanisi na uzalendo wa hali ya juu.

Haijawhi kutokea kabla ya hapo kiongozi wa Muso kuongoza nafasi Moja kwa vipindi viwili, hili kwangu liliwezekana tena nikiwa na umri mdogo.

Ufanisi na uadilifu niliouonyesha katika nafasi hiyo kwa muda wote ulifanya nitunukiwe tuzo ya ufanisi katika uongozi,nimepewa barua za pongezi "letter of appreciation" na menejiment ya Chuo na kupata vyeti vya uongozi uliotukuka.

Tuhuma kuwa kuna pesa za wanachuo nilizokula ndio nazisikia na kusoma kupitia Jamii Forums,ni vema tukaacha mzaha wa kuwapa watu tuhuma bila uthibitisho usio na ukweli wowote.

Kuhusu kuchukua trekta kama ilivyochangiwa humu kwamba nilichukua kwa mgongo wa vijana hili si kweli sijafanya hivyo kwa kuwa mgongo wa yeyote ni vema wakaanza utamaduni wa kumuogopa Mungu kwa kuacha tabia ya kutunga hadithi za kitoto.

Binafsi ninayo trekta niliyokopa kupitia taratibu zote za ukopaji na zile za kiserikali na so vinginevyo.

Pia nimewezesha kuleta trekta nne katika wilaya ya Igunga ambayo leo yanakabidhiwa kwa wakulima waliojiunga katika vikundi, zoezi hili litafanywa na katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.

Kuhusu mgogoro wa wafugaji na wakulima Igunga ieleweke kuwa ni wakulima wa Igunga ndio waliovamiwa na wafugaji kutoka Kishapu na wakauliwa zaidi ya watano.

Katika migogoro hiyo ya ardhi Mimi ni kiongozi niliyeweza kuweka rekodi kwa kutatua migogoro mikubwa ya ardhi ikiwemo ya Mwanzugi, Mgogoro uliodumu kwa miaka 12.

Niliweza kuumaliza kwa katika kipindi kifupi cha uongozi wangu na ilipelekea ripoti ya mgogoro huo kutatuliwa kutangazwa katika vyombo vya vya habari vikubwa duniani ikiwemo CNN na BBC nami kupata pongezi kutoka lands zote za dunia.

Hiyo sihusiki wala kuendesha mashamba ya umwagiliaji Igunga kwa kuwa sina tabia ya kujilimbikizia Mali

Kuhusu malalamiko ya mapunjo ya fidia ya umeme kwa wananchi wa Igunga Mimi ndiye niliyeshughulikia kero hiyo kwa kuagiza Takukuru kuchunguza na kuwachukulia hatua waliohusika na malipo.

Sihusiki kwa namna yoyote na ubadhirifu wala sijawahi kutuhumiwa kwa kukosa maadili.

Nimeiongoza wilaya ya Igunga kwa ufanisi na kuwa mfano kwa kufungua ajira ya vijana katika sekta ya kilimo na uzalishaji katika maeneo yote.

Nimeweka maridhiano ya kisiasa katika wilaya kwa kutoa uwanja huru kwa vyama vyote name sasa wana Igunga no wamoja.

Hivyo basis mwenye tuhuma dhidi yangu anapaswa azithibitishe badala ya kuandika kwa dhana na dhamira ya kunichafua.

Nimechagua kuwa mzalendo kwa taifa langu nitaishi hivo kwa kufanya kwa bidii na katika taratibu zinazokubalika, nitajitoa na kujituma kwa ajili ya watanzania popote nitakapokuwa huku nikiongozwa na dhamira njema kwa nchi yangu

Ni mategemeo yangu kuwa haitajitokeza tena

Wenu Elibariki Kingu
Mkuu wa wilaya Igunga.
 
Aliiba malipo ya fidia ya vijiji ambapo nguzo za grid ya umeme ya taifa inapita
 
Mkuu kwenye issue ya Fidia ya Tanesco kwa wananchi wa Igunga hawezi vuka kihunzi,tayari watumishi wa halmashauri wameanza kusimamishwa,Mpima ardhi pamoja na cashier,Bw.Kingu ndo alikuwa mwenyekiti wa kamati
 
kuna tetesi kwamba amewezesha kupatikana kwa trekta la kuhonga kiongozi wa cdm .
 
Huyu ni DC na kada wa CCM ambaye pia katabia ka ufisadi amekuwa nacho tangu akiwa chuoni pale mzumbe nakumbuka alivyokula pesa za serikali ya wanafunzi (MUSO) akiwa kama Vice President. Jamaa huyu ni hatari sana kwenye issue ya pesa. Kuwa kada wa CCM naona yupo uwanja wa nyumbani kabisa.

Aliiba malipo ya fidia ya vijiji ambapo nguzo za grid ya umeme ya taifa inapita

Mkuu kwenye issue ya Fidia ya Tanesco kwa wananchi wa Igunga hawezi vuka kihunzi,tayari watumishi wa halmashauri wameanza kusimamishwa,Mpima ardhi pamoja na cashier,Bw.Kingu ndo alikuwa mwenyekiti wa kamati

kuna tetesi kwamba amewezesha kupatikana kwa trekta la kuhonga kiongozi wa cdm .
fitna tu hizo hata kama hatuipendi ccm,dogo ni kiongozi sina wasiwasi nae
simjui vizuri sana ila mara ya kwanza tulikutana bungeni wakati anagombea MP eac,then akiwa DC wa kisarawe anaonyesha ni kijana mwenye vision nzuri
 
Kumbe wewe ulikutana naye bungeni juzi? sisi tumesoma naye tumeishi naye. Sasa wewe utakuwa Obama wa Uongo siyo Bongo
 
ukweli utajulikana soon
 
huu utaalam wa propaganda umemtokea lema bungeni leo, ametumia muda mwiiingi kumchafua ole medeye tangu akiwa waziri kumbe ni baada ya kugundua kuwa medeye anagombea ubunge arusha mjini mwakani...haya mleta mada unagombea jimbo moja na kingu???
 
Kumbe wewe ulikutana naye bungeni juzi? sisi tumesoma naye tumeishi naye. Sasa wewe utakuwa Obama wa Uongo siyo Bongo

Huyu Hajuhi Kitu. Naweza Kusema nilimtoa kwa Mkono wangu Mwenyewe kwa Kuvunja na Kufunga Ofisi yaSerekali ya wana Chuo Mzumbe(Pale mbele ya White house). Nakumbuka alikuwa Spika wa Bunge, na Tuliunda serekali nyingine mpya Kabisa.
 
Hhaa! Ngumi Labda akapige Polisi wa JK lakini sio kwa watu wanaojitambua. Jeuri najua mmnampa baada ya Kupiga Polisi kipindi kile na kamakama chama cha majambazi mulimkingia Kifua.
ngumi jiwe za kiutendaji sio hizo za akili ndogo kama za kwako
 
huu utaalam wa propaganda umemtokea lema bungeni leo, ametumia muda mwiiingi kumchafua ole medeye tangu akiwa waziri kumbe ni baada ya kugundua kuwa medeye anagombea ubunge arusha mjini mwakani...haya mleta mada unagombea jimbo moja na kingu???

Wewe kweli nazi, ubunge kwako ndo kila kitu
 
Wajinga kukesha kumzungumzia maisha ya mtu na kumchulia mabaya, welevu kukesha wakifikiri jinsi gani ya kuleta maendeleo!

Hamna jipya nyie Kingu ni miongoni mwa MaDC bora katika kizazi Hiki kipya! Kingu ni kweli ngumi jiwe chapa kazi usirudi nyuma! Tena Kwa taarifa yako Kingu anafaa kabisa kuwa RC.

Songela sana Kingu chapa kazi hizi kelele za chura!
 
Kingu ni zaidi ya DC kwa hakika mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Kingu anafaa kuwa hata RC ameonesha uwezo mkubwa katika kipindi kifupi!

Hivi vijana tumerogwa na nani? Hata wewe mkeo anakulalamika hakuna mkamilifu! Tuwe na tabia ya kupongezeana wenyewe kwa wenyewe!

Wivu wa kike midomo mirefu!
 
Kingu wee ni kijana bora sana! Wana Igunga wanakupenda na watazidi kukupenda!

Kingu chapa kazi bro!
 
kingu ni kichwa, zalendo wa kweli, mtendaji smart, kijana mwenye upeo mkubwa na msomi asiyeabudu miungu watu....utamchafua kwa uongo na uzushi unadhani utafanikiwa??? mleta mada anaonekana ni mtumishi mzembe katika wilaya ya kingu sasa ameamua kuja kumchafua huku
 
Kingu atahesabiwa kwa maendeleo ya wilaya ya igunga, atahesabiwa kwa uadilifu sio kwa majungu ya jf
 
Huyu ni DC na kada wa CCM ambaye pia katabia ka ufisadi amekuwa nacho tangu akiwa chuoni pale mzumbe nakumbuka alivyokula pesa za serikali ya wanafunzi (MUSO) akiwa kama Vice President. Jamaa huyu ni hatari sana kwenye issue ya pesa. Kuwa kada wa CCM naona yupo uwanja wa nyumbani kabisa.
Weka ushahidi, ikiwemo vielelezo sio unabweka kama mbwa aliyezaa
 
Back
Top Bottom