Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?


Mkuu, sisi wa zamani tunaikumbuka hiyo. Hicho ndo kilifanya Mwalimu amkatae EL.
 
Tuzidi kumwomba Mungu amjaalie EL afya njema up to 2015.
 
Pasco,

Nimepita tu ... ninaogopa kuuliza maswali maana huwa unayakwepa.
Keil, umefanya busara kupita tuu bila kuuliza maswali pia ni kweli kuna maswali mengi juu ya Lowassa mimi nayakwepa kwa sababu kwanza mimi sio CCM, pili mimi sio kibaraka wa Lowassa, sio mpambe wake na wala sio msemaji wake, sijatumwa wala silipwi bali nayafanya haya kwa mapenzi mema ya taifa letu!.

Maswali mengine nayakwepa just to save the best for the last maana ngoma ikipigwa sana mwishowe hupasuka!. Hii ngoma ya mkesha, saa hizi ni katikati ya usiku, hivyo sitaki kuipiga sana hii ngoma isije tupasukia kabla hakujechwa!.
 
Kwame Nkrumah, asante kwa hili, kama jf ni reflection ya cross section ya jamii yetu Watanzania, basi safari ya ukombozi wa kweli bado ikingali mbali!.

Kusema ukweli sijawahi kuwazia kuingia kwenye siasa, ila issue ya ignorance ya watu wetu inataka kunilazimisha kufika huko, kusema kweli kuna baadhi ya mijitu Mitanzania ni mijinga ajabu mpaka natamani nishike nyundo ni komelee misumari ya sense kwenye mibichwa yao!.
 
Akili Kichwani, kama ulidhani mimi ni mtakatifu you must be wrong!, vile vi little brown envelopes vya media nimeshavikunja sana tuu mpaka sasa mimi ndio navigawa!.

Kama unaishi kwa ujanja ujanja kuvitegemea hivyo vibahasha, ili uweze kuvivuta vingi, lazima urefushe muda wa kazi kwa kuanza mapema!, hivyo this is the right time kuanza kuvuta, tena kwa kuzingatia nilianzia kausafiri ka boda boda, sasa niko kwenye bajaj, mpaka kufika 2015, Vogue itakuwa barabarani!.
 

Anayejua pesa anatoa wapi ni yeye mwenyewe na mkewe, kuhusu habari zake kupewa kipaumbele na vyombo vya habari labda anafanya mambo yanayoigusa jamii.
 

Ngoja twende nao taratibu wataelewa tu ikifika 2015.
 
Acha tu, kuna watu nimeamini sasa si tu wanaweza kuuza huo utu, wanajiuza miili na akili zao, kwa ajili ya viji pesa.... ni hatari sana kwa watoto waliuo na wazazi wa aina hii.....

Wanaojiuza ni waliongia mikataba ya kinyonyaji ya Bulyanhulu, Kahama, ATC, TRL na mingine mingi. Lowassa aliweza kuvunja mikataba isiyo na ufanisi kama hii. mfano ni CITYWATER na mkataba wa kuuza eneo lote la Mnazi Mmoja. NI nani unamjua amewahi kufanya hivyo kama si Nyerere, Sokoine na Lowassa?
 
Okada, ndani ya CCM hakuna zaidi ya Lowassa!. Dr Salim ni "spent force", Sitta ni too ambicious ana pupa na papara ( "mwenye pupa hadiriki kula tamu"). Magufuli ni dictator tena huyu anaweza kuamuru utekelezaji wa ile adhabu ya kunyongwa itekelezwe instantlyhalafu rufaa ifuatie baadae, tofauti yake Mrema, Magufuli ni genius upstairs!. Dr. Shein is too good kwa uchafu uliopo CCM, who else?. Mwandosya/Mwakiembe ndio hivyo tena (I Wish then get well soon). Nani kwenye CCM ana guts za kulinusuru taifa hili hapa lilipofikia hoi bin taaban!. Kitu kinachaweza kuifanya CCM isimteu Lowassa ni uoga wao maana nakuhakikishia Lowassa akiingia, hadi JK atasimamishwa kizimbani kwa kosa la ....(naomba nisilitaje tusije itwa wachochezi)!.

Kwenye hili la usafi wa Lowassa nimeisha lizungumza sana!. CCM are devils!, but betwen the two devils, choose the lesser!. Kati ya Mashetani CCM, Lowassa ndiye mwenye afadhali!. Anaiba na kuketa maendeleo, hii mijizi mingine mbona nayo inakwiba, inafanya nini?.

Guts za kumjibu Nyerere?!. Hii ndio ameonyesha ukomavu na heshima ya kiafrika kwa wazee wetu!. Ulitaka ajibizane na Mwalimu?. Wewe ukimkosea Baba yako ukigombezwa utajinyamazia au utajibishana nae?. Alichofanya Lowassa was very right, ukikosa unakaa kimya na kama ni kitu cha kutia hasira usithubutu hata kuuleta uso wako mbele zake!.

Hii la heshima na ushujaa, Lowassa ni mpaka amepitiliza!, just imagine zigo la Richmond alilotwisha!. Zigo hili linamwelemea lakini yupo tuu, amejinyamazia!. Niambie nani mwingine ndani ya CCM ana kiwango cha ustahimilivu na uvumilivu hata wa nusu tuu ya Lowassa?. Hakuna!.
 
Gracious, natumaini mengi ya majibu ya maswali yako umeshayapata kupitia michango mbalimbali na sikukujibu wewe specifically ili kuondoa dhana ya tunamsafisha kutafuta uubgwaji mkono na watu!. No, tunamshafisha ili kuwafungua macho Watanzania waone jinsi CCM ilivyo chafu imeoza kwa rushwa na ufisadi toka juu mpaka chini kiasi kwamba huyo Lowassa ambaye wamemtoa kafara kuonyesha CCM ni safi na yeye ndie mchafu, its quite the opposite Lowassa sasa ndiye msafi na ndiye pekee ataweza kuipatia nchi hii ukombozi wa kweli!.
 
Kama upendo wake kwa swahiba wake na nchi yake limekuwa kosa, then tumhukumu kwa hilo!. Ila kwa sisi tulio na imani ya Kikristo, Lowassa ana upendo wa Agape kwa chama chake!. Kwa maana jinsi Mungu alivyoupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe mpendwa wake, aje kuukomboa ulimwengu, ambapo alizibeba dhambi zetu na kwa kuteswa kwake, sisi tuliponywa!.

Vivyo hivyo kwa jinsi Lowassa alivyoipenda chama chake cha Mapinduzi, akajitoa nafsi yake, akaubeba msalaba wa Richmond, na kwa kuteswa kwake, CCM ikaponywa!.

Kuna mahali tumeelekezwa tuchukuliane mizigo kwa upendo!. Ule msemo wa kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe, unaapply kwa ile siku ya mwisho tuu, ile siku ya hukumu!.

Mimi sio mwana CCM na sina chama, hivyo nyinyi wana CCM wenye mapenzi ya dhati kwa chama chenu, just imagine ingekuwaje kama Lowassa asingebeba hilo zigo la Richmond?!. Mngekuwa wageni wa nani saa hizi?. Hao mnaowasifia kwa kuwaimbia nyimbo za shangwe na mapambio si wangeshaozea Keko kitambo!. Badala ya kumshukuru Lowassa kwa kukinusuru chama chenu ndio kwanza mnampigia vuvuzela la kujivua gamba?. CCM isipomsimamisha Lowassa, itapata laana ya ukosefu wa shukrani na itaadhibiwa milele!.
 
Usafi pengine una maana pana zaidi kwenye siasa

Maswali yako ni ya msingi sana ngoja Pasco aje atujibie maana hata mimi nina kiu ya majibu...
bht natumaini majibu umeyapata!.
 
Ndugu yangu Malunkwi, kumbe wewe bado hujajua kuwa CCM ndicho chama chenye hati miliki ya kutawala nchi hii milele?. Amini nakuambia CCM hata ikisimamisha jiwe, linachaguliwa sembuse Mtakatifu Lowassa!.
 
Ndugu yangu Wambandwa, Tangu baada ya Baba wa Taifa, waliifuatia wote ndio hivyo tena, mmoja alitoa ruksa za kila kitu hivyo kujenga matabaka ya wenye nacho na wasio kuwa nacho. Aluyefuata alifanya biashara mahala patakatifu, sasa hivi pale ni pango la wahalifu, hivyo kumpitisha Lowassa makes no difference.

Nakubaliana na wewe CCM wote wezi, ila kwenye wezi hawa, kuna wenye afadhali, na Lowassa ndio miongoni mwao!.
 
Knowless, kwanza asante kunigeshimu, heshima ya kweli inajegwa, haiji tuu hivi hivi, sasa kama nilijijengea heshima huko nyuma lakini kwenye issue hii ya Lowassa ninajivunjia heshima yote niliyojijengea!, then nakubali heshima hiyo na ipotee.

Mimi siogopi kugombana na rafiki/ndugu na jamaa zangu katika jambo ambalo tutakuja kupatana!. Kuhusu Lowassa bora tugombane tuu na heshima ishuke, mbele ya safari tutapatana tuu na nitaijenga tena!.

Nikimalizia la bei yangu, amini usiamini mimi sina bei, ni bure kabisa!. Kama una issue yoyote kwa maslahi ya taifa, nitasimama na wewe kama ninavyosimama na El ateuliwe kuwa mgombea wa CCM!.
 
Gracious, hili la kumtenganisha Lowassa na Richmond, tusiandikie mate, wino upo and its only a matter of time!.
 

Hebu jikumbushe ubabe wake ulivyogonga mwamba kwa DC wa Shinyanga mjini.
 
Pasco,

Nimepita tu ... ninaogopa kuuliza maswali maana huwa unayakwepa.

Ni kwlei kabisa, kwa maana hadi sasa hakuna aliyweza kujibu utajili wake umetokana na nini. waakti watetezi wake walipigania rekodi yake ya utendaji (ambayo inafutwa kabisa na ufisadi wake), wana JF wanauliza utajili wake umetoka wapi? This is the dilema, ndio maana huu mjadala hauishi
 

Usitegemee majibu ya maana kwa maswali haya. hawa watu wanaroho ngumu kama paka, (kama ya EL) yaani wanang'ang'ania mada ilkiyokufa, haina nguvu za hoja, lakini wapo tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…