Mh. Edward Lowassa na vita dhidi ya taaluma ya mitandao ya kijamii (troll)

John Okello

JF-Expert Member
Sep 24, 2014
459
207
MH. ERWARD LOWASSA NA VITA DHIDI YA TAALUMA YA MITANDAO YA KIJAMII (TROLL).
Tangu tarehe 7/02/2008 ambapo kiongozi mzaliwa wa Ngarash Monduli mwaka 1953 ajiuzulu nafasi ya uwaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa iliyoitwa scandal ya Richmond imepita miaka kadhaa ambapo mimi pia ilinivutia kuianza rasmi safari ya kumjua kiundani kiongozi huyu na mambo yanayomzunguka.

Nashukuru safari ya kumjua kiongozi huyo na mambo kadhaa yanayohusu kiongozi huyu yalichagizwa na vyanzo mbalimbali kama wasomi mbalimbali, viongozi wastaafu na hata tovuti yake www.elowassa.com , n ahata pia kwa vijana wanao muunga mkono www.4umovement.com vyote hivi vilinijengea ujasiri wakuibua maswali mengi ya msingi na kwa kina dhidi ya zengwe mbali mbali ambazo zinaendelea katika mitandao ya kijamii na kuniachia swali hii sio ule weledi ambao kitaalamu hufahamika kwa neno la kiingereza troll ( kuibua hisia za mtu katika mitandao ya kijamii) kwa Edward Lowassa. Sasa naomba nieleze hili neno troll lilivyo na mahusiano na hizi hoja taratibu kama ifuatavyo.


1.UFISADI
Hii ni hoja ambayo kila uchao yeyote ambae atakua anampinga Edward Lowassa basi ndio funguo ya kuanzia popote atakapo simama, siko hapa kuyashusha matusi au kuwakosea heshima walioshika nyadhifa kubwa katika nchi yangu au kuonyesha nidhamu ya woga kwa taifa linalohitaji ukombozi wapili wa kiuchumi baada ya ukombozi wa Baba wa Taifa hayati Mwl.Nyerere na mapambano yaliyoendelezwa na viongozi wa awamu zote, ila nipo kukujuza na kama utambuavyo kuwa hii kashfa kwa Lowassa ilianza muembe Yanga na Dr. Slaa aliopo toa orodha ya kwanza ya mafisadi hadi katika magazeti na watu kukaa hadi vikao wakitaka jina la Lowassa na bahati mbaya jina la Lowassa halikuwemo wakilenga atajwe katika scandal ya DAWASCO na kizuri zaidi serikali ilishinda katika kesi ile kwa maamuzi magumu ya Lowassa mpaka akahoji katika kikao cha ndani NEC mbele ya mwenyekiti kipi nilikifanya usicho kijua?

Na huu ndio muendelezo wa mashambulizi hadi katika scandal iliyoitwa Richmond. Baada ya kujiuzulu kwa kiongozi huyu 2008 nilifuatilia sinema ile kwa umakini na nilishangazwa kuona kesi iliyofunguliwa dhidi ya Richmond na kuelezwa kuwa kampuni hii haipo na wala haijawahi kuwepo inashindaje kesi na mashauri yake yote yaliyo funguliwa dhidi yake ?, pili inakuwaje serikali inakubali mitambo inauzwa kwa DOWANS na baadae SYMBION kwa baraka za baraza la mawaziri?, inakuwaje mitambo hiyo inagharimu pesa za wamarekani ambao tunaamini wapo makini kwa waziri wao wa mambo ya nje H. Clinton na Rais wa Dunia Barack Obama wanaikagua kwa ziara ya gharama za fedha za Wamarekani?. Jibu hapa vita dhidi yake na mipango ilikwama na wanaposema fisadi alifisadi nini ? au ndio trolling mitandaoni dhidi yake?.


2.KUJIVUA GAMBA Naweza sema wale ambao watakua na weledi wakuchambua mambo ya kisiasa hapa watakua wanarejea taratibu na mimi kipindi kile ambacho msemo huu ulipata kusikika sana na sekeseke la kisiasa ndani ya chama tawala CCM. Wanaojua chama tawala nje na ndani na utundu wangu wa kutaka kuyajua mambo nilipata kujua manabii 11 wa chama cha mapinduzi na hapa ndipo migogoro huanzia, hoja hii ilizaliwa miongoni mwa mitume hii ya chama tawala iliyo endesha vita dhidi ya Edward Lowassa mpaka kujiuzulu sasa nia ilikua ni kumtoa kabisa katika ramani ya siasa na uongozi wa nchi hii wakiwa wana hoja ya kukisaficha chama kwani kilishuka katika matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Hapa ni ukweli wa wazi walikuwa ukiwalenga ndugu Edward Lowassa,Rostam Aziz na Andrew Chenge wakiwa wanadaiwa kukiangusha chama katika uchaguzi na kusahau kuwa mipango mibovu iliyokuwepo kichama na kutafunana wenyewe kwa wenyewe, lakini kwa umakini mkubwa na utulivu ambao nathubutu kusema ni malezi ya baba wa taifa hayati Mwl. Nyerere pale alipoamua kuwachukuwa wahitimu wa chuo kikuu Dar es salaam baadhi mwaka 1977 kuitumikia TANU na baadae CCM ndio uliomvusha kiongozi huyu huyu na ni sinema ile ile ya kumpinga Jk 2 kabla ya kuwa Rais 2005 ilikuwa inaendelezwa kwa Edward Lowassa. Hawa ni watu ambao siku zote waliazimia chama cha mapinduzi kifie mikononi mwa Dk.Jakaya.


3. ALIKATALIWA NA HAYATI BABA WA TAIFA MWL. NYERERE
Edward Lowassa hawezi kuwa rais sababu alikataliwa na Mwl. Nyerere , hii ni miongoni mwa hoja ambazo huniacha hoi si kifikra tu hata kiuhalisia na kujiuliza ni kwa sababu tu Mwalimu hayupo hai ndio maana haya yanawatapanya nyie mnao kinzana nami fikra au ni mwendelezo wa hoja zile zile za akina fisadi?? Ukweli wa historia ya Edward Lowassa haukuwahi kufungiwa katika masanduku, mara tuu baada ya kuhitimu chuo kikuu mlimani 1977 Edward Lowassa akiwa ameaminiwa na kwa heshima waliopewa na Mwalimu yeye na wenzake akiwamo raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya, Isidori Shirima,Chiligati , Mkuchika na wengineo waliajiriwa moja kwa moja na Chama tawala TANU na kuanza kazi akiwa ameaminiwa katika ngazi mbali mbali ndani ya chama mfano akiwa msaidizi wa Hayati Simba wa Vita pale Lumumba 1987,

Alikwenda Ubelgiji kupokea nishani kwa niaba ya Mwlm J.K Nyerere, Lowassa amedumu ndani ya chama na anakijua vyema na kama ilivyo desturi ya muasisi wa chama alikuwa na falsafa moja uongozi ndani ya chama unahitaji muda na subira ukiwa unaendelea kuijua nchi na chama, haya yalitokea kipindi cha mwaka 1995 ambapo vijana hawa wawili walipo jitokeza kutaka kugombea mwalimu alikuwa wazi hivyo aliwaambia subirieni huku Lowassa akiambiwa asubiri kabisa kuingia katika demokrasia ya chama katika nafasi ya ukuu wa kaya mpaka nyakati za Mkapa na Jakaya zipite ili kuweza kulitumia vyema kundi lile aliloliamini kulipa madaraka katika ngazi mbali mbali , Je ni wapi iliandikwa na mimi ninukuu kwa maandiko hayo kuwa Lowassa hafai kuwa Rais kutoka katika kinywa Cha Mwalimu Nyerere ? Sina maana nampigia kampeni bali ni maswali ninayo jiuliza dhidi ya mwendelezo wa mbinu chafu juu yake yaani trolling.


4.VISASI NA HOJA YA USULUHU NDANI YA CHAMA Sasa imefika nyakati chama tawala kimeamua sasa kutojadili hata kidogo namna gani shida na dhiki za Watanzania zinaweza kutatuliwa mathalani huduma za afya, maji safi, changamoto ya ajira ,miundombinu na makazi bora ya watu wa hali ya chini na kujisahau kabisa kuanza kujadili ni nani na nani wana visasi na nani basi wampishe fulani ambaye hana makundi, nalisema hili ikiwa sasa taifa lina aminishwa kuwa ndugu Edward Lowassa anavisasi na baadhi ya makundi hivyo hapaswi kuwa Mgombea uraisi, kwani akipata atalipa visasi.

Ni ukweli Lowassa kama binadamu ana visasi tena visasi dhidi ya wafuatao moja Ujinga, Maradhi na Umasikini kwani Hayati baba wa taifa alipo mlea ndani ya chama yeye pamoja na Rais Jakaya na wengineo waliambiwa hawa ndio maadui wa TANU na Serikali tangu mwaka 1977 analitambua . Hivyo kama kiongozi jazba na hasira dhidi ya utatuzi wa haya anao, nasi kama inavyo aminishwa ana makundi na visasi dhidi ya watanzania wenzake huu ni uongo na si hoja ya kuwashughulisha Watanzania kwa sasa ambao wana kiu na maendeleo. Visasi wanaongea wale wanaofanya ufisadi wa kweli leo na ambao wanaendelea kumtukana yeye, wamepata uoga wa ujasiri wa Watanzania wa kutaka mabadiko. Leo wameongezwa watu wa kuibia kodi za bandari yetu kwa ajili tu ya pesa kumchafua Lowassa?

Miradi ya mafuta machafu na mwishowe ESCROW ndiyo uchafu wa ajabu zaidi, Rais Kikwete amesikitika sana na jinsi watu aliowaamini walivyomuangusha, na wote leo hii wanamdanganya na kumtisha ili wao waendelee kulinda maslahi yao au niamini wazi kuwa sasa chama tawala hakina viongozi bali kina watawala na watawala hawa wanayumba kwa ombwe la manabii wake, au ndio weledi wa troll ukifanya kazi.


5. KUHUSU UGONJWA Hapa ndipo ambapo ule weledi wa wenzetu walio somea na kuwa na uzoefu wa zaidi ya miaka ishirini na kuwa matajiri wakubwa katika dunia ya leo unaofahamika kwa jina la kitaalam Troll ninavyo uona unatumika ndani ya nchi yangu kwa manufaa ya watu wasioitakia mema nchi yangu.

Lowassa ninaye mfahamu mimi kama Mtanzania huyu ni binadamu kama mimi, moja anaugua magonjwa ambayo wanadamu wengine huyapata na ni binadamu wakawaida, ila mtu anaposimama na kusema Lowassa mgonjwa ikiwa yeye tu kwa taaluma ni mhasibu au mwanasheria ananishangaza!! pili Lowassa anautaratibu ambao wa wazi amabapo hata watu wakawaida kabisa waliopo Dodoma humuona Asubuhi kila siku akifanya mazoezi awapo huko, sasa napata majibu kuwa hawa watu wanatengeneza mazingira ya huyu kiongozi kusimama na kuanza kuwajibu watu ambao walikaa tu katika vijiwe vya kahawa na kufurahishana kwa soga au walichanganyikiwa kwa picha za gazeti mzee akifanya ratiba yake ya kila siku?


6. KUCHANGANYIKIWA KWA MATOKEO MBALI MBALI YA RIPOTI JUU YA NANI ANAFAA KUIONGOZA TANZANIA. Sio siri tena kwani wasomi mbalimbali na taasisi zao mfano pale chuo kikuu cha Dar es salaam kitivo cha siasa kikiongozwa na TEMKO, asasi nyinginezo kama SINOVET bila kusahau majarida kama African Continent zote zimefanya tafiti mbalimbali kujua mustakabali wa kiongozi ambaye Watanzania wengi wanamtazamia kuwa Rais, majibu yanaonyesha wazi Lowassa anaongoza kwa asilimia kubwa akiwaacha mbali viongozi wengine wote wakiwa na asilimia chache mno. Hii inawapa shida mno hawa wapinzani wake, wanatafuta kila namna kupambana na hili, kumpotezea sifa na hata kumdhohofisha kisiasa na kujaribu kumfanya apayuke au kufanya lolote lile ambalo watapata pakusemea.hakika Lowassa anafanya vyema kukaa kimya na ndio uongozi aliowafunza hayati Baba wa Taifa.

MWISHO Edward Lowassa hajatangaza nia ya kugombea urais na wapinzani wake wamesahau kuwa ametangaza safari ya matumaini kwa Watanzania ,safari ambayo itakuwa ni ya ukombozi kwa mkulima na mfugaji, mwalimu na mwanafunzi, vijana na wazee, watumishi na wafanyabiashara, sasa akiwa katika utekelezaji wa safari ya matumaini chama kika muhusisha na mbio za urais na kumpa onyo.

Pia manabii hawa wanasuka kila njama kumgombanisha na mwenyekiti wa chama tena mpaka na familia yake vitu ambayo havina msingi mbele ya mahitaji ya Watanzania. Nina shauri kwa sasa watumiaji wa hii mitandao ya kijamii ni bora tuka jadili mahitaji yetu kama Watanzania na kuangalia kwa kina nani atatufaa na tutamuhitaji wakati ukifika, walio CDM wakajenge chama na demokrasia, walio CCM wakamalizie utekelezaji wa SERA na tulio mtaani huku tuendelee na mapambano ya kulijenga taifa hili na sio matusi au kufanya (trolling) kwa viongozi wetu kama Edward Lowassa , Mkapa, Warioba na Wengineo..

 
Well spoken,hizo hoja ulizoainisha hapo juu kuna mtu anaitwa Chabruma, amekomaa nazo kila uchao yeye anaandika tu thread zisizo na ushahidi kwa kutumia hizo hoja dhaifu hapo juu akishirikiana na ndugu yake Lizaboni, na hotlady,
 
Last edited by a moderator:
Well spoken,hizo hoja ulizoainisha hapo juu kuna mtu anaitwa Chabruma, amekomaa nazo kila uchao yeye anaandika tu thread zisizo na ushahidi kwa kutumia hizo hoja dhaifu hapo juu akishirikiana na ndugu yake Lizaboni, na hotlady,

wengine ni: Weston Songoro, Pipitofitamu, Mzizi wa mbuyu, Simiyu yetu, Mjepo, na wengineo......hawa watu they have nothing worth to say than attacking personality.... Nawasikitikia kwani badoo wametawaliwa kifikra.
 
Kwa kutumia hiyohiyo troll bwana okello hebu tufafanulie kuhusu hizi habari za kuwa mwl alimsifia sana huyu mteule wako juu ya utajiri aliyojipatia kwa muda mfupi sana wengine huitwa ukwasi?


Kwa maneno rahisi nini chanzo cha huo ukwasi wake? Kama anao kweli? Au ndio huo utumishi uliotukuka na kuaminika kwa chama na serikali chini ya mwalimu. Tuelimishe tafadhali... karibu.
 
  • Thanks
Reactions: 999
Umenena vyema kaka...kwa hakika umethibitisha wewe ni graet thinker........safi sana tupe Lowassa kiundani ili tuzidi kumjua na sio matusi kama wale majamaa wa WAMA........kwa sasa kila kundi la watu kumi kijiweni 8 umuunga mkono mwamba wa kaskazini, na ukiwauliza kwa nini? bila kusika wanakujibu ni kwa sababu ni mtendaji bora na ni mtu wa kusema na kutenda.........
 
Kwa kutumia hiyohiyo troll bwana okello hebu tufafanulie kuhusu hizi habari za kuwa mwl alimsifia sana huyu mteule wako juu ya utajiri aliyojipatia kwa muda mfupi sana wengine huitwa ukwasi?


Kwa maneno rahisi nini chanzo cha huo ukwasi wake? Kama anao kweli? Au ndio huo utumishi uliotukuka na kuaminika kwa chama na serikali chini ya mwalimu. Tuelimishe tafadhali... karibu.

Nyie sii mumejiandikia kile kitabu cha KISOKYA anayedai kuwa alisikia nyerere akimkataa Lowassa, sasa sijui kwenye hayo maongezi kana ni kweli yeye alialikwa kama nani? vijana wa WAMA bana mna tabu sana aisee....... kuhusu utajiri alishajibu kuwa yeye ana utajiri wa watu na kweli hili liko wazi kuwa Lowassa ana nguvu ya watu........Pili tokea akiwa mtumishi akipata shilling 10 anajitaidi kusave shillingi 7 na kutumia 3, hiyo shillingi 7 shillingi 5 aliingiza kwenye biashara ili iweze kuzalisha sasa kama wengine walikuwa wanapata ela then wanazidisha wanawake unategemea nini.....ndio mana leo hii vijana tujifunze kutoka kwa Patrick Ngowe kutoka kuuza vocha mpaka billionea naye baada ya miaka kumi tutasema ni fisadi....Think Big
 
wengine ni: Weston Songoro, Pipitofitamu, Mzizi wa mbuyu, Simiyu yetu, Mjepo, na they have nothing worth to say than attacking personality.... Nawasikitikia kwani bano wametawaliwa kifikra.

Hao vijana wa WAMA hawana jipya.....mgombea wao hauziki kabisa wamejitaidi sana lakini wapi hauziki......wanasubiria mke wa rais awabebe, Mwai Kibaki anamsemo wake anakuambia BURE KABISA yani rais wa zaidi ya millioni 46 tuchaguliwe na mke wa rais please and please tuwe serious jamani....hatujawa disparate kiasi hicho mpaka mke wa rais atuchaguliye rais wa 2015
 
Bwana john okello ni vema umetufafanulia zaidi ili tuweze kumjua kiundani zaidi mh edward lowassa mana tulikuwa na mkanganyiko na madai mbambali dhidi ya muheshimiwa tunakuomba uzidi kutujuza mana wengine tunaamini kuwa mti wenye matunda hupigwa mawe ..... hata hao wanao mkashfu wanajua kabisa lowassa ni kiongozi shupavu....
 
Nani amekudanganya kuwa raisi ajaye atatoka ccm?

Mkuu EL au Magufuli wakipitishwa na chama haina ubishi atatoka ccm......ila ukileta sijui Membe (mgombea wa mama Salma), Wassira, Migiro, Kigwangalla, Makamba amini usiamini ifikapo saa nane watu wakiwa wanatoka makanisani tayari mtaa wa Ufipa wanasherekea ushindi wa Dr Slaa kuwa rais wa 2015....
 
Bwana john okello ni vema umetufafanulia zaidi ili tuweze kumjua kiundani zaidi mh edward lowassa mana tulikuwa na mkanganyiko na madai mbambali dhidi ya muheshimiwa tunakuomba uzidi kutujuza mana wengine tunaamini kuwa mti wenye matunda hupigwa mawe ..... hata hao wanao mkashfu wanajua kabisa lowassa ni kiongozi shupavu....

Tena uzuri hajatukana mtu wala kutoa kashfa kama wale majamaa wa WAMA wanavyofanya.....tujuze zaidi Mr Okello
 
Well spoken,hizo hoja ulizoainisha hapo juu kuna mtu anaitwa Chabruma, amekomaa nazo kila uchao yeye anaandika tu thread zisizo na ushahidi kwa kutumia hizo hoja dhaifu hapo juu akishirikiana na ndugu yake Lizaboni, na hotlady,

Hhahahaha Mkuu mtende saizi uwawezi kuwaona watakuja saa usiku.... wako ulaya kwaiyo tunapishana masaaa, bado wanakomalia kutafuta ripoti ya afya ya EL....juzi walifukuzwa katika ile hosptali so walichofanya wameingia mtaani na kutengeneza ripoti feki wakiongozwa na Jack Gotham
 
Back
Top Bottom