Mh. Dk Mwakyembe chukua hatua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Dk Mwakyembe chukua hatua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FILOMBE, Jul 10, 2012.

 1. F

  FILOMBE Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wana JF.

  Kwanza nianze kwa kukupongeza Mh. Waziri kwa hatua ambayo umeanza kuichukua, yaani hatua ya kuongoza wizara kwa kutoka Ofisini na kutizama matatizo ya wananchi yanayowakabiri yaliyo chini ya Wizara yako, kwa kweli hiyo ni hatua nzuri kabisa.

  Kwanza kabisa ulianzia pale TRL kwa kusafiri na Treni kutoka DSM hadi Dodoma na wewe kujionea mwenyewe hali ya usafiri wa reli ndani ya nchi yetu Tanzania, na jana nasikia tena umefanya ziara ya kishtukiza pale katika kituo cha mabasi cha Ubungo kwa mabasi yanayoenda Mikoani, ama kwa hakika mie nakupongeza sana.

  Sasa ndugu yangu Mh. Waziri nakuomba uangalie na uchukuzi wa abiria ndani ya jiji la Dar es Salaam. Mh. Waziri hali ya usafiri katika jiji la Dsm unatisha ndugu yangu. Mie binafsi nashindwa kuelewa ama ni kuongezeka kwa abiria yaani wakazi wa jiji au kupungua kwa wawekezaji katika kuwekeza kwenye usafiri huu wa daladala. Ziara yangu binafsi ilianzia jana jioni ambapo nilitokea maeneo ya katikati ya jiji, safari yangu ikianzia mnamo majira ya saa 1 jioni, kulekea Tabata, mh Waziri huwezi kuamini mbali ya kuchelewa kufika mwisho wa safari yangu pia ilinilazimu kutumia mabasi/daladala 4 hadi kufika Tabata yaani Posta-Bugurunu gari 1, Buguruni-Tabata Reli gari la 2,Tabata Reli-Tabata bima gari la 3, Tabata bima-Tabata Segerea basi la 4.

  Katika mlolongo huo magari yalikuwa ya shida na kugombania na hivo kumaliza safari yangu mnamo majira ya saa 5. Ziara yangu vivyo hivyo leo asubuhi hali ni hiyo hiyo, kufika kituoni saa 12 asubuhi na kufika mjini saa 2 asubuhi.

  Mh. Waziri hali ni mbaya sana, ninakuomba pia na wewe katika dhana ile ile ya kuongoza wizara kwa kutoka na kutambua matatizo ya Wananchi, ujongee na kujaribu pia usafiri wa daladala ndani ya Jiji hili la Dar es Salaam. Mh. Waziri karibu ili kwa pamoja tuone ni kwa jinsi gani maisha haya ya wakazi wa Jiji hili la Dsm yanavozidishwa ugumu.

  Fanya kitu Mheshimiwa Mwakyembe na wakazi hawa wa Dsm watakukumbuka kama, tunavyowakumbuka majemedari waliopita katika jiji hili Mh. Keenje, na Mh Mwaibula. Karibu Mh.
   
 2. Ufipa-Kinondoni

  Ufipa-Kinondoni JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 4,488
  Likes Received: 2,147
  Trophy Points: 280
  For my believe, Mwakyembe is very smart but the system is very vague. Hiki anachofanya kinaweza kikawa cha kuwafurahisha wananchi wa hali ya chini. Wananchi tunalia kwa sababu hatuji kesho ikoje lakini wezetu haya siyo kazi mfumo umesimamia unyonyaji wa Watz.

  Hii inamanisha ninin basi! Wenye vyombo vya usafiri wanakula na mfumo wa na ndio wanawalinda kwa gharama kubwa sana. Mwakyembe anajitahidi lakini nyuma kuna watu wanamcheka.

  Hawazeikupigana na mfumo uliomuweka.
   
 3. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Utamaliza kuni kwa kuchemsha mawe huyo nae dhaifu tu hawezi leta changes katika system ambayo ni corrupted,,ccm na serekili yake ni failurer na vimeshindwa kabisa,,ni mamaneno mengi kuliko vitendo.
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hana lolote anatafuta cheap popularity kwenye Treni na daladala atakuja kufia huko ohooo!!!!!!!!!!
   
 5. Ally Kanah

  Ally Kanah JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 1,433
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Wivu wa kishamba huo
   
 6. Ufipa-Kinondoni

  Ufipa-Kinondoni JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 4,488
  Likes Received: 2,147
  Trophy Points: 280
  Mhe Mangungo,

  Unachosema nakubaliana nawe ila ujuwe kuwa TZ inakufa kwa sababu ya kukosa wasimamizi wa sheria ambay inatokana na uzembe mkubwa unaoonyehwa na viongozi wetu katika kuwaajibisha wavunja sheria kwa misingi ya sheria iliyowekwa kisheria.

  Hivyo, cha kufanya kama mzee ananyofanya ingawa inahitaji umakini mzuri zaidi kwa sababu vingine ni vitumbua vya wakubwa haohao.

  Ansateni
   
 7. RICARDO KAKA

  RICARDO KAKA JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 867
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Mwanzo mzuri kwa Dkt. Mwakyembe. pia jaamani naomba kuulizia nauli kamili za mikoani, kama Dar-mbeya, dar-arusha na mikoa mingine, maana nimesikia kuwa amekata mkwara kuwa dar_mwanza ni tsh. 30,000/= aliyesikiliza huo mkwara anipe taarifa kamili.


  "HODI YA CHOONI HAHIITIKIWI KARIBU"
   
 8. Ngangasyonga

  Ngangasyonga JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2012
  Joined: Sep 13, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BIG UP! My Bro. Mwakyembe, tungepata mawaziri kama Mwakyembe na Magufuli japo watano tu, angalao kungekuwa na mabadiliko, kilio cha daladala ningemshauri Mhe.Mwakyembe afufue UDA, wenye daladala wana operate wanavyotaka, wanaangalia pesa na sio huduma kama serikali inavyotegemea pia magari ni machache sana watu ni wengi ukijumlisha na wanafunzi.
  MHE. MWAKYEMBE FUFUA UDA, UDA, UDA- WATU WA DAR WANATESEKA KWA USAFIRI HASA ASUBUHI NA JIONI.
  Nawakilisha!!!
   
 9. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,168
  Likes Received: 1,103
  Trophy Points: 280
  Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, akizungumza na waandishi habari mbele ya abiria na wahudumu wa mabasi kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam jana. Mwakyembe alifanya ziara ya kushtukiza kufuatia ripoti kuwa nauli za usafiri wa mabasi ya mikoani zimepanda maradufu kwa kile kinachodaiwa na watoa huduma ni ongezeko la abiria katika kipindi hiki ambapo wanafunzi wanarejea shuleni kutoka likizo ndefu..

  UShauri wa Bure;

  Vijana tupo tunaweza ondoa wazee ofcn; Hawawezi kuamuka asubuhi stendi kukagua.

  TANGAZA KAZI KWA VIJANA;
   

  Attached Files:

 10. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  aiseeee.....
   
 11. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  hana lolote...analeta mambo ya mzee wa kiraracha enzi zake akiwa naibu waziri mkuu.

  nchi haiwezi kwenda kwa biashara ya zima moto.
   
 12. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #12
  Jul 10, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tatizo letu hatu-appreciate pale mtu anapofanya juhudi kutatua matatizo-tunawavunja moyo wanaojituma, kama hatuwezi kupongeza wanaothubutu sasa tofauti yao na wachumia tumbo itakuwa nini?
   
 13. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Kujituma kwa kwanza ni kujitenga moja kwa moja na mafisadi nakuhakikishia hata afanye ziara kama hizo 100 hapo Ubungo tatizo litabaki palepele. Si unakumbuka kuwa Jangwani alitangaza kuanza na daladala zimemshinda sasa ana rukia Ubungo. Kwa style za mwakyemebe ataonekana sana katika vyombo vya habari lakini hataachieve chochotena itafika wakati atakuwa akiwakimbia waandishi wa habari mwenyewe kwa kuwa anakurupuka kabla ya kutafiti ukubwa wa matatizo ya sekta husika. ikumbukwe kuwa hata Magufulli anatamba sekta ya barabara tu alipoanzia mwaka 1995 kama naibu waziri ambapo alitumia kipindi hicho kuitafiti sekta hiyo na kuanza kupendekeza mabadiliko ya sheria zinazosimamia sekta ya ujenzi;hata alipokuwa waziri kamili wa ujenzi mwaka 2000 ilikuwa ni muendelezo wa sekta aliyokwisha itfanyia utafiti.

  Tazama pale kiraka huyu wa CCM alipopelekwa wizara ya ardhi alichemka kabisa na kuzidiwa kete na mafisadi kama ambavyo Mwakyen=mbe atakavyozidiwa na mafisadi katika sekta hii mpya kwake. inabidi tumpatie muda wa kuisoma na kuijua sekta hii
   
 14. M

  MVENGEVENGE Senior Member

  #14
  Jul 11, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Toka lini sumatra waende wakajikague wao ni sehemu ya ufisadi unaendelea pale, otherwise wangechukua hatua siku nyingi. tumekufa kila sehemu !
   
 15. M

  Mpalisya Imbogo Member

  #15
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Inaonyesha unaogopa sana kufa. Kufa kupo tu hata ujifiche wapi. Heri ufe ukiwaa shujaa na ukaacha alama ktk kizazi kijacho. Una uhakika gani kuwa wewe hutakufa? Na inawezekana wewe ni mgonjwa zaidi bila kujijua. Acha kufuru, Mungu ndio amepanga kifo wala sio mwanadamu.
   
 16. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280

  Sumatra ni Genge la wahuni.
  Nenda Ubungo terminal ndogo ya kwenda Kimara na Mbezi mara tu inapofika saa tatu usiku utasikia nauli ya Mbezi shilingi 500, tena wanakwambia hata ushuke kituo kinachofuata utalipa 500.

  Kama hiyo haitoshi nenda POSTA na Kariakoo ikifika mida ya kuanzia saa kumi jioni utasikia nauli mbezi elfu moja.

  Inapofika mida hiyo huwezi kuwaona Sumatra wala Trafic ktk maeneo hayo niliyokutajia.
  Na hata ukigoma kulipa nauli hiyo Konda na Dereva wanakuwa na kiburi na wanasema wazi nenda kokote unakotaka...

  Dah
   
 17. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280

  Huyu mzee wa Kiraracha amepelekea mrungi uitwe haramu....sina hamu nae
   
 18. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  mkuu naamini kazi ya kiongozi ni kuonyesha njia, yeye mwenyewe hawezi kufanya kila kitu, ni lazima aonyeshe kinachotakiwa na waliobaki kuendeleza kuanzia hapo-sasa kwa kuwa hawaendelezi zile juhudi zinazoanzishwa ni jukumu letu sisi kuonyesha kwamba tunaridhika na kitu fulani huenda waliopo pembeni, chini yake au hata juu yake wataona aibu na kubadilika. Endapo nasi tutabakia kwenye mkumbo huu wa kudharau hata mazuri machache yanayofanywa na baadhi ya viongozi wachache tulionao, viongozi dhaifu tulionao hawataamka toka kwenye usingizi mzito walimolala!
   
Loading...