Mh. Bashe unawadanganya wakulima

Mkuu mimi ni miongoni mwa wakulima wa mahindi..na huwa sikubaliani na walanguzi kununua mahindi yangu.
Kilimo changu ni cha kisasa(IRRIGATION FARMING)huwa natumia mbegu aina ya CARGIL kwa kupanda na inakua ndani ya kiezi mi3 tu,kisha navuna.
Namshkuru mungu huku kwetu mahindi yana bei ya juu na nimeuza kwa raha zangu zote.
Yana bei kubwa yapo mikononi mwa wafanyabiashara siyo kwa wakulima.
 
Hakuna anayetoa solution wote mnalalamika
mlitaka waziri afanyaje
Au wafanye kama korosho?

Binafsi nimeona kutoingilia bei ni hatua nzuri ya awali

Hatua inayofuata sasa inatakiwa wakulima wajengewe uwezo/ wapewe elimu ya uhifadhi wa mazao na kutafutiwa masoko ya nje ili kushindanisha na soko la ndani.

Serikali lazima iwekeze kwenye kilimo itoe ruzuku misimu yote ya kilimo ili kupunguza gharama za uzalishaji

Serikali / wizara ya kilimo lazima ijikite kutafuta masoko ya nje ili kuwapa wakulima fursa ya kuuza mazao kwa bei nzuri zaidi na sio kufunga mipaka

Serikali isiishie kukusanya kodi tu ni jukumu la serikali kutoa elimu, pembejeo na kuboresha miundombinu ili kupunguza gharama na kuongeza uzalishaji
 
Kauli ya Mheshimiwa bungeni kuwa bei iliyopanda ya mahindi ni faida kwa wakulima hakika si kweli na uwazi kuwa hujui tabu za wakulima.

Mahindi huanza kuvunwa mwezi wa 4 hadi wa 7 na ndiyo miezi ambayo wakulima huhitaji mazao yao yanunuliwe na serikali au na wafanyabiashara kwa bei nzuri ili waweze kulipa ada na mahitaji mengine.

Kwa bahati mbaya, serikali hainunui bali huwaachia wafanyabiashara wanaonunua kwa bei ya kunyonga na wakati huu wakulima maghala yamekauka wananunua mahindi waliyouza mteremko kwa walanguzi.

Leo Waziri anasema mkulima anafaidika wakati sio kweli, anayefaidika ni mfanyabiashara kwa sasa. Waziri usipende kupata sifa za uongo wakati serikali kuhusu kilimo ilishachemka.

Mahindi yote yanayouzwa bei ghali yanatoka katika maghala ya wafanyabiashara na sio wakulima.

Waziri rudi ukajiridhishe sioni mipango mizuri ya kumuokoa mkulima zaidi ni propaganda tu.
Mkuu tukiachana na mabadiliko ya tabia nchi kumbuka mazingira ya kibiashara yanatengenezwa na forces mbili,demand na supply ambazo mfanyabiashara anacheza nazo. Na ili uweze kufanya hivyo unahitaji mtaji mkubwa ambao siyo rahisi mkulima wa kawaida kuwa nao. Wafanyabiashara wanachokifanya ni sahihi kabisa katika soko huria unatengeneza demand kwa kununua mzigo mkubwa kipindi supply ikiwa kubwa unahifadhi baadae unakuja kuuza kwa faida. Hizi stori za sijui kangomba,bei elekezi ni siasa za kutafuta wapiga kura kwa kuwa wengi ni wakulima wadogo ila soko huria halina features hizo
 
Kama serikali inalenga kumuinua mkulima basi serikali ndye awe mnunuzi wa mazao yote ya wakulima , kisha waone kama kuna kijana atatembea na bahasha ya kaki barabarani kuomba tena kazi
 
Wawezeshwe mara ngapi? Siku zote wanaambiwa jikusanyeni mshirikiane mkachukue mikopo bila riba. Huyajuwi hayo? Hayajaanza leo.
Hujui chochote kuhusu kilimo cha kujikimu na wakati mwingine si lazima uchangie
 
Mleta mada bado upo mbali sana. Mahindi siku hizi yanavunwa mara 4 kwa mwaka. Anza kulima kisasa ufaidike, achana na mazoea.
Wewe nawe umekuwa lopolopo tu siku hizi. Hujui lolote kuhusu kilimo cha vijijini.
 
Wawezeshwe mara ngapi? Siku zote wanaambiwa jikusanyeni mshirikiane mkachukue mikopo bila riba. Huyajuwi hayo? Hayajaanza leo.
Hawa wakulima wanahitaji elimu sahihi kulingana na mabadiliko ya tabia ya nchi, wanahitaji masoko ya uhakika na hili ndio tatizo kubwa mara nyingi wanalima vizur tatzo ni soko na hapa wanufaika wakubwa ni wafanyabiashara wanaenda kulangua mazao kwa wakulima.
Kuongeza thamani mazao yao(value addition) wanaofanya hivi ni wachache sana.
Mazao yao mengi hayana ubora hivyo hata sokoni ni bure tuuh
Usitegemee kumpa mkulima mkopo ukafkir tayar umemalza matatizo yake yote. Kilimo cha miaka ile na miaka hii ni tofauti kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom