Mh. Alli Kessy nusura apigwe na wabunge wenzake

Attachments

  • dog-mini-300x297.jpg
    dog-mini-300x297.jpg
    9.1 KB · Views: 269
Umesahau mwamba wabunge wa ccm zanzibar wote ni watanganganyika

Huo ni ukweli wa wazi Mkuu,Tukumbuke kuwa CCM zanzibar ni ASP nimesoma kitabu cha "Kwaheri ukoloni kwaheri uhuru",Afro Shirazi walipowachagua watu 14 ambao walikuwa ndio wennye maamuzi yote ya zanzibar(memba wa baraza la mapinduzi) walihakikisha wale wote waliokuwa memba wana asili ya bara kwasababu walikuwa hawaamini wazanzibari asilia, na hali inaendelea hivi hivi mpaka leo...
 

simplemind, nawe ni mzenji!!! maana wao wanalipenda sana hilo neno. Namkumbuka Asha Bakari (ndiye wewe nini?) Labda kama sijakuelewa vizuri kwa neno hilo "fyata" ni hayo tu mkuu, lakini Kessy amepasua jipu watu watulie akamue kidonda kipone.
 
Nawashangaa hawa Wabunge Wazanzibari, Ally Kessy jana kawasaidia sana lakini kwa fikra zao finyu hawakuliona hilo.

Nani kakudanganya wanataka msaada wa aina hii.hawataki kabisa.Nani asyetaka kuishi katika nchi hata ndogo kiasi gani ambapo kila famili ina kiongozi ama kwenye bunge,baraza la wawakilishi,NEC ya chama kimojawapo au Serekalini smz na jmt.Kimsingi Wazenj wanachumia kivulini
 
Hapa ndio unaona wabunge wa ccm walivyondumila kuwili. Wakiwa kwenye lile bunge wanaunga mkono msimamo wa wallio wengi, wakifika huku wanalalamika Z'bar hawachangii na wanabebwa. Sijui wanafikiri haya yatabadilika yenyewe tu bila ya kufanyiwa kazi!. Mahali pa kufanyia kazi ndio pale, nafasi ndio hii. Fungukeni acheni kufuata mkumbo hata kama hamridhiki, nyie ndio mtakaosaidia kuleta mabadiliko na kuwa na muungano wenye furaha pande zote.

Kasoro hii na zingine zinahitaji mfumo ulio wazi, mpaka wakati tulionao mfuko wa serekali 3 ndio unaonekana kuwa jibu!.
 
Kuna utapeli mkubwa sana juu ya mambo ya muungano, binafsi siwaelewi hao CCM kwa kug'ang'ania muundo wa serikali 2 ambao ndo mwanzo wa matatizo yote hayo. Bila shaka kuna wizi na ujanjaujanja wa kila namna ndani ya muundo wa serikali 2.
Namshangaa huyo Kessy kuwalalamikia wazanzibar wakati akijua chama chake kinaunga mkono muundo huo huo wa kitapeli. Kessy acha kuwalaumu wazanzibar kakilaumu chama chako ambacho hakitaki kutumia fursa ya mabadiliko ya katiba kusawazisha utata wa muungano tulio nao.

Munajitapa sisi ni waumini wa serikali mbili bila kutuonyesha ni mapato gani yatokanayo na muungano? kama siyo wizi ni nini. Kessy anajitia anasema ukweli ebu atueleze ukweli juu ya muundo wa serikali 2 wanazolazimisha zijadiliwe kwenye rasimu ya katiba wakati hazijaandikwa popote

Mkuu naungana na wewe lakini hata swala la serikali 3 bado litakuwa na utata itakapofika uchangiaji wa serikali ya muungano kwa upande wa Zanzibar ambayo bado itabidi ibebwe na Tanganyika, suluhisho hapa ni serikali 1 au kuvunja kabisa muungano


Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
attachment.php

mbunge wa nkasi kaskazini, ali mohamed kessy (kushoto) akiwakwepa wabunge wa cuf, kombo khamis kombo (kulia)
na ibrahim mohammed sanya (wa pili kushoto) walipokuwa wakimfokea nje ya ukumbi wa bunge mjini dodoma jana


dodoma.kelele, kukunjana na kunyoosheana vidole jana mchana vilitawala nje ya ukumbi wa bunge wakati wabunge wa cuf kutoka zanzibar walipotaka ‘kumkanya’ mbunge wa nkasi kaskazini (ccm), ally keissy.

Sakata hilo la aina yake lililodumu kwa takriban dakika 15 lilitokea saa 7:05 mchana baada ya naibu spika, job ndugai kuahirisha kikao cha bunge.

Wabunge hao mussa haji kombo (chakechake), kombo khamis kombo (magogoni) na muhammad ibrahim sanya (mji mkongwe), walitaka ‘kumkanya’ keissy kutokana na kile alichosema alipokuwa akichangia bajeti ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mwaka 2014/15 na kusema zanzibar haichangii katika muungano, hivyo haina haki ya kuhoji mambo ya upande wa pili.

Kauli hiyo licha ya kulalamikiwa na wabunge wote wa cuf kutoka zanzibar kiasi cha kufikia hatua ya kusimama na kuomba mwongozo wa spika, keissy alizidi kuwashambulia na kusema kuwa majimbo ya zanzibar watu wake wanaweza kukusanywa sehemu moja kwa kupigiwa filimbi tu.

“nyie zanzibar idadi yenu ya watu ni asilimia 2.8 ya watu wote wa tanzania. Sasa mnataka kupata kila kitu sawa ili iweje! Mnataka ajira asilimia 21 na watanganyika wakafanye kazi wapi?” alisema keissy.

Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho na wabunge kuanza kutoka nje, wabunge hao wa cuf walikwenda kumsubiri keissy karibu na jengo la kantini.

Mbunge wa kwanza kumvaa keissy alikuwa khamis kombo ambaye kabla ya kumfikia alizuiwa na mbunge wa mpanda kaskazini (ccm), moshi selemani kakoso.

Wakati keissy akishangaa alitokea haji kombo ambaye naye alizuiwa na mbunge wa mikumi (ccm), abdulsalaam selemani amer.

“mimi sitaki kupigana bwana ninachokijua ni kwamba nilikuwa nikichangia mjadala wa bajeti na nilichokisema ni ukweli mtupu,” alisema keissy huku akiwa amenyanyua mikono yake juu na kuondoka eneo hilo.

“wewe (keissy) sijui una nini wewe. Unapenda kutufuata fuata sana watu wa zanzibar. Hivi una nini wewe? Hivi hujui kuwa tanzania ni muungano wa nchi mbili za tanganyika na zanzibar?” alisikika akisema khamis kombo.

Kwa upande wake, sanya hata baada ya wenzake kutawanyika eneo hilo, aliendelea kumlaumu keissy na kuwataka wabunge wa ccm kumuonya.

“anapenda sana kutoa kauli mbaya dhidi ya zanzibar. Jamani mkanyeni mwenzenu haiwezekani kila siku awe yeye tu anayetukashifu bungeni,” alisema sanya huku akitulizwa na mbunge wa kibiti (ccm), abdul jabiri marombwa.

Baadaye keissy alisema: “nimesema ukweli kabisa hakuna jambo hata moja la uongo. Sina kosa hata kidogo kwa sababu nimeonyesha ujasiri kwa kusema ukweli.”

kwa upande wake, haji kombo alisema: “ana kauli za kibaguzi sana na tulitaka kumkanya tu na siyo kumpiga.” alisema mbunge huyo amekuwa akitoa kauli za kibaguzi na kwamba walimvamia kutokana na kupandwa na jazba.

“ndiyo maana siku zote tunasema muungano wa serikali mbili siyo muungano kabisa, ni bora serikali tatu, alichokifanya si kitu kizuri.”

sakata lilivyoanza

sakata hilo lilianza wakati haji kombo akichangia bajeti ya mambo ya nje na kueleza kuwa zanzibar haitendewi haki katika uteuzi wa mabalozi nje ya nchi, akisema haiwezekani iwe na asilimia 1.3 ya mabalozi 34 wa tanzania.

“bajeti hii ipo katika mambo ya muungano lakini zanzibar ina mabalozi wanne tu, huku ni sawa na kuoneana. Tanganyika inaifanya zanzibar kama koloni lake. Ndiyo maana tunasema tanganyika imevaa koti la muungano,” alisema kombo.

Ilipofika zamu ya keissy kuchangia mjadala huo alisema: “idadi ya wazanzibari ni asilimia 2.8 ya watanzania wote na wala hamchangii gharama ya muungano kwa miaka 20 sasa. Hao mabalozi wanalipwa kwa kodi za wananchi wa nkasi, biharamulo na dar es salaam.”

keissy alimtaka waziri wa mambo ya nje, bernard membe atakapokuwa akijibu hoja za wabunge aeleze, zanzibar inachangia kiasi gani katika muungano.

“mnasema upande mmoja umevaa koti la muungano, hata sisi (tanganyika) koti hilo limeshaanza kutubana. Kama koti limewavaa amueni moja njia mbona nyeupe, acheni chokochoko zenu,” alisema keissy na kuongeza:

“fedha za mfuko wa jimbo mnachukua mara mbili (kwenu na bara). Kwanza jimbo moja la zanzibar ni kama mawili ya jimbo la nkasi na hata ukitaka kuwaita watu wake unapiga filimbi tu wote wanakusanyika.”

keissy alizidi kuwapandisha hasira wabunge hao baada ya kuwaeleza kuwa zanzibar hailipi umeme unaotoka bara.

“usimchokoze mwehu halafu unakimbilia nyumba ya vioo. Sisi pia tuna uchungu na nchi yetu, hatuna maji wakati kwenu mnasema kila mtu anapata maji na umeme.

Baada ya kauli hiyo haji kombo aliomba mwongozo kwa spika na kabla ya kupewa ruhusa, keissy alisikika akisema, “toa taarifa nitakujibu.”

katika mwongozo wake kombo alisema, “nchi hii haina wendawazimu namna hii. Hii ni nchi yenye heshima na watu wanaoheshimiana.”

kauli hiyo ilimchefua ndugai ambaye alimkatisha kombo na kumtaka aeleze mwendawazimu ni nani. “mwendawazimu ni mtu anayesema maneno yasiyo na busara. Wazanzibari siyo watu maskini na wameingia katika muungano kwa masikitiko makubwa. Kati ya watanzania milioni 45, wazanzibari wapo milioni 1.3 tu,” alisema kombo na kuongeza:

“hakuna chochote mnachotusaidia. Ni aibu mbunge wa ccm, chama ambacho kimekubali kuungana na zanzibar kuzungumza maneno kama haya. Naomba mwongozo wako mheshimiwa spika, mwambie (kessy) asivuke kuja zanzibar.”

hata hivyo, ndugai aliukataa mwongozo huo kwa maelezo kuwa ulikuwa ni taarifa tu na kumtaka keissy kujibu taarifa hiyo. “siikubali hiyo taarifa na namwona yeye ndiyo mwendawazimu zaidi.”

kessy alisema lazima zanzibar ichangie muungano kama inataka kuwa na idadi sawa ya mabalozi kauli ambayo iliwafanya wabunge wa cuf kutoka zanzibar kusimama, huku mbunge wa ole, rajab mbarouk mohamed akiomba mwongozo.

“jamani niacheni nizungumze mbona nyinyi mlizungumza na mkaachwa. Subirini nimalize kuchangia mwiba unatokea ulipoingilia, vumilieni tu na kama hamtaki tokeni nje,” alisema keissy.

Ndugai aliingilia kati na kusema, “naona mmeamua kuleta mada ya bunge maalumu la katiba la mheshimiwa sitta (samwel). Subirini litakapoanza.”

source: Mwananchi

mimi nampongeza sana mheshimiwa kessy kwa kusema ukweli na siku zote amekuwa akisema ukweli na ukweli huu wapinzania hasa cuf wanamchukia bila sababu point ya maana usawa wa ajira haiwezekani maana bara ni wengi kuliko zanzibar. Msema kweli ni mpenzi wa mungu. Mungu atamlinda kessy
 
Sielewi Kwanini wamsubiri nje ya bunge! Kama walikuwa na hoja siwangemjibu ndani ya bunge.
 
Katika ili naona kanikuna, unajua ukitaka kuuma usitumie mdomo bali meno ili umng'ate vizuri asikie maumivu, hawa wazanzibar wanatuona Watanganyika kama hatuna uchungu na Tanganyika yetu
Mh. Kessy huwa ana point sana lakini uwasilishaji wake ni wa kimzaha zaha.
 
Wabunge wa CCM karibia wote wanautindio wa ubongo...

Mioyoni mwao wanaipenda Tanganyika ila wanaishi kwa mawazo ya Vuvuzela Nape na Mzee wa meno ya tembo Kinana..
 
Duh hii hotuba nimepata point 3 tu
1. Koti la muungano hata sisi watanganyika limeanza kutubana
2. Mwiba ulipoingilia ndio unatakiwa utolewe
3. Majimbo ya znz ni madogo watu wanaweza itwa kwa filimbi

Aisee huyu mfipa huyu sijui anapata wapi haya maneno
 
Ni Uhamsho hao,ugomvi wameweka mbele.

Nadhani hauko sawasawa kwa kuwahusisha UAMSHO na ugovi, UAMSHO ni taasisi ambayo imesajiliwa kihalali na serikali ya mapinduzi ya zanzibar kufanya shughuli zake sasa wapi walianzisha UGOMVI? Au kukataa muungano dhalim huu hadharani ndio ugomvi? Tumia akili na maarifa.
 
ukweli kusema zanziba hachangii lolote kwnye muungano? kweli atakaekubali ukweli huu nimjinga tene zaidi hana akili.
sasa mm nauliza mjambazi, wizi wa tanganyika kama zanziba haichangii muungano wale TRA pale badarina unguja na kule pemba pesa wanazozikusanya wanazipeleka wapi? kodi wanayokusanya pale uwanja wa ndege unguja na pemba wanazipeleka wapi?
Misaada kutoka nchi wahisani inaombwa kwa kupitia jina la tanzania, je! kama kusinge kuwa na zanzibar tanzania ingekuwepo?
je! kodi wanazokatwa wafanyakazi wa zanzibar ktk sekta za muungano zinaingi mfuku upi (wa zanziba au wa muungano)? au z
c wananchi wa zanziba wanalipa kodi hizo?
watanganyika ni matapeli, wizi, majambazi tena madhulumati. wanachukua kodi zetu halafu wanasema hatuchangii muungano.
Ndio mana tunataka pawe na mamlaka tatu ili mifuko iwe mitatu kwani sasa hivi kuna mifuko miwili tu wa muungano ambao unakusanya mapato yote yanayotoka ktk sekta za muungano kuto tanganyika na zanzibar.
na mfuko wa zanzibar ambao unakusanya mapato yanayotoka ktk sekta zisizo za muungano kv. karafuu, mwani, samaki, utalii nk.
Sasa tunataka kuwe na mfuku wa tanganyika utakaokusanya mapato ya tanganyika yatokanayo na skta zisizo za muungano kama vile madini, kahawa, korosho nk.
sio tangayika kujichanganya kwenye mfuko wa muungano kisha waseme zanziba haichangii muungano badalayake wao tu ndio wanaochangia huu utakuwa ni ujinga wao wenye kwani sisi hatuja watuma wajichanganye humo.
lla kwa upande mwengine wao watakuwa ni wezi, wanaiibia zanzibar mapato yake halafu hawipi chochote kisha wakidai yite ni yakwao zanzibar hawachangii lolote.
tanganyika acheni wizi zanzibar inachangia muuongano
 
Huo ni ukweli wa wazi Mkuu,Tukumbuke kuwa CCM zanzibar ni ASP nimesoma kitabu cha "Kwaheri ukoloni kwaheri uhuru",Afro Shirazi walipowachagua watu 14 ambao walikuwa ndio wennye maamuzi yote ya zanzibar(memba wa baraza la mapinduzi) walihakikisha wale wote waliokuwa memba wana asili ya bara kwasababu walikuwa hawaamini wazanzibari asilia, na hali inaendelea hivi hivi mpaka leo...

Ikitokea mzanzibari anataka kubishana na mimi kuhusu mambo ya kisiasa, suali la mwanzo namuuliza umeshakisoma hiki kitabu? Kama bado namwambia kwanza kakisome halafu ndo uje ulete hoka zako

Hiki kitabucha kwa heri ukoloni ni kizuri sana kwa ukombozi wetu
 
Back
Top Bottom