Mguu wa mwenye ualbino uliofukuliwa wapatikana

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
15,149
16,229
Tanga. Jeshi la Polisi mkoani hapa limefanikiwa kuupata mguu wa mtu mwenye ualbino, Heri Shehe Kijangwa, ambaye kaburi lake lilifukuliwa na kisha mguu huo kukatwa na wahusika kuondoka nao.

Tukio hilo lilitokea Oktoba mwaka huu katika kijiji cha Tanda, halmashauri ya wilaya ya Bumbuli mkoani Tanga.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Safia Jongo amesema baada ya tukio, polisi walifanya msako na kufanikiwa kuwakamata watu watatu na kisha kuuonyesha mguu huo wakiwa wameufukia katika shamba la mmoja wa watuhumiwa hao.

‘’Shamba hilo lipo umbali wa kilomita 30 kutoka mahali alipokuwa amezikwa marehemu, alisema Jongo.

Kamanda Jongo alisema uchunguzi unaendelea na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani, baada ya upelelezi wa tukio hilo kukamilika.

Katika tukio jingine kamanda huyo amebainisha kuwakamata ‘watoto wa ibilisi’ 117 wenye umri kati ya 12 na 18 wanaounda vikundi vinavyoendesha matukio ya uporaji wa mali na kuwajeruhi watu kwa mapanga.

Amesema baadhi ya watoto hao wamekabidhiwa kwa wazazi wao kulingana na umri wao kuwa mdogo, huku wengine wakifikishwa mahakamani na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali .

Amesema wazazi wanne wa watoto hao walikamatwa, kwa kosa la kushindwa kuwalea watoto wao na wao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom