Mgomo wa Wahadhiri na Wanafunzi UDOM 2011

Mgomo wa Wahadhiri na Wanafunzi UDOM 2011

Sakata la mgomo wa wahadhiri wa chuo kikuu cha dodoma leo limeingia katika sura mpya baada ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) Ludovic Uttoh kuwasili chuoni hapo. Habari za uhakika kutoka udom zinadai kua Uttoh amefika chuoni hapo kufuatia taarifa za kuwepo harufu ya ufisadi dhidi ya pesa za wahadhiri wa chuo hicho. Wahadhiri hao walianza mgomo wa kutoingia madarasani tarehe 10 mwezi huu hadi hapo hoja zao za msingi zitakaposikilizwa na kupatiwa ufumbuzi na waziri mkuu pinda au rais kikwete. Madai ya wahadhiri hao ni pamoja na mshahara mpya ulioanza kutolewa tangu mwezi novemba mwaka jana. Madai mengine ni pesa za kujikimu, mapunjo ya mshahara na kutokuwepo kwenye orodha ya malipo ya hazina kwa walimu wapatao 409. Taarifa kutoka chuoni hapo pia zinadai makatibu wakuu wa wizara za elimu, utumishi na hazina wanatarajiwa kufika chuoni hapo. Hadi mchana huu wahadhiri wanaendelea na kikao chao ambacho amekibatiza jina la kikao endelevu.
 
Awatimue wezi wote wanaowaibia wanataaluma wetu! Hasa huyo Mlacha
 
Mr. Nice aliimba "Kikulacho kumbe kinguoni mwako, kuku kapanda baiskeli Bata kavaa laizoni" wekeni waraka wa UDOMASA hapa tuusasambue vizuri.
Msikubali kuibiwa haki yenu kama ni ya kweli
 
Waraka wa udomasa unapatikana katika thread isemayo tamko rasmi udom. Acheni majungu hapa tunaongelea ufisadi wa hali ya juu, tuelewe pia kwamba harakati hizi hapa udom zilianza 2009 na zikazimwa siku ya kwanza tu kwa walimu watatu kusim amishwa kazi. Hili liliwezekana baada ya kusalitiwa na viongozi wao, mwaka huu tumewashika pabaya, tuelewe kwamba mapinduzi ni mchakato wa muda mrefu., kwa wakati huu tumefikia kilele cha mapinduzi. Tunamshukuru Mungu kwa hapa tulipofika, hebu fikiria kamati tatu zimeundwa tayari na serikali kufuatilia mambo haya, kamati hizi ni ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, kamati ya makatibu wakuu wa wizara na nyingine....
 
Mkuu zilianza nov 2008,
 
Dowans wakubuhu wizi

picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 05 January 2011

dowans_123.jpg

VIGOGO ndani ya serikali wanatuhumiwa kupanga njama za kutaka kuilipa inyemela mabilioni ya shilingi kampuni ya Dowans, kabla taratibu muhimu kuhitimishwa.
MwanaHALISI lina taarifa kuwa Dowans Tanzania Ltd., imewasilisha ankara zake Hazina, tayari kwa malipo kabla maamuzi kusajiliwa mahakama kuu.
Wakati taarifa hizo zikivuja, umetokea utata wa kampuni ipi hasa ya Dowans ilipwe, kwani kuna makampuni mawili yaliyojitokeza.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, kampuni ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) ndiyo ilikuwa na mkataba na Tanesco kupitia kurithi mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond.
Bali uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya Biashara (ICC) wa 15 Novemba 2010, unaagiza Tanesco kulipa Sh.185 bilioni kwa makampuni yote mawili.
Makampuni hayo ni Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Dowans Tanzania Limited.
Utata huo unaongezeka kwa vile wakati wote wa mgogoro wa Richmond na Dowans, hakukuwa na Dowans Tanzania Limited ambayo sasa imetinga katika maamuzi ya ICC.
Nayo kampuni ya Dowans Holdings SA (Costa Rica), hata hivyo iliwahi kutajwa na msajili wa makampuni nchini Costa Rica kuwa haijawahi kusajiliwa nchini humo.
Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wiki mbili baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Dowans ni mradi wa vigogo watatu wakubwa ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa kutoka ndani ya serikali zinasema, mpango wa kulipa makampuni hayo unasukwa kwa ustadi mkubwa na watumishi wawili –mmoja kutoka wizara ya nishati na madini na mwingine ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (AG).
Alipoulizwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo kuhusu njama za kutaka kulipa Dowans kinyemela alisema, "Hapa ninapozungumza na wewe niko Kilosa. Sina taarifa za karibuni za ofisini." Mkullo alikana pia kujua iwapo Dowans wamewasilisha ankara kwa ajili ya malipo.
Kwa mujibu wa sheria za usuluhishi nchini na zile za kimataifa, uamuzi wa ICC sharti usajiliwe katika mahakama kuu ya Tanzania.
Aidha, kwa mujibu wa makubaliano yaliyopo katika mkataba kati ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Tanesco, yote yaliyokubaliwa ndani ya mkataba yatafuata sheria za Tanzania.
Hata hivyo, taarifa zinasema, msukumo wa kutaka malipo hayo kufanywa kinyemela, umefuatia kutajwa katika mwenendo wa kesi, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
"Hapa kuna kitu kinafichwa. Rostam hataki kesi hii isajiliwe hapa, maana jina lake limetajwa ndani ya kesi hii zaidi ya mara tatu. Hivyo anajua kuwa iwapo itasajiliwa ataumbuka," ameeleza ofisa mmoja wa serikali.
Naye mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini amethibitisha kuwa ankara za madai ya Dowans tayari zimewasilishwa serikalini kwa hatua zaidi.
"Bodi ya Tanesco iliarifiwa jambo hili katika kikao chake kilichofanyika 21 Desemba 2010, na kila mmoja alishtuka," ameeleza mtoa taarifa.
Alisema, "…wanaleta ankara za madai hata kabla mahakama kuu haijasajili kesi yao? Hapana! Tukasema, sisi bodi hatuwezi kuidhinisha malipo haya…"
Kutajwa kwa Rostam katika shauri la Dowans kulifuatia kubanwa na majaji wa mahakama hiyo, mfanyakazi wake mmoja kutoka kampuni ya Caspian.
Mfanyakazi huyo aliyekuwa anahudhuria bila kukosa vikao vyote vya mahakama vilivyokuwa vikifanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, alieleza mahakama, "…niko hapa kufuatilia maslahi ya bosi wangu."
Mtoa taarifa anasema, "Yule bwana aliulizwa na wale majaji, mbona kila siku anaingia mahakamani na hatoki mpaka muda wa kesi unamalizika."
Anasema, "Ndipo yule kijana akajibu, ‘nimetumwa na bosi wangukumwakilisha.'" Mahakama ikataka kujua huyo bosi ni nani? Ndipo akamtaja Rostam," anaeleza mtoa taarifa wa gazeti hili.
Anasema mara baada ya kutaja jina la Rostam, majaji waliokuwa wanasikiliza shauri lile, haraka wakauliza, ‘Kwani Rostam ni nani katika Dowans?' Yule bwana akajibu, ‘Ni mwanahisa…'"
Kuna taarifa za kuaminika kuwa mmoja wa watu wawili waliosaini makubaliano ya kuhamisha mkataba kutoka Richmond kwenda Dowans, ni Henry Surtees, Mwingereza anayedaiwa kuwa mtumishi wa kampuni ya Rostam ya Caspian.
Wiki iliyopita, gazeti la kila siku la Mwananchi lilimnukuu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema akisema, Dowans ilisajiliwa nchini Costa Rica na Rostam ndiye aliyepewa nguvu ya kisheria kusimamia malipo hayo.
Werema hakuzungumzia kwa undani hatua ya wanaojiita wamiliki wa Dowans kumpa Rostam nguvu hizo za kisheria.
Tarehe 7 Februari 2008, Rostam alikana kumiliki aina yoyote ya hisa kwenye kampuni mbili – Dowans na Richmond.
Mmoja wa wanaotajwa kuwa wamiliki wa Dowans katika nyaraka za sasa zilizopo ofisi ya usajili wa makampuni (BRELA), Brigedia Jenerali Sulaiman Mohamed Yahya Al Adawi amekana mara kadhaa kuifahamu kampuni hiyo.
Naye raia wa Canada, Andrew James Tice anayeonekana katika nyaraka za sasa za BRELA, aliwahi kuwa meneja uzalishaji katika kampuni ya Songas na baadaye kushika nafasi hiyo katika kampuni ya Richmond.
Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali ambazo gazeti linazo, Tanesco na Dowans wamekubaliana kuwa maamuzi yoyote ya suala hilo, ni lazima yafuate sheria za Tanzania.
Ibara ya 14 ya mkataba wao inasema pamoja na suala hilo kufikishwa ICC, pale ambapo kutatokea mgogoro, bado sheria za ndani ya Tanzania zitatumika wakati wa kufikia utatuzi.
Ibara ya 17 ya sheria ya usuluhishi inasema, mara baada ya maamuzi husika kutolewa, yatasajiliwa na mahakama kuu na baada ya hapo itachukuliwa kuwa ni amri halali ya mahakama ya nchi.
Nchini Costa Rica, ambako Dowans inadaiwa kusajiliwa, hakuna rekodi zozote inazoonyesha kuwapo kwa kampuni hiyo. "Dowans si kampuni halali ndani ya Costa Rica," inasema barua kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali nchini Costa Rica.
Barua hiyo ilisainiwa na Marianela Jimenez, Jumamosi ya 3 Agosti 2008 na kutumwa ofisi ya katibu wa Bunge la Jamhuri, saa 11:09 jioni ya siku hiyo.
Mmoja wa wanasheria nchini ameliambia gazeti hili kuwa serikali haistahili kulipa hata shilingi kwa Dowans kwa kuwa kampuni hiyo ilinunua mkataba kutoka kwa kampuni feki – Richmond.
Amesema, "Hata hatua ya Dowans Holding kuingiza kampuni ya Dowans Tanzania Limited katika madai yao, wakati wakijua fika kwamba kampuni hiyo siyo iliyosaini hati ya kuhamisha mkataba, ni kinyume cha taratibu na sheria za makampuni."
Kampuni ya Dowans ilirithi mkataba kutoka kampuni nyingine yenye utata ya Richmond ambayo ilipewa kazi ya kufua umeme kuanzia Januari 2007 hadi Juni 2008.
 
Dowans wakubuhu wizi

picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 05 January 2011

dowans_123.jpg

VIGOGO ndani ya serikali wanatuhumiwa kupanga njama za kutaka kuilipa inyemela mabilioni ya shilingi kampuni ya Dowans, kabla taratibu muhimu kuhitimishwa.
MwanaHALISI lina taarifa kuwa Dowans Tanzania Ltd., imewasilisha ankara zake Hazina, tayari kwa malipo kabla maamuzi kusajiliwa mahakama kuu.
Wakati taarifa hizo zikivuja, umetokea utata wa kampuni ipi hasa ya Dowans ilipwe, kwani kuna makampuni mawili yaliyojitokeza.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, kampuni ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) ndiyo ilikuwa na mkataba na Tanesco kupitia kurithi mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond.
Bali uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya Biashara (ICC) wa 15 Novemba 2010, unaagiza Tanesco kulipa Sh.185 bilioni kwa makampuni yote mawili.
Makampuni hayo ni Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Dowans Tanzania Limited.
Utata huo unaongezeka kwa vile wakati wote wa mgogoro wa Richmond na Dowans, hakukuwa na Dowans Tanzania Limited ambayo sasa imetinga katika maamuzi ya ICC.
Nayo kampuni ya Dowans Holdings SA (Costa Rica), hata hivyo iliwahi kutajwa na msajili wa makampuni nchini Costa Rica kuwa haijawahi kusajiliwa nchini humo.
Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wiki mbili baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Dowans ni mradi wa vigogo watatu wakubwa ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa kutoka ndani ya serikali zinasema, mpango wa kulipa makampuni hayo unasukwa kwa ustadi mkubwa na watumishi wawili –mmoja kutoka wizara ya nishati na madini na mwingine ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (AG).
Alipoulizwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo kuhusu njama za kutaka kulipa Dowans kinyemela alisema, “Hapa ninapozungumza na wewe niko Kilosa. Sina taarifa za karibuni za ofisini.” Mkullo alikana pia kujua iwapo Dowans wamewasilisha ankara kwa ajili ya malipo.
Kwa mujibu wa sheria za usuluhishi nchini na zile za kimataifa, uamuzi wa ICC sharti usajiliwe katika mahakama kuu ya Tanzania.
Aidha, kwa mujibu wa makubaliano yaliyopo katika mkataba kati ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Tanesco, yote yaliyokubaliwa ndani ya mkataba yatafuata sheria za Tanzania.
Hata hivyo, taarifa zinasema, msukumo wa kutaka malipo hayo kufanywa kinyemela, umefuatia kutajwa katika mwenendo wa kesi, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
“Hapa kuna kitu kinafichwa. Rostam hataki kesi hii isajiliwe hapa, maana jina lake limetajwa ndani ya kesi hii zaidi ya mara tatu. Hivyo anajua kuwa iwapo itasajiliwa ataumbuka,” ameeleza ofisa mmoja wa serikali.
Naye mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini amethibitisha kuwa ankara za madai ya Dowans tayari zimewasilishwa serikalini kwa hatua zaidi.
“Bodi ya Tanesco iliarifiwa jambo hili katika kikao chake kilichofanyika 21 Desemba 2010, na kila mmoja alishtuka,” ameeleza mtoa taarifa.
Alisema, “…wanaleta ankara za madai hata kabla mahakama kuu haijasajili kesi yao? Hapana! Tukasema, sisi bodi hatuwezi kuidhinisha malipo haya…”
Kutajwa kwa Rostam katika shauri la Dowans kulifuatia kubanwa na majaji wa mahakama hiyo, mfanyakazi wake mmoja kutoka kampuni ya Caspian.
Mfanyakazi huyo aliyekuwa anahudhuria bila kukosa vikao vyote vya mahakama vilivyokuwa vikifanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, alieleza mahakama, “…niko hapa kufuatilia maslahi ya bosi wangu.”
Mtoa taarifa anasema, “Yule bwana aliulizwa na wale majaji, mbona kila siku anaingia mahakamani na hatoki mpaka muda wa kesi unamalizika.”
Anasema, “Ndipo yule kijana akajibu, ‘nimetumwa na bosi wangukumwakilisha.’” Mahakama ikataka kujua huyo bosi ni nani? Ndipo akamtaja Rostam,” anaeleza mtoa taarifa wa gazeti hili.
Anasema mara baada ya kutaja jina la Rostam, majaji waliokuwa wanasikiliza shauri lile, haraka wakauliza, ‘Kwani Rostam ni nani katika Dowans?’ Yule bwana akajibu, ‘Ni mwanahisa…’”
Kuna taarifa za kuaminika kuwa mmoja wa watu wawili waliosaini makubaliano ya kuhamisha mkataba kutoka Richmond kwenda Dowans, ni Henry Surtees, Mwingereza anayedaiwa kuwa mtumishi wa kampuni ya Rostam ya Caspian.
Wiki iliyopita, gazeti la kila siku la Mwananchi lilimnukuu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema akisema, Dowans ilisajiliwa nchini Costa Rica na Rostam ndiye aliyepewa nguvu ya kisheria kusimamia malipo hayo.
Werema hakuzungumzia kwa undani hatua ya wanaojiita wamiliki wa Dowans kumpa Rostam nguvu hizo za kisheria.
Tarehe 7 Februari 2008, Rostam alikana kumiliki aina yoyote ya hisa kwenye kampuni mbili – Dowans na Richmond.
Mmoja wa wanaotajwa kuwa wamiliki wa Dowans katika nyaraka za sasa zilizopo ofisi ya usajili wa makampuni (BRELA), Brigedia Jenerali Sulaiman Mohamed Yahya Al Adawi amekana mara kadhaa kuifahamu kampuni hiyo.
Naye raia wa Canada, Andrew James Tice anayeonekana katika nyaraka za sasa za BRELA, aliwahi kuwa meneja uzalishaji katika kampuni ya Songas na baadaye kushika nafasi hiyo katika kampuni ya Richmond.
Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali ambazo gazeti linazo, Tanesco na Dowans wamekubaliana kuwa maamuzi yoyote ya suala hilo, ni lazima yafuate sheria za Tanzania.
Ibara ya 14 ya mkataba wao inasema pamoja na suala hilo kufikishwa ICC, pale ambapo kutatokea mgogoro, bado sheria za ndani ya Tanzania zitatumika wakati wa kufikia utatuzi.
Ibara ya 17 ya sheria ya usuluhishi inasema, mara baada ya maamuzi husika kutolewa, yatasajiliwa na mahakama kuu na baada ya hapo itachukuliwa kuwa ni amri halali ya mahakama ya nchi.
Nchini Costa Rica, ambako Dowans inadaiwa kusajiliwa, hakuna rekodi zozote inazoonyesha kuwapo kwa kampuni hiyo. “Dowans si kampuni halali ndani ya Costa Rica,” inasema barua kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali nchini Costa Rica.
Barua hiyo ilisainiwa na Marianela Jimenez, Jumamosi ya 3 Agosti 2008 na kutumwa ofisi ya katibu wa Bunge la Jamhuri, saa 11:09 jioni ya siku hiyo.
Mmoja wa wanasheria nchini ameliambia gazeti hili kuwa serikali haistahili kulipa hata shilingi kwa Dowans kwa kuwa kampuni hiyo ilinunua mkataba kutoka kwa kampuni feki – Richmond.
Amesema, “Hata hatua ya Dowans Holding kuingiza kampuni ya Dowans Tanzania Limited katika madai yao, wakati wakijua fika kwamba kampuni hiyo siyo iliyosaini hati ya kuhamisha mkataba, ni kinyume cha taratibu na sheria za makampuni.”
Kampuni ya Dowans ilirithi mkataba kutoka kampuni nyingine yenye utata ya Richmond ambayo ilipewa kazi ya kufua umeme kuanzia Januari 2007 hadi Juni 2008.
 
CCM bwana wanaharibu ata nyumani,iki si ndio chuo ambacho kila kizuri au kibaya cha CCM wao kwao sawa tuu.
Hongereni kwa kuichagua CCM tena muache huo mgomo mara moja hasa wanafunzi
 
Nataka nishuhudie mwenyewe kama CAG anaweza kweli kuwaambia ukweli wakubwa zake, na kumwambia mfalme(serikali) tazama sasa u mtupu na jamii inakucheka
 
Uongozi wa Umoja wa Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dodoma (Udomasa), umeazimia kuipeleka mahakamani menejimenti ya Udom kwa tuhuma za kughushi na wizi wa mishahara yao mipya inayotolewa na Hazina.
Wahadhiri hao walianza mkutano endelevu Jumatatu ya wiki hiii kwa ajili ya kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kuwalipa mshahara mpya ambao ulianza kutolewa na Hazina Novemba, 2010.
Pia, wahadhiri hao walisisitiza kuwa hawataingia madarasani hadi watakapoonana na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kumweleza malalamiko yao.
Hata hivyo, kabla ya kutangaza hatua hiyo ya kwenda mahakamani, iliripotiwa kuwa ujumbe kutoka Hazina ulitarajiwa kwenda Udom Jumanne ya wiki hii kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa mishahara hiyo, lakini ulishindwa kwenda hadi sasa.
Akizungumza na NIPASHE jana, Mwenyekiti wa Udomasa, Paul Loisulie, alisema hatua ya kuyafikisha malalamiko yao mahakamani ilifikiwa kwenye mkutano endelevu ambao uliandaliwa na kuhudhuriwa na wanataaluma kuishinikisha menejimenti kuwalipa haki zao.
Loisulie a lisema mkutano huo ambao umefikia siku ya nne tangu uanze, umeamua kuipeleka menejimenti mahakamani kuwa ndiyo chanzo cha uchakachuaji wa mshahara wao.
“Sisi hatuna shida na Hazina kwa kuwa wao wanatoa mshahara wao kama kawaida, lakini ukifika huku Udom ndo unakuwa tofauti. Kutokana na hilo, tumeamua kwenda mahakamani,” alisema.
Loisulie alisema kutokana na hali hiyo, tayari wameshawasiliana na mwanasheria wao ambaye atasimamia kesi hiyo inayotarajiwa kufunguliwa wiki ijayo.
Alisema mchakato wa ufunguzi wa kesi hiyo bado unaendelea ambapo pia wanaandaa taarifa muhimu ambazo wanatarajia kuziwasilisha kwa mwanasheria wao atakayesimamia kesi hiyo.
“Tutaendelea hivi hadi tunahakikisha haki yetu tunaipata kama wao wamezoea kuchakachua mishahara ya wenzao, basi tutaonana mahakamani,” alisema.
Leo wanatarajia kukutana na mwanasheria wao kuanza mchakato wa kuandaa kesi hiyo.
CHANZO: NIPASHE
 
hali bado ni tete kwani wanafunzi wanaosoma college ya education waendelea kusimamia madai yao huku ikifikia ni wiki 1 huku mgomo hou ukiendelea
 
Acha uendelee kwanza hicho ni chuo cha kata ya CCM!
 
sasa chuo kimempamtu Phd kwa kitu gani ! kama mna matatizo hivyo kuanzia wahadhiri mpaka wanafunzi mnapatia mtu Phd kwa mchango gani? Si ndo nyie mlioenda kumchukulia form ya kugombea urais pia?
Inawezekana sio wote mlifanya hivyo ,ila nyie kama wanazuoni mlitakiwa kuelewa impact ya hayo ...mlitakiwa kusema ni asilimia chache wenye msimamo huo na wana uhuru wa kufanya hivyo jamii ingeelewa sasa mnavyolialia sasa hauwaelewi kwa kweli,

Yeye ni anaweza kufanya mslahi yenye yatekelezwe pia kuwachukulia hatua viongozi wabadhilifu hapo chuoni,,,ila yuko kimya ahahaaaaaaaa kama hizo hela mlizo katwa wahadhiri ndizo zilizotumika kununua t-shirt na kofia mlizokuwa mkichekelea kuvaa.

CCM mnaofata mkombo inabidi mpate displinary action kama hizo ili mpate kutuelewa,mkiletewa tshirt next timekataeni maana ndio hela hizo ,waambieni hapana no thank you hizo weka ili tusipate taabu ya umeme kupanda au maji ama mishahara na mikopo ya shule kuchelewa kwa maana ndizo hizo pesa zitumikazo .

Na huu ni mwazo tu ...
 
Back
Top Bottom