Mgomo wa UDOM: Ni kweli FFU waliua wanafunzi wawili?

Habari za ndani udom zinasema kuwa kuna wanafunzi wawili waliuawa kwenye maandamano, mmoja wao akiwa ni mja mzito. Lakini hili linafunikwa ili skendo hii isiwe isijulikane.

Yuko na mwanafunzi mwingine aliyebakwa na ffu hao hao. Waulizeni wanafunzi udom watawaambia vyema mambo haya. Hii ni dalili ya hatari sana na inapaswa kuundiwa kamati ya uchunguzi ili haki itendeke. Kama jeshi la polisi likianza kutuulia na kubaka watoto wetu basi kinachobaki ni kuwa wakimbizi nchini mwetu. Utamaduni huu ukiachwa ujijenge ni hatari.

Is it!or you are trying to instigate more chaos!!
 
acha uchawi... it is as if ungependa iwe kweli mpate kulaumu watu, na mpate boost ya jitihada zenu za kufanya nchi isitawalike.

Habari za ndani udom zinasema kuwa kuna wanafunzi wawili waliuawa kwenye maandamano, mmoja wao akiwa ni mja mzito. Lakini hili linafunikwa ili skendo hii isiwe isijulikane.

Yuko na mwanafunzi mwingine aliyebakwa na ffu hao hao. Waulizeni wanafunzi udom watawaambia vyema mambo haya. Hii ni dalili ya hatari sana na inapaswa kuundiwa kamati ya uchunguzi ili haki itendeke. Kama jeshi la polisi likianza kutuulia na kubaka watoto wetu basi kinachobaki ni kuwa wakimbizi nchini mwetu. Utamaduni huu ukiachwa ujijenge ni hatari.
 
Nasikia kule hali sio nzuri kunatokea machafuko makubwa hebu tuhabarisheni mliopo Dododma hasa hapo chuoni UDOM

Habari si ndo kama hz?!?kinachotakiwa ni kuzifanyia kazi habari kama hizi! Tetesi za ubakaji na mauaji siku ya mgomo wa wanafunz wa Social mwshon mwa Decemba zimezagaa sana miöngon mwa wanafunzi!wao wenyewe hawawez kuthibitisha kwan inasemekana taarifa zinafichwa!WANANCHI,VIONGOZI WA KADA MBALIMBALI+NA WOTE WENYE MAPENZ MEMA NA WATOTO/WAJUKUU ZETU KULE UDOM!!tuungane kupeleleza hili jambo ili ukweli uwekwe waz na wahusika wachukuliwe hatua kali!UDOSO FANYEN KAZ YENU!
 
Jamani tuache udaku. Habari ziwe za uhakika. Hakuna cha mwanafunzi kufa wala kubakwa. Mwenye uhakika na habari za ndani ataje jina au majina ya marehemu au waliobakwa, kozi wanazosoma, mwaka wanaosoma, kwao wapi na kama wazazi wana taarifa za kupotea watoto wao.

.....
Hii ilishawahi kutokea UDSM wanafunzi walidai kuwa kuna mwenzao amekufa tena mjamzito, waandishi wa habari walikwenda kufuatilia suala hili kila aliyeulizwa kama anajua mwanafunzi aliyekuwa akawa anamaka tu ati kuwa na yeye kasikia kuna mwanafunzi mwenzao kafa lakini hamjui. Haikuishia hapo tu wazushi wakazidi kulifanya suala hili lionekane ukweli wakatunga jina, kozi, mwaka na namba ya usajili ya marehemu ilipofuatiatiliwa ikagundulika kuwa hakukuwa na mwanafunzi mwenye jina lililotajwa hapo chuoni, kwenye kozi iliyotajwa hakuna aliyepotea, wote walikuwepo, namba iliyotajwa ilikuwa ya mwanamme na si mwanamke kama ilivyodaiwa na alikuwa kozi tofauti kabisa na alikuwepo chuoni.

Nchi yetu imekuwa kama tupo vitani, watu huamua kuzusha uwongo ili wateke akili za wenzao ambao wataunga mkono matakwa yao. Tabia hii ya kuzusha zusha tu mambo haifai. Msitufanye kama watoto. Hata sisi tumepitia vyuo vikuu na migomo tumeshiriki na kupigwa na FFU tumepigwa. Kwenye vurumai la FFU kubaka au kubakwa si rahisi
Hii ndio Tanzania mpya MaMkwe! Ukweli hautakikani sana kama uongo unaowafurahisha wengi. Tunasahau kwamba tunaowapinga leo nao watakuwa wapinzani kesho... tunaowatungia uongo leo watakuwa watunga uongo wa kesho, tunaowafurahia leo, tutapingana nao kesho... basi na tujitahidi kuwa wenye kusimama kwenye ukweli kwa Tanzania ijayo.
 
Sasa JF kukaa kiChadema inahusiana vp na mada husika?
Nina mashaka uanafunzi wako, University haiwezi kuwa na mwanafunzi anaecoment pumba kama hizo.
Mdau uliye m'quote hapo juu alikuwa anaomba tu uthibitisho toka kwa member yeyote ambaye ni mwanachuo wa Udom. Sasa wewe badala ya kukanusha tu kuwa habari si za kweli unaita watu wazushi, wanafki na wachochezi.
Baadae unasema "ukweli utajulikana"
Which is which?
Shame on you unayejiita mwanafunzi wa Udom.
Asamehewe bure maana si yeye anayenena bali anajaribu kutekeleza matakwa ya chama yaani ,anadumisha Amani na utulivu aliohubiriwa na ssm na kuufahamu vyema, hivyo kila akiona kitu chenye kuelekea kinyume na mapokeo hayo anakurupuka kutoa kauli kama hizo zenye red.
 
Hamna mwanafunzi aliye kufa udom, ila kuna mwanafunzi mmoja yupo hospitali kutokana na kuchezea kichapo kutoka kwa FFU
 
UDOM hamna vurugu kupo shwali, vijana wanadai haki kisomi na kwa amani huku wakimsubiri kwa hamu Mizengo Pinda tu,
 
UDOM hamna vurugu kupo shwali, vijana wanadai haki kisomi na kwa amani huku wakimsubiri kwa hamu Mizengo Pinda tu,
 
Back
Top Bottom