Kawambwa aliudanganya umma kuhusu mgomo wa UDOM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kawambwa aliudanganya umma kuhusu mgomo wa UDOM

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kombati, Dec 1, 2011.

 1. kombati

  kombati Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ..Naomba nianze kwa kunukuu maneno ya Profesa Isaa Shimvji akielezea wajibu wa msomi katika jamii alipokuwa akizindua kitabu cha MAKUADI WA SOKO HURIA kilichoandikwa na Profesa Seithy Chachage ambaye kwa sasa ni marehemu mnamo octoba 2002 “ wasomi tunao wajibu situ wa kuwawakilihsa kimawazo na kivitendo msimamo na muelekeo wa wanyonge bali pia kuchambua na kuonyesha unafiki wa mawazo na muelekeo wa matabaka tawala” Mnamo tarehe 20 desemba mwaka 2010, hakuna mwana UDOM hata mmoja kutoka college ya social science ambaye haielewi ni nini kilitokea…kufuatia mkutano wa dharula wa wabunge juu ya ni hatma ya baadhi ya kozi anbazo hazina field katika skuli ya sanaa na sayansi za jamii, yaaani kwa kimombo (school of humanities and social sciences)… chini ya rais ambaye binafsi namkubali kuwa mwasisi wa mapinduzi ya kweli hapa UDOM, LEONARD SINGO..serikali ya wanafunzi (UDOSO) iliazimia na kupitisha maamuzi ya kufanya mgomo na maandamano ili kuushinikiza uongozi wa chuo kukubaliana na matakwa ya wanafunzi kuwa kozi zoote ni lazima ziwe na mafunzo ya vitendo yaani (PRACTICAL TRAINING) maarufu kama field. Na kwa moyo mmoja wanafunzi woote walijitokeza kwa nguvu moja kudai haki yao hiyo ya msingi pamoja na kubezwa na baadhi ya viongozi wa college husika wakidai kuwa kama wanafuzi hao wakipata field basi wao wangeacha kazi.
  Binafsi nikiwa ni mhanga wa waliokosa field nilidamka asubuhi na mapema saa kumi alfajiri ili kuhakikisha maandamano hayo hayakwami eti kwa kukosekana kwangu, mguu kwa mguu kuelekea mjini lakini tukakutana na nguvu ya dola inayokanadamizwa na hao bosi zao, hapa namaanisha polisi wa kutuliza ghasia FFU, ndio wanakandanmizwa uashangaaa nini? Kumleta polisi aje anilipue mabomu ya machozi mwanafunzi nisiye na siraha hata moja na ninayedai haki yangu ya msingi halafu umlipe poshoo ya Tsh 2700 kwa siku ni dhuluma tena kubwaa… basi nguvu kubwa ya dola ikatumika kuyatawanya maandamano yale na wakafanikiwa..lakina cha ajaubu na kilichonishtua sana ni ujio wa mawaziri wawili kutoka sirikalini, waziri wa elimu na mafunzo ya ufindi amabye ni mbunge wa bagamoyo bila shaka anakotokea mkuu wa nchii hii ya jamhuri ( Dr Shukuru Kawambwa) na waziri wa mambo ya ndani ambaye ni mbunge wa kuteuliwa ( Ndugu Shamsi Vuai Nahodha) eti kuja kutafuta suruhu ya tatizo letu ili hali jana tu waliagiza tupigwe mabomu kwa maana madai yetu hayana msingi wowote.
  Tukaamshwa saa kumina mbili asubuhi mnamo tarerhe 22, desemba 2010, wakatumia vipaza sauti na spika za kanisa kutamka kile waalichokiita mwafaka uliofikiwa usiku kwenye kikao kati ya, serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo iliwakilishwa na kawambwa, serikali ya wanafunzi (UDOSO) na menejimenti ya chuo…..waziri kawambwa akanena kwa niaba ya serikali kuwa ni haki ya kila mwanafunzi wa chuo kufanya mafunzo kwa vitendo (FIELD) na akaiagiza menejimenti ya chuo kuaandaaa upya mtaala ambao utaonyesha kuwa kozi zote zinafanya mafunzo kwa vitendo na akakazia kuwa (PROSPECTUS) sio kitabu kitakatifu kwamba hakiwezi kubadilishwa, hivo iandikwe upya haraka iwezekanavyo na kupigilia msumali kuwa bajeti au pesa ya kugharamia mafunzo hayo kwa vitendo itatengwa na serikali na hivyo itatolewa moja kwa moja na hazina kuu. Na kwa haraka hatua zingine kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wa mwaka wa tatu na wa pili ambao hawakutakiwa kufanya mafunzo hayo kwa vitendo wanafanyiwa mkakati wa kuhakikisha wanafanya mafunzo hayo mapema mwezi julai na akaongeza kuwa ili mwanafunzi wa chuo kikuu aheshimike kuwa kweli amehitimu shahada ni lazima awe amefanya vit vikuu vitatu

  1. masomo kwa nadharia (theories)
  2. mafunzo kwa vitendo ( practical training)
  3. utafiti (research)
  hali hii ilitufanya wanafumzi woote tuamini kuwa serikali yetu inatujali japo ni mpaka tuikumbushe na tukashangilia kwa nguvu ushindi wa kuipata haki yetu ya msingi na mawaziri hao wakatuomba tuingie madarasani na wao waondoke kwenda kuanza kusimamia haraka iwezekanavyo utekelezaji wa hayo waliyoyasema na kawambwa kutuahidi kuwa atarudi si zaidi ya mwezi mmoja kuja kutupa ripoti ya wapi wamefikia katika utekelezaji huo na ni vip wanafunzi wa mwaka wa tatu watafanya mafunzo hayo kwa vitendo, tena akatuomba sana kuwa ameishaitisha kikao cha pamoja kati ya wizara ya elimu, bodi ya mikopo na tume ya vyuo vikuu (TCU) anasubiliwaa yeye ili kikao kiendeleee hivyo anaomba aruhusiwe akaendelee na shughulia za kutatua tatizo hilo. Kwa kuamini kuwa kilio chetu kimefika mahali husika na kimefanyiwa kazi kwa asilimia thememnini tayarri, wanafunzi wote hatukuwa na kinyongo na hivyo mgomo ukasitishwa na tukaelekea madarasni kuanzia mida ya saa tatu subuhi baada ya kikao hicho na mawaziri..
  tangu tarehe 22, si kawambwa wala nani aliyekuja kuzungumzia utekelezaji wa suala hilo unaendeleaje, hatukupenda sana kuhoji kwa nguvu kwa sababu matumaini ya kufanya hiyo FIELD yalikuwa yanaonekana kwani kulichapishwa kijitabu kilichoitwa THE UNIVERSITY OF DODOMA PRACTICAL TRAINING GUIDELEINES, ambacho kilitoa mapendekezo ni jinsi gani mafunzo hayo kwa vitendo yatafanyika na vile vile juhudi za uongozi wa chuo kutafuta maeneo sehemu mabalimbali za nchi kwa ajili ya wanafunzi kwenda kufanya mafunzo hayo kwa vitendo zilionekana wazi kiasi cha sisi soote kuami kuwa kweli haki tuliyoipigania tumeipata na tukamshukuru mungu wetu na serikali kwa kusikia kilio cha wana UDOM. Tukaendelea na masomo, hususani kujiandaa na mitihani ya jufungia mwaka ambayo ilikuwa ifanyike kuanzia tarehe 20, juni 2011.
  Bumbuwazi, butwaa na mfadhaiko ukatushika mnamo tarehe 9, juni pale kulipobandikwa matangazo ya kuwa hakutakuwa na mafuzo kwa vitendo kwa kozi zile ambazo awali haikuonyeshwa katika prospectus na hivo ni kozi zilezile tajwa tuu ndo zitafanya mafunzo hayo kwa vitendo, hii ilitokana na uamuzi wa kikao cha 22 cha seneti ya chuo ambacho kilikubaliana na maamuzi ya TCU ya kutoruhusu mabadiliko ya mafunzo kwa vitendo kama ambavyo ilipendekezwa na kijitabu cha THE UNIVERSITY OF DODOMA PRACTICAL TRAINING GUIDELINES..ni nini amabacho kingefuata??
  Manaake ni kwamba zile juhudi za kudai haki zetu za tarehe 20 desemba amoja na kupigwa mabomu, na haki hiyo tuliyoahidiwa kuwa tutaipata kwa maneno ya serikali kupitia kwa waziri kawambwa manamo tarehe 22 desema, ni kwamba hiyo haki yetu imeota mbawaaaa???????.
  Hili likawa ndilo chimbuko la mgomo na maandamano ya awamu ya pili yaliyoafanyika mnamo tarehe 10 mwezi wa 6 baada ya wana funzi wote kuafikiana katika kikao cha college baraza amabacho kilifanyika mapema jumapili ili kushinikiza TCU kutengua msimamo wao wa kuwa mabadiliko ni mpaka watakapofanya mapiti ya vyuovyot Tanzania kwa ujumla, swali je ni chuo ganu Tanzania chenye madai kama ya Udom ili Udom wakisubiri kujumuishwa nacho katika maauzi hayo?..Asilimia kubwa ya vyuo vingine wanafunzi woote wanafanya mafunzo kwa vitendo. Mgomo huu ndio uliopelekea kufungwa kwa college hii na kusimamishwa masomo kwa baadhi ya wanafunzi na wanafunzi wote wa mwaka wa pili wanaosoma shahada ya mahusiano ya kimataifa..swali kubwa vichwani mwa wanafunzi hawa wa mwaka wa pili ambalo bado linahitaji kujibiwa ni nini walichokifanya mpaka kusimamishwa kozi nzima mpaka mgonjwa ambaye kwa wakati huo alikuwa hoi ICU ya MOI?..Majibu bado nia magumu nab ado hayajapatikana, KWANINI BAIR?, NINI WAMEFANYA BAIR? NINI NAFASI YAO KATIKA MGOMO HUO?..JE NI BAIR MWAKA WA PILI PEKEE AMBAO WALOGOMA? AU NI WAO TU NDIO HAWANA MAFUNZO KWA VITENDO? AU NI WAO NDIO WALIOPITISHA AZIMIO HILO LA MGOMO? AU NI KWAMBA WAO HAWANA MTETEZI KATIKA MENEJIMENTI? Yanayotajwa kama makosa ya BAIR ni miongoni mwa vitu ambavyo mimi binafsi kama BAIR nilifanyiwa ikiwemo kugongewa mlango kwa fujo asubuhi ili nikaandamane lakini leo imekuwa mimi ndio nimefanya tena?? Bado nashindwa kuelewa nini hasa kiini cha yote haya..POLE SANA KWA BAIR WOTE WA MWAKA WA PILI KWA YOTE MLIOPITIA KATIKA KIPINDI KIGUMU CHA KUWA NYUMBANI BILA KUJUA NINI HATMA YENU NA UDOM…POLE..POLENI SANAAAA.
  Nilimfuatilia kwa makini sana waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi mheshimiwa shukuru kawambwa katika kipindi kinachorushwa hewani na moja ya vituo vya televisheni hapa nchin na nadiriki kusema kuwa ameudanganya umma kuwaaminisah kuwa wanafunzi wa chuo kikuuu cha dodoma walikaidi azimio la serikali ya kuwa ilitengua tamko ya tume ya vyuo vikuu nchini TCU na kutaka kuwa wanafunzi hao wangeenda kufanya mafunzo kwa vitndo na kwamba serikali ilikuwa imetenga pesa kw a ajili ya mafunzo hayo na akasema kuwa serikali ilimtma makam wa chuo idrusa kikula kwenda kutoa taarifa hiyo kwa wanafunzi. Nikiwa mmjo wa wanafunzi waliokuwepo muda ambao makam alifika hosteli hapo yapata saa saba usiku, alisema ya kuwa serikali imeamua na imekubali kuwa wanafunzi watafanya mafunzo kwa vitendo, wala hakusema kuwa serikali imebatilisha maamuzi ya TCU ambao ndio waliosababisha mtafaruku huo baada ya kuzuia mafunzo hayo kwa vitendo, na vilevile akasema kuwa baada ya wao kukaaa na kufanya tathmini walipata jumla ya fedha zinazohitajika kugharamia mafunzo hayo kuwa ni 1.6 bilioni za kitanzania. Sasa rejea katika hansard ya kikao cha bunge la tarehe 13 mwezi wa sita mwaka 2011, tamko la naibu waziri wa elimu juu ya mafunzo kwa vitendo Udom alisema serikali imetenga shilingi nagapi???? Ni shilingi 386 milioni kama kumbukumbu zangu ziko sahih. Sasa ni nani asiye na nidhamu kati ya kawambwa na wanafunzi?. Mimi ninavoona wanafunzi waliendelea kugoma kutokana na vitu vifuatavyo

  1. baada ya kutatua mgooro huo mwaka jana baada ya maandamano ya tar20 desemba, kawambwa alisema serikali imeamua, imeamua serikali haishindwi kitu na kwamba baada ya kuondoka kutoka katika kikao kila na wanafunzi anakwenda moja kwa moja kufanya kikaona TCU pamoja na bodi ya mikopo na angerudi kutoa muielekeo mzima wa ni jinsi gain wanafunzi watafanya mafunzo hayo kwa vitendo, na hajawahi kurudi mapaka leo
  2. TCU wao walitoa tamko wakidai ni chombo huru kisichoingiliwa na chombochochote kile wala serikali, hivo ilikuwa bado ni vigumu kuamini maneno ya kawambwa ikiwa alikuwa hukohuko jikoni iweje akakubaki chakula kiletwe sebuleni kikiwa kibichi???
  3. bajeti iliyotajwa na makamu wa chuo na ile ya wizara ya elimu vina utofauti mkubwa sanaa
  4. bado tatizo kubwa halikuwa hizpo pesa, bali ni tamko la TCU, mbona tangu mgomo mapka leo hajawahi kutamka kuwa TCU ndio waliopelekea mgomao ma badala yake wamekuwa wakisemaa siasa ndio chanzo????
  5. kumuamini kawambwa ilikuwa ni taaaabu hasa baada ya kudanganya umma wa wanachuo desemba mwaka jana kuwa suala hilo limeisha
  6. kawambwa ndiye aliyetoa tamko la kuwa wanafunzi watafanya mafunzo kwa vitendo, kama alikuwa anaamini na ana uhakika na hayo waliuoyomtuma makam mkuu wa cho, kwanini asingeenda mwenyewe muhusika mkuu wa tukio hio na kutoa tamko hilo kwa wanafunzi??, na ni kwanini makamu wa chuo hakutaka kuulizwa swali lolote kuhusu hilo tamko alilotumwa kutoa kwa madai kuwa yeye ni mjumbe tu???.......
  jaribuni kulifuatilia hili jambo kwa makini ndugu mhariri, wanachotaka wananchi waamini sio ukweli halisi wa kilichotokea Udom kwa mtazamo na upeo wangu, serikali iliwadanganya wanafunzi, ilikuwa ni kutaka kufunika kombe mwanaharamu apite.
   
Loading...